Akam Di Nelu
New Member
- Jul 27, 2022
- 2
- 0
Ilikua mchana nikichochea jiko la kuni kwa ajili ya kuandaa chakula, mara simu yangu iliyokua pembezoni mwa figa ikatoa mlio wa ujumbe mfupi. Baada ya kuifungua naona ujumbe kuwa "hongera umechaguliwa kujiunga masomo ya chuo kikuu ya shahada ya sayansi ya maabara".Nilipiga kelele na kububujikwa na machozi ya furaha.
Mama mzazi aliyekua akichanja kuni nyuma ya nyumba alikuja mbio kunitazama kwa kujua kwamba nimepatwa na jambo la hofu. Nilimrukia na kumkubatia huku nikisema "Mama ndoto zangu zinakwenda kutimia nimepokea ujumbe kuwa nimeshachaguliwa kujiunga na masomo ya chuo kikuu. Oooh, siku hiyo ilikua ni shangwe, mama yangu alifurahi sana.
Siku zilipowadia mama yangu aliuza baadhi ya vitu vya ndani ili kupata nauli ya kuendea chuo. Usiku wa kuamkia safari sikupata hata usingizi kwani nilikua nikiwaza safari yangu itakavyokua. Hatimaye alfajiri nilianza safari yangu. Njiani nilikua nikitafakari wosia wa mama yangu na kuapa ya kua sitamwangusha mama yangu, bali nitatekeleza yote aliyonifundisha.
Jioni nilifika jijini humo, nilipofika chuoni nilipokelewa na dada ambaye alikua ni mkarimu na kuhisi kwamba ni rafiki mwema. Nilimpenda sana dada chauza kwani alikua ni mtu wa karibu sana kwangu na nilipokua na shida alinisaidia.
Lugha yangu ilikua ni utata kwani nilionekana nikiongea kiswahili chenye rafudhi ya kuchekesha, mavazi yangu yalikua ni ya kufurahisha, kwani nilipovaa watu walinicheka, hata baadhi yao kunitemea mate na kunitenga nisiongozane nao.Baadhi ya wanafunzi walinitazama kwa dharau."Ooooh masikini Sikitu", nilijisemea moyoni. Nilipata faraja baada ya kumweleza dada Chauza , kwani alinipa maneno ya faraja na kunitia moyo.
Jumamosi asubuhi, mara napokea simu na kusikia sauti ya dada Chauza "Sikitu jioni nataka nikakutembeze mjini"Nilifurahi na kuhisi masaa yanachelewa kufika.Hatimaye muda uliwadia tukaenda kutembea.Shingo yangu ilikua juuu juu nikitazama magorofa, barabara nzuri na magari ya kila aina. "Mmmmmmh! hakika mji huu ni wa kupendeza sana"nilijisemea kimoyomoyo.Ama kweli akufaae kwa dhiki ndiye rafiki, tuliingia maduka mbalimbali na kununuliwa nguo, viatu na mafuta, hiyo haikutosha niliipelekwa saloni na kutengenezwa nywele zangu zilizokua zimesukwa mtindo wa twende kilioni.Nilimshukuru sana dada yangu na kujivunia sana kwani alinifaa sana kwa kila hali.
Siku nyingine nilipokea ujumbe kutoka kwa dada Chauza akinitaka tukatembee. Wala sikusita kwani nilimuamini dada yangu kipenzi. Nilipanda bajaji na kufika sehemu ile aliyonielekeza.Ilikua ni ajabu kidogo kwani eneo halikua na makazi ya watu isipokua nyumba moja kubwa iliyozungushiwa uzio. Mara Paaap! dada Chauza alitokea getini, nilipomwona hofu yangu iliondoka kwa kuamini kuwa niko salama kwa kuwa rafiki yangu kipenzi nimemwona. Basi tuliingia ndani, nilihoji kuwa huku ni wapi na ni kwa nani? Dada Chauza alisema "ondoa shaka hapa ni kwa kaka yangu na nimekuja kumwona kwa sababu ni mgonjwa, hivyo nikaona vyema pia na wewe umwone kaka yangu". Nilifurahi kumwona kaka yetu kwani alikuwa mchangamfu kama dada Chauza, pia tulikula pamoja.
