Ngigana
JF-Expert Member
- Apr 16, 2010
- 2,106
- 1,443
Kwa wale ambao huenda hawatapata nafasi ya kusoma gazeti la Tanzania daima la leo (7/02/2013), kuna makala nzuri kuhusu mada tajwa hapo juu.
Makala hii ktk gazeti husika imeandikwa na NASRA ABDALLAH
"KITAALAMU kiwango cha kinga mwilini, maarufu kama CD4, hujulikana kama matibabu asili ya mwili ambapo husaidia kuulinda usipatwe na magonjwa. Endapo tu kinga hizi zitatoka, ni wazi mwili utapoteza uwezo wake wa kujihami na mashambulizi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo ukimwi.
Hata hivyo yaelezwa kwamba upungufu wa kinga mwilini unaweza ukatokea hata kama mtu hana maambukizi ya virusi ya ukimwi. Kushuka kwa kinga hizi husababishwa na kukosekana baadhi ya virutubisho mwilini, hivyo kama mtu atapata tatizo hili, mwili wake utaruhusu magonjwa mbalimbali kuingia.
Kwanini huwa hivyo? Kitendo cha mwili kutokuwa na kinga hii ya asili, ni kama nyumba iliyo wazi bila milango na madirisha, hivyo usalama wake kuwa mdogo kwa mwizi, wadudu ama takataka kuingia ndani. Hivyo virusi vya ukimwi vyaweza kuingia kama kinga zitakuwa chini, hivyo kupata magonjwa mbalimbali kama homa ya matumbo yasiyoisha, mabaranga, kukohoa, kuharisha na magonjwa mengine nyemelezi.
Hata hivyo, tatizo hili la kushuka kwa CD4 kwa sasa linaonekana kuwa kero zaidi kwa waathirika wa ukimwi na kutokana na ugonjwa huo kuenea kwa kasi, serikali ilianza utaratibu wa kutoa dawa bure za ARVs kwa ajili ya kuwezesha kurefusha maisha.
Wakati wengine wakisaidika, yaelezwa kwamba kwa baadhi yao dawa hizi zimekuwa zikiwaletea madhara mbalimbali, ikiwemo kukosa hamu ya kula, kutapika, kichefuchefu na wengine kufikia hata kuharibika ngozi. Jambo hili limekuwa likielezwa kwamba linatokana na ARVs kutoendana na mwili wa mtumiaji kwa maana ya kemikali zilizomo katika dawa hizo. Lakini, Dk. Abdallah Mandai anaelezea namna ya kukabiliana na tatizo hilo kwa kutumia ARVs mbadala ambazo kama kuna kushuka kwa kinga za mwili, zitakuwa msaada mkubwa.
Dk. Mandai anasema kuna aina nane za matunda ambapo mtumiaji atatakiwa atengeneze juisi yake kwa kufuata vipimo kwa maelekezo ya daktari, na kutaja matunda hayo kuwa ni limao, kitunguu saumu, tui la nazi, karoti, parachichi, ndizi, mbegu za papai na nanasi.
Akifafanua kimoja baada ya kingine namna kinavyofanya kazi mwilini, Dk. Mandai anasema kama mgonjwa atapata maji ya limao, kwake itakuwa ni tiba nzuri kwa kuwa itamsaidia katika ulainishaji wa chakula tumboni, kusafisha damu, kuongeza kinga za mwili na zaidi ya hapo ni yenye wingi wa vitamini C, B na E.
PUNJE ZA KITUNGUU SAUMU
Dk. Mandai anasema katika punje za kitunguu saumu, yapo magonjwa 40 yanayotibiwa, ikiwemo utumbo mwembamba, kuharisha, kuondoa minyoo tumboni na husaidia kuongeza nguvu kwa watu ambao wamekuwa wakifanya kazi ngumu.
TUI LA NAZI
Kwa tui la nazi, anasema ni tiba kwa kuwa ndani yake hupatikana virutubisho A, B na E, ambapo mbali ya kuimarisha afya ya damu, hufanya viungo kuwa na nguvu na pia husaidia katika kurudisha kumbukumbu na kuondoa homa ya matumbo.
KAROTI
Dk. Mandai anasema kwamba karoti ina virutubisho vingi ambavyo husaidia katika kulainisha tumbo, uvimbe wa kansa, kusafisha damu, kuponya vidonda vya tumbo koo na kibofu cha mkojo.
PARACHICHI
Tunda hili huwa lina virutubisho A, B na C, hivyo Dk. Mandai anaeleza kwamba husaidia katika kusafisha Uric Acid mwilini ambayo kwa kiasi kikubwa, husababishwa na ulaji nyama.
Anasema nyama huchangia magonjwa mengi mwilini, ikiwemo kufunga choo, vidonda vya tumbo, magonjwa ya ini na gout, hivyo tunda hili hufanya kazi ya kuulinda mwili na maradhi kwa mtumiaji.
NDIZI
Dk. Mandai anasema ndizi ni mojawapo ya matunda yanayoongeza CD4 kutokana na aina ya virutubisho vinavyopatikana ndani yake ambavyo ni vitamini A, B, C, E na GG, huku mbegu za papai zikiwa na virutubisho vya vitamini A, B, C, D na E. Hivi husaidia kuua vidudu vyote tumboni na kuzuia homa ya manjano.
NANASI
Kwenye nanasi kuna vitamini A, B na C ambapo kuna madini ya chuma, calcium, magness na copper, vyote hivi vikiwa vinasaidia kuimarisha damu, mifupa, meno na misuli.
Wito wa Dk. Mandai kwa jamii, anashauri kuwepo kwa utunzwaji wa mazingira kwa ajili ya kuhifadhi mitishamba ambayo Mwenyezi Mungu kaijalia nchi hii.
Anasema hayo akitolea mfano wa nchi ya China, akisema imefanikiwa kwa kiasi kikubwa hadi kufikia hatua ya kuuza dawa zao nje ya nchi.
Dk. Mandai anasema hiyo ni kutokana na kujiwekea utaratibu mzuri katika usimamizi wa dawa asili kwa ushirikiano wa karibu na serikali yao.
Kwa upande wa serikali, ameishauri kuwa karibu zaidi na waganga wa tiba asili kama inavyokuwa karibu na wadau wengine kama wasanii, kwani kutokana na mabadiliko makubwa ya mfumo wa maisha, ikiwemo soko huria, ni muhimu kurudi kwenye tiba za asili ambazo ziliweza kutumiwa na mababu.
Anaongeza kuwa, mbali ya kutibu hivyo Watanzania wengi kuwa wenye afya njema tayari kwa uzalishaji mali, pia tiba asili zinaweza kuwa sehemu ya pato la taifa kwa kuuzwa nje ya nchi.
Kwa upande wa wagonjwa aliwataka kutosita kufika hospitalini kwake Ukonga ili kuweza kupewa masharti ya namna ya uchanganya juisi za matunda hayo kwa kuwa huenda na vipimo sio kwamba mtu unajinywea tu.
Katika hili, anasema ameshaweza kuwasidia wagonjwa wengi ambapo kwa siku moja amekuwa akipokea wastani wa watu sita hadi 10, wakiwa wamepata madhara mbalimbali baada ya kutumia ARVS.