Nimetoka kuangalia Video mpya ya Mr bluu "mboga saba" na nasikitika kusema kwamba sijaipenda sio kwamba nyimbo ni mbaya bali ni kwa haka katabia ka wasanii wa Bongo kuwaweka kwenye video Madem weupe(waarabu,wahindi,wazungu na wale wenye muonekano wa light skins). Hii inaonesha ni jinsi gani sisi watu weusi hatujikubali wenyewe na ndo mana sishangai kuona idadi ya wanawake wetu weusi wakijichubua ngozi zao.
Kila Msanii anataka ashoot na dem mweupe. Rejea video za Diamond, Alikiba,Ommy Dimpoz,Blue,Hamonaiza na wengine kibao. Hata hao wazungu wenyewd wanatushangaa kuona jinsi tunavyowanyenyekea. Mfano yule dem alioshuti "Bado" ya Hamonaiza ilitokea ajali kidogo basi dem akagoma, Wacha majamaa wampigie magoti kisa dem mweupe mpaka akakubali na dau wakapandishiwa.
ACHENI USHAMBA WASANII WA BONGO FLEVA
Nakusahihisha kidogo Mkuu,
Directors ndiyo wanapaswa kulaumiwa,
Lakini pia kuna Maeneo ambayo hawa Jamaa wanafanya Shooting Kumpata Model wa Kiafrika Pure ni shughuli,
Kwa hiyo naomba tuweke akiba ya Maneno, Tuwapongeze kwa hatua waliyofikia, halafu Binafsi nawashauri wanamziki waangalie yafuatayo:
1.Kuwa na Menejimenti Nzuri-Najua ni gharama, lakini nothing come easy
2.Kuwa na Madirector wa uhakika,
3.Kuwa na Maproducer Tofautitofauti ili tupate ladha tofauti
4.Kuwa na Fashionista, Designer Tofautitofauti
5.Kufanya Video Maeneo ya hapa Tz kwa Nyakati tofautitofauti
6.Kujaribu Kupata Vifaa Bora Zaidi ili Video Ziwe katika Ubora wa hali ya Juu, at least sasa tumetoka quality ya 360 mpaka 480, Basi tufike 720.
Hivi vyote ni gharama, lakini kidogokidogo Mkiweza kuwekeza basi Wasanii watafika.
7.AOB: Kubali kushauriwa, kuandikiwa Nyimbo,Kushirikishwa, Being flexible is what made me Successful Man, Don't quote me wrong, I am not rich! I am successful man.