we ukitaka kuyala huyaoshi? si utaosha tena?mimi nimeona kwa macho
kariakoo na tegeta..
wanayaosha na sabuni na kuyafuta na vitambaa
yanang'aa mno halafu...
ndo mbinu ya biashara wamegundua...
kumbee
mimi nilikuwa sijui its ok....
Basi waogope kwanza madhara mengine kabla ya kuogopa madhara ya OMOmimi yes..
unafikiri kila mtu anafanya hivyoo?
kweli sio kila king'aacho ni dhahabu
Hii inanikumbusha kuna miaka nilipita na Dakar, Senegal nikakuta wa Senegali wanaosha nyama kwa sabuni (wanaifua) kabla ya kuipika. Kuuliza nikaambiwa hao ni Waislaam na dini yao inawaambia wasile damu, kwa hiyo wanahakikisha nyama haibaki na damu kabla ya kuipika.
Umeona mambo hayo? sisi huku tunaiosha kwa maji tu na kuipika (nyumbani) wauza mishkaki mitaani huko mwiko kuosha nyama, wanakuambia unaitoa ladha, hapo sasa.