Maskini Sikitu! Kikulacho kinguoni mwako. Alfajiri nashtuka najihisi mwili wangu ni mchovu sana. Naangaza macho yangu na kuona ni mazingira ambayo sikumbuki nilifikaje, nguo zangu zimezagaa sakafuni, niliona pesa ambazo sikujua ni kiasi gani juu ya kiambaza cha kitanda. Mwili wangu ulitetemeka kama mtu mwenye baridi kali, huku jasho likinitoka, nilipatwa na hofu na kuhisi kushikwa na jinamizi. Natazama shuka iliyokuwa juu ya miguu yangu imetapakaa damu pamoja na kinyesi, najaribu kujisogeza napata maumivu makali sana sehemu zangu za siri pamoja na haja kubwa."Maskini Sikitu nimeshapoteza usichana wangu". Nilipigwa na butwaa kwa dakika kadhaa, ndipo akili iliponijia ya kuamka pale kuvaa nguo zangu huku nikibubujikwa na machozi. Nilitoka nje na kugundua kuwa ilikua ni nyumba ya kulala wageni, niliomba msaada kwa wasamalia wema na ndipo nilipata msaada wa kufika chuoni.
"Fyuuuuuuh! Hivi ulidhani pesa ya kukununulia vile vitu ilitoka wapi? Hakuna vitu vya bure"ilisikika sauti ya Dada Chauza baada ya kuuliza kwanini alifanya vile. Kinywa changu kilikosa hata neno la kusema,nilizubaa kwa sekunde kadhaa huku machozi yakinitoka.
Ufaulu wangu ulishuka, sikuweza kusimamia masomo yangu. Hali ya pesa kwangu ilikuwa ni changamoto kwani bumu nililopata niligawana na familia yangu. Nilikosa baadhi ya mahitaji muhimu kwa ajili ya masomo yangu. Nilikosa jinsi ya kufanya ndipo nikaamua kumtafuta dada Chauza anisaidie hata kiasi kidogo cha pesa. Mmmmmh!!, aliniambia kuwa nikihitaji pesa ni lazima nikubaliane nae kuwa ni lazima nipate mwanaume wa kunihudumia.Sikua na jinsi ya kufanya, maskini Sikitu sikusita kukubaliana nae.
Kutoa Mwili wangu kwa mkufunzi ilikuwa ni kawaida yangu ili niweze kufaulu mitihani yangu. Kumbi za starehe , kunywa pombe, kutembea na wanaume tofauti tofauti hayo yalikua ni maisha yangu. Sikujutia Nilipompata Zungu, Mwanaume ambaye alionesha mapenzi mema kwangu na kunitaka tuwe wachumba. Hakika Zungu ni mwanaume niliempenda kwani alinishauri mambo mengi pamoja nakuachana na pombe. Binti nilipangiwa chumba na kuwekewa vitu vya thamani, kideo na vyombo.Tuliahidiana mambo mengi pamoja na kuoana mara tu nitakapomaliza masomo yangu.Nilihisi kuwa na tumaini jipya katika maisha yangu.
Miaka mitatu baadae, nilimaliza masomo yangu huku nikisubiri matokeo. Jioni nikiwa natoka bafuni, ghafla nilihisi kizunguzungu, nilijitupa kitandani na kuhisi kuishiwa nguvu. Oooh, Sikitu mimi, nilijikuta niko hospitali, pembeni yangu alikuwa ni jirani yangu aliyenipatia msaada, ndipo aliponipoza na kunijuza ndiye aliyenileta hospitali.
"Pole sana Sikitu vipimo vinaonesha u mjamzito, pia umeathirika na virusi vya UKIMWI, pamoja na magonjwa ya zinaa"hayo yalikua ni maneno ya Daktari. Jasho jembamba lilinitoka na kuhisi niko ndotoni, mwili wote unatetemeka. Nitafanya nini mimi Sikitu, Je haya ndio malipo yangu? Ni laana gani iliyonikumba!!! Nilinyanyua simu yangu na kumpigia Zungu, sauti ilisikika kuwa" Marufuku kunipigia simu kuanzia leo, kwani hunifai na huna lolote kwa sasa, tafadhari sana nina mke hivyo usinitafute tena" Ama kweli ng'ombe wa maskini hazai nilijisemea moyoni.Nilihisi kufa ganzi mwilini mwangu na kuhamaki kama mtu niliyenyang'anywa tonge mdomoni. Siku mbili baadae natazama matokeo yangu.Khaaaaaah.....!!! Sikitu sifai tena mimi, matokeo yangu yanaonesha nimefeli.
Nitafanya nini mimi, naogopa kurudi nyumbani. Elimu yangu si kitu, utu wangu si kitu, mwili wangu si kitu.Hatimaye nimeambulia magonjwa, mimba na kupoteza thamani ya mwili wangu.Je matunda ya Elimu niliyoitafuta ndiyo haya.Sina tumaini tena. Ee mama Sikitu haya ndiyo yaliyonikuta, tafadhari pokea ujumbe huu, siwezi hata kukutazama machoni, siwezi kurudi nyumbani, najua nitakuumiza mama, kila la kheri mama Sikitu.
KUMBUKUMBU REJEO
1. Niggar stoper (2019) katuni 2
2. Nestory vijana FM (2020) katuni

Attachments
Upvote
0