Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Mara nyingi mifuko laini na miepesi ya nailoni au Rambo kama inavyojulikana na wengi Tanzania iliwahi kutumiwa na baadhi ya wananchi katika kufungashia chakula na hasa vyakula vya haraka kama chips au wali kwa wale wenye migahawa midogo.
Hata hivyo kuna baadhi ya familia wao walikuwa wakichana mifuko ya nailoni na kuitumia kufunikia vyakula pale wanapokua wakipika kwa imani kuwa inasaidia kuivisha chakula haraka, kwani hufunika vizuri na kuganda kwenye sufuria hivyo mvuke wote hubaki ndani, mfano kufunikia wali, ugali na wakati wa kuchemsha mahindi, viazi au mihogo. Tofauti na mifuko, kumekuwa na matumizi makubwa ya vyombo vya plastiki katika familia nyingi hapa Tanzania. Kwa mujibu wa taasisi ya kilimo na sera ya biashara IATP, plastiki zote zinaundwa kwa kemikali ambayo inauwezo wa kuharibu afya ya mtu moja kwa moja.
Baadhi ya kemikali hizo ni BPA maarufu kama Bisphenol A na DEHA inayojulikana kama Diethylhydroxylamine, kemikali hizi mbili ndo zinatajwa kuhusika na mabadiliko ya tishu, kuharibiwa kwa vinasaba, kuharibu mimba, matatizo wakati wa uzazi na mabadiliko ya homoni. Kwa upande wa watoto kemikali hizo zinatajwa kuharibu kinga yao ambayo inatakiwa kuongezeka hali inayosababisha homoni kubadilika na kusababisha matatizo katika tabia zao.
Kwa Tanzania kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na taarifa mbali mbali zinazoeleza juu ya madhara ya kuweka chakula katika vyombo vya plastiki na zaidi ni mifuko laini ya plastiki.
Mfano: Jumuiya Ya Madaktari Wa Marekani Imetoa Majibu Ya Vyanzo Vya saratani:

- Usinywe Chai Kwenye Vikombe vya Plastic Kuanzia Sasa.
- Usile Chochote Chenye Moto Kilicho Ndani Ya Mfuko Wa Plastic Mfano Mihogo, Viazi.
- Usipashe Chakula Kwenye Microwaves kwakutumia chombo cha Plastic
Ila sasa kuna watu wanapika chapati kwa kutumia sponge, sponge hizi kiukweli ni hatari kwa Maisha, ingawa sijajua kama wanafahamu hilo, mwanzoni wafanyabiashara wengi wa chakula walikuwa wakitumia vitambaa kwa madai kuwa wasiugue na moto wakiwa wanageuza chapati na kadhalika, ila hili la Matumizi ya plastiki sidhani kama ni jambo sahihi sana. Nimepata kuliona Dar es Salaam, Mwanza, Shinyanga na baadhi ya sehemu ya Dodoma.
Ukitumia Microscope tunaweza kuona vitu vya ajabu sana kwenye vyakula vyetu. Wiki iliyoisha nilipata kuzungumza na Rafiki yangu kuhusu mada hii na kuniambia kuwa niache ubabaifu, ila ilimchukua siu tatu tu alikuja kunieleza jambo lile lile. Tukisubiri Mamlaka sidhani kama watafanya jambo ila jamii kama jamii tuna kila sababu ya kuzungumza na hawa wafanyabiashara.
SIO KWA UBAYA! TUMIENI HATA MIKO YA MBAO TU!