Matunzo kwa mwenza siyo hisani, ni lazima

Mr George Francis

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
234
Reaction score
376
MATUNZO KWA MWENZA SIO HISANI BALI NI LAZIMA.

Je wajua kuwa mume au mke kutoa matunzo kwa mwenza wake ni lazima kisheria?

Soma hapa upate majibu.

Tulio wengi tunadhani kuwa kutoa matunzo kwa wenza wetu ni hisani tu kama namna ya kuwasaidia au kuonesha upendo tu dhidi yao na wala sio jambo la lazima wala halipo kisheria.

Lakini sasa leo nataka ufahamu kwamba kutoa matunzo kwa mwenza sio hisani wala sio msaada bali ni wajibu wa lazima kisheria.

Sheria ya Ndoa hapa kwetu Tanzania ya mwaka 1971 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 hasa Kifungu cha 63 (1) & (2) kimeeleza bayana kuhusu hili.

Kifungu cha 63(1) cha sheria hii kinaeleza kwamba mume ana wajibu wa kumtunza mkewe kwa kumpa mahitaji yote muhimu katika maisha kama vile mavazi, chakula na malazi kulingana na uwezo wake.

Kifungu cha 63(2) cha sheri husika kinampa mwanamke wajibu wa kumtunza mumewe. Kwa mujibu wa kifungu hiki mwanamke mwenye uwezo wa kufanya hivyo ana wajibu wa kutoa matunzo kwa mume wake. Mwanamke ana wajibu wa kumtunza mumewe endapo mume ana ugonjwa au ulemavu wa kimwili au kiakili unaoweza kumfanya hashindwe kufanya kazi inayoweza kumwingizia kipato.

Hapa tunagundua kwamba mume kutoa matunzo kwa mkewe ni jukumu la muda wote lakini mwanamke hutoa matunzo kwa mumewe ni pale tu ambapo mume wake amefikwa na maradhi au ulemavu unaomuondolea uwezo wa kufanya kazi ya kumwingizia kipato.

Sheri imeendelea kueleza kuwa mume au mke akishindwa kutekeleza wajibu huo kwa makusudi, basi Mahakama chini ya Kifungu cha 115(1) &(2) cha Sheria ya Ndoa yaweza kumwamuru kutelekeza wajibu huo hata kama mume na mke hawaishi pamoja kwa wakati huo kutokana na sababu zilizowekwa wazi chini ya Kifungu hicho. Hivyo, nikuombe utenge muda wa kusoma zaidi kifungu hiki kwaajili ya kujenga uelewa wako binafsi.

Lakini pamoja na kuwepo kwa wajibu huu kisheria lakini, haki ya mwanamke kupata matunzo inakoma tu pale anapoolewa na mtu mwingine na haki ya mwanaume kupata matunzo inakoma tu pale anapooa mwanamke mwingine, isipokuwa kwa makubaliano maalumu. Hii ni kwa mujibu wa Kifungu cha 120(1) & (2) ya Sheria ya Ndoa

Hivyo, kama mahakama kwa mujibu wa sheria itakuamuru utoe matunzo kwa mke au mume uliyetengana nae arafu ikatokea mke au mume huyo ameingia katika mahusiano na kuishi na mtu mwingine, hapo mojakwamoja wajibu huo wa kutoa matunzo utafikia ukomo.

Ahsante kwa kuwa pamoja nami katika mada hii. Mwisho wa mada hii ni mwanzo wa mada nyingine nzuri. Endelea kufuatilia mada zinazofuata.

Karibu Telegram: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓
_______________
It's me
A Lawyer and LifeCoach
Mr. George Francis
Contacts: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com

Like, Comment, Share
 
Karibu Telegram: TANZANIA LAWYERS FORUM [emoji310]
_______________
It's me
A Lawyer and LifeCoach
Mr. George Francis
Contacts: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com

Like, Comment, Share
Badirisha title mkuu. Andika "MATUNZO KWA WANANDOA SIO HISANI BALI NI LAZIMA" usifungulie mlango wazinifu kujipenyeza kwenye Sheria za WANANDOA.
 
Bila shaka kuna tofauti kati ya Mwenza sio mpenzi au mchumba. Mwenza ni mke au mume wa ndoa
 
Tatizo wa siku hizi hawana adabu ya ndoa na hawana hekima ya kutii mume wake.

Mimi nispend sehemu ya income yangu kwa mtu ambaye hatuelewani ananikwaza kila saa, hilo haliwezi kutokea.
 
Back
Top Bottom