INJECTION TECHNICIAN
JF-Expert Member
- Jan 9, 2020
- 356
- 794
JE, SERVICE ROAD NI KWA MATUMIZI YAPI HASA?
Ni swali ambalo limekuwa linasumbua sana vichwani mwa madereva wengi sana. Kwani si mara nyingi hasa tunaelezwa service road zilijengwa kwaajili ya nini hasa na nani wanaopaswa kuzitumia.
Ukisoma ROAD TRAFFIC ACT hakuna popote inapozungumziwa service road, hata hivyo ukisoma Kanuni za sheria ya barabara yaani The ROADS ACT Regulations za 2009 kuna mahali panazungumzia service road.
Kanuni ya 9(10) ya Kanuni za Barabara inasema kwamba No person shall drive on a service road as a carriageway unless that person intends to access the nearest road of access
Maana yake nini?
Maana yake ni kwamba Hakuna mtu anayeruhusiwa (au ni marufuku) kuendesha kwenye service road kama vile hiyo ni barabara halali, isipokuwa tu kama mtu huyo anataka kutumia njia hiyo kwa ajili ya kufikia barabara ya karibu ya kuingilia [mahali]
Road of access maana yake ni nini?
Road of access maana yake ni barabara yoyote inayowezesha kufika mahali au kuifikia barabara nyingine. [a road giving access to a place or to another road]
Kwa mantiki hii nini hasa matumizi ya service road?
Kwa mujibu wa kanuni ya 9(10) ya Kanuni za Barabara za mwaka 2009, matumizi halali ya service road ni kumuwezesha:
(a) Dereva aliye katika barabara kuu kuweza kuingia kwenye makazi au nyumba za pembeni nje ya barabara;
(b) Kumuwezesha dereva anayetoka katika nyumba au makazi yaliyo nje ya barabara kuingia barabarani. Mfano mtu anatoka pale DANUBE HOME Nyerere road anataka kurudi tena barabara kuu ya Nyerere. Au Mtu anatoka pale NISSAN Vingunguti anataka kurudi tena barabarani kuelekea Mjini kupitia Nyerere road au yupo along Nyerere road anataka kuingia ofisi yoyote iliyopo upande wa kushoto au kulia mwa barabara.
Lakini sio matumizi halali ya service road kwa dereva kwa mfano, kuanza kuendesha gari kutoka pale Caterpillar au sheli ya njia panda ya Chang'ombe kuelekea Tazara kwa kutumia service road huku akizipita Unilver, Bahkressa, Quality Plaza, Toyota, Sigara, Radio Tanzania kisha ndio afike kwenye intersection ya Tazara.
Ni imani yangu umeelewa matumizi sahihi ya service road.
RSA TANZANIA.
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.