Matunda ya fedha za Uviko-19

Matunda ya fedha za Uviko-19

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
204
Reaction score
231
Wakati Shirika la Fedha Duniani (IMF) likitoa fedha shilingi trilioni 1.3 kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya Korona, matumizi yake nchini Tanzania yalikua ya tofauti jambo lililoibua mijadala kwenye makundi mbalimbali wakihoji uamuzi uliochukuliwa na Rais Samia Suluhu.

Rais Samia aliamua fedha hizo zitumike kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali iliyopewa kipaumbele katika jamii na kwenda kinyume na matarajio ya wengi ambao walidhani fedha hizo zingetumika katika ununuzi wa barakao, vitakasa mikono na chanjo.

Baadhi ya maeneo yaliyolengwa zaidi ni Ununuzi magari ya wagonjwa ya kisasa 20 na magari ya kawaida 365, Ujenzi wa vituo vya dharura na vifaa kwa hospitali zote kuanzia Taifa hadi halmashauri, Uimarishwaji wa mfumo wa usambazaji na ununuzi wa mitungi ya gesi katika hospitali za rufaa.

Pia usimikaji wa vinu 44 vya hewa ya Oksijeni kwa ajili hospitali za Taifa na halmashauri, Ununuzi wa mashine za X-Ray 85, Ufungaji wa mashine za MRI kwa hospitali za Taifa, kanda na mikoa, Ujenzi wa vituo vinne vya Telemedicine.

Ujenzi wa vyumba na ununuzi wa vifaa vya uangalizi maalum (ICU) 72 kwa ngazi ya Taifa, kanda, mikoa na baadhi ya halmashauri, Utekelezaji wa miradi ya maji kwa wananchi, Utekelezaji miradi ya elimu kama vile madawati, vyumba vya madarasa katika vyuo 17 na Vituo vinne vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Wote sasa ni mashuhuda wa namna ambavyo miradi iliyojengwa kupitia fedha hizo imezaa matunda kwenye jamii, mfano ujenzi wa vituo vya afya umewezesha upatikanaji wa huduma kwa haraka kwa kuwa sasa hospitali zipo karibu na makazi ya watu, pia uwepo wa vifaa tiba umeokoa maisha ya wananchi waliokua wakipoteza uhai kutokana na ukosefu wa vifaa tiba na dawa.

Utekelezaji miradi ya elimu kama vile madawati, vyumba vya madarasa katika vyuo 17 na Vituo vinne vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) umeongeza ufaulu kwa wananfunzi hasa wasichana mfano hai ni namna ambavyo Shule ya Sekondari Ziba wilayani Igunga mkoani Tabora ilivyoweza kuingia kwenye kumi bora ya shule zilizofanya vizuri matokeo ya kidato cha sita mwaka 2022.

Uamuzi huo uliochukuliwa na Rais Samia katika utekelezaji wa miradi hiyo, umafanya dunia iitambue Tanzania kama nchi yenye matumizi mazuri ya fedha hivyo kuweza kukopesheka kwa mikopo nafuu ambayo inatumika katika utatuzi wa changamoto katika jamii kama ujenzi wa miundombinu ya maji, afya na elimu.
 
Tulikopeshwa hizo pesa ,hatukupewa msaada kama ulivyoeleza hapa
 
Tulia chawa wa mama wafanye kazi yao wewe enzi zile uliifanya kwa weledi pia. Zama zako zimepita kaa kwa kutulia
 
Tulikopeshwa hizo pesa ,hatukupewa msaada kama ulivyoeleza hapa
Siku nyingine uquote uzi wake ili comment yako ibaki kuwa relevant. Mwenzakoo kesha edit uzi na comment yako imebaki hewani,
 
Wakati Shirika la Fedha Duniani (IMF) likitoa fedha shilingi trilioni 1.3 kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya Korona, matumizi yake nchini Tanzania yalikua ya tofauti jambo lililoibua mijadala kwenye makundi mbalimbali wakihoji uamuzi uliochukuliwa na Rais Samia Suluhu.

Rais Samia aliamua fedha hizo zitumike kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali iliyopewa kipaumbele katika jamii na kwenda kinyume na matarajio ya wengi ambao walidhani fedha hizo zingetumika katika ununuzi wa barakao, vitakasa mikono na chanjo.

Baadhi ya maeneo yaliyolengwa zaidi ni Ununuzi magari ya wagonjwa ya kisasa 20 na magari ya kawaida 365, Ujenzi wa vituo vya dharura na vifaa kwa hospitali zote kuanzia Taifa hadi halmashauri, Uimarishwaji wa mfumo wa usambazaji na ununuzi wa mitungi ya gesi katika hospitali za rufaa.

Pia usimikaji wa vinu 44 vya hewa ya Oksijeni kwa ajili hospitali za Taifa na halmashauri, Ununuzi wa mashine za X-Ray 85, Ufungaji wa mashine za MRI kwa hospitali za Taifa, kanda na mikoa, Ujenzi wa vituo vinne vya Telemedicine.

Ujenzi wa vyumba na ununuzi wa vifaa vya uangalizi maalum (ICU) 72 kwa ngazi ya Taifa, kanda, mikoa na baadhi ya halmashauri, Utekelezaji wa miradi ya maji kwa wananchi, Utekelezaji miradi ya elimu kama vile madawati, vyumba vya madarasa katika vyuo 17 na Vituo vinne vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Wote sasa ni mashuhuda wa namna ambavyo miradi iliyojengwa kupitia fedha hizo imezaa matunda kwenye jamii, mfano ujenzi wa vituo vya afya umewezesha upatikanaji wa huduma kwa haraka kwa kuwa sasa hospitali zipo karibu na makazi ya watu, pia uwepo wa vifaa tiba umeokoa maisha ya wananchi waliokua wakipoteza uhai kutokana na ukosefu wa vifaa tiba na dawa.

Utekelezaji miradi ya elimu kama vile madawati, vyumba vya madarasa katika vyuo 17 na Vituo vinne vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) umeongeza ufaulu kwa wananfunzi hasa wasichana mfano hai ni namna ambavyo Shule ya Sekondari Ziba wilayani Igunga mkoani Tabora ilivyoweza kuingia kwenye kumi bora ya shule zilizofanya vizuri matokeo ya kidato cha sita mwaka 2022.

Uamuzi huo uliochukuliwa na Rais Samia katika utekelezaji wa miradi hiyo, umafanya dunia iitambue Tanzania kama nchi yenye matumizi mazuri ya fedha hivyo kuweza kukopesheka kwa mikopo nafuu ambayo inatumika katika utatuzi wa changamoto katika jamii kama ujenzi wa miundombinu ya maji, afya na elimu.

Sijui nichukue yapi. Kuna video yake sehemu- labda u tub akihojiwa aaah nimekumbuka Alipoenda Diaspora ku-promote Film ya Royal Tour.

Nafikiri majibu yake, alichokisema,yanatosheleza.

...lakini kwa spidi hiyo ya mijengo na vifaa n.k mhhh yaani katika miaka miwili yamefanyika yote hayo?
 
Back
Top Bottom