Yale yale tu, hujasema chochote ambacho hakijaimbwa humu, kwanza kasome vizuri chanzo chako cha taarifa ufahamu hao Ethiopia tumewazidi kiuchumi pamoja na kwamba liinchi lao likubwa na wana watu wengi ambao ni mara mbili yetu, ni kama mlivyo huko Tanzania, muungano wa nchi mbili na nchi kubwa yenye rotuba kila sehemu lakini maskini wa kutupwa.
Kingine, reli kawaida kama muundo wowote, huwa hatuhesabu mapato tu, tunaangalia na manufaa yanayopatikana wakati jamii inaitumia, jifunze kitu kinaitwa socio-economic benefits.
Nyie reli yenu kasafu ka 200km bado mnahangaika hata sijui mko wapi maporini, leo mnataka mshindane na sisi ambao tulikamilisha zaidi ya 500km na tupo kwenye hatua za kukamilisha safu ya pili. Hayo ya treni kusafiri kwa kasi ya umeme sio kitu cha kupigia debe humu, cha msingi, kwenye mahesabu ya biashara huwa tunazingatia viashiria vingi tu.