Matumizi ya Pemba Yanavyosababisha Mtindio wa Ubongo na Saratani

Matumizi ya Pemba Yanavyosababisha Mtindio wa Ubongo na Saratani

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
Matumizi ya pemba yamebainika kuongeza hatari ya kupata maradhi ya saratani, pamoja na kuongeza uwezekano wa mtoto aliye tumboni kuzaliwa akiwa na mtindio wa ubongo.

Hayo yameelezwa na Dkt. Joseph Mwanga, mhadhiri mwandamizi wa Afya ya Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Bugando (CUHAS), alipokuwa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha habari nchini Tanzania.

Licha ya kuwa pemba hutoa baadhi ya madini, hutolewa kwa kiasi kikubwa kupita kiasi, hali inayochangia hatari ya kupata saratani kwa wanawake wanaojihusisha na matumizi ya pemba.

Aidha, imeelezwa kuwa matumizi ya pemba yamekuwa chanzo cha watoto kuzaliwa njiti, hali ambayo huathiri ukuaji wao wanapozaliwa.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na CUHAS, pemba hutoa madini ya arseniki (arsenic), ambayo yamehusishwa moja kwa moja na chanzo cha saratani kwa binadamu.

Tafiti zinaonyesha kuwa mara nyingi wanawake wamekuwa wakitumia kiasi cha takriban gramu 60 za ugondo kwa siku — kiwango ambacho ni kikubwa mno na hatari kwa afya ya binadamu.

 
Okay, tafiti zifanyike kwa ukweli na uwazi bila kuwa na influence za hovyo
 
Okay, tafiti zifanyike kwa ukweli na uwazi bila kuwa na influence za hovyo
 
Back
Top Bottom