Elections 2010 Matusi au 'tuhuma' katika kampeni?

Elections 2010 Matusi au 'tuhuma' katika kampeni?

Mwizi ni mwizi tu hata akiwa Miss World or Universe. Huwezi kuitwa kistaarabu kama matendo yako si ya kistaarabu. Neno/jina la kistaarabu linalohusiana na mwizi au wizi ni nini? Kiswahili nilijitahidi sana nikalamba F kwenye HKL, naomba kueleweshwa.:smile-big:
 


Na ninamini bila chembe ya shaka kwamba jana Tido alipigiwa simu na mmoja kati ya vigogo wa CCM kumuamuru akate matangazo – kwani nina hakika baada ya kukaa BBC miaka kadha Tido anajua maadili ya profession yake na hivyo uamuzi huo haukuwa wake.
NI YULE YULE ALIYEMTOA BBC NA KUMLETA TVT...kwa hiyo ni lazima achunge maslahi yake
 
Mbona magazeti mengi tu yanaongelea kesi zilizopo mahakamani? Yaani mtu akiwa na kesi mahakamani hasitajwe kuhusiana na hiyo tuuma yake? Hawataki wajulikane kama wao ni wezi? Hivi ndio ilikuwa mbinu ya kutengeneza maadili? Tume ya uchaguzi ni chombo cha CCM na wala si serikali!
 
Katika mbinu za Uchaguzi, makosa yoyote yaliyofanywa na viongozi wa chama chochote hutumiwa kama mbinu ya kupata ushindi.. Inaruhusiwa na kama CCM wanaona sii vizuri wangewaondoa hao watu ktk kugombea au hata Uanachama ili kukinusuru chama. Unapolea donda ni lazima ukubali kuumbulika siku linapovuja usaa..

Hhakuna nchi yeyote kisiasa wangeliacha swala la EPA kutumika ktk kapeni za uchaguzi, inafanyika nchi zote na hakika cvyama vyote hujaribu sana kujiepusha na makosa kama waliyoyafanya CCM kuwabeba wafisadi na hata kuwapa nafasi ya kugombea tena Ubunge..Hizi ndio Miscalculations za CCM..
 
Nimeshangaa kumwona kinana akijaribu kuleta propaganda baada ya kuzungumza ukweli,anadai dr slaa na marando wanawapotosha watanzania kwa kuwataja kwa majina wahusika wakuu wa sakata la epa,nani ni mgeni wa kashfa ya epa?anajaribu kuficha nini na kwa maslahi ya nani?uadilifu wake upo wapi?ni mzalendo kweli?klwanini asiende mahakamani kama anaona mgombea wao anakashfiwa kwa kuambiwa ni mshiriki ktk kukwapua rasilimali za watanzania?
 
huyo kinana kwanza mfitini sana
hana jipya tusilolijua

NDIYO kikwete ana mkono wake pale EPA
 
Kinana nae si ndiyo wale wale, wengi wa CCM viongozi siyo wazalendo.
Mmoja wao akiiba ndiyo wanaona YES!!!! mbabeee!!! mwanaume wa kweli kweli.

Waajabu sana hawa CCM.
 
Nimeshangaa kumwona kinana akijaribu kuleta propaganda baada ya kuzungumza ukweli,anadai dr slaa na marando wanawapotosha watanzania kwa kuwataja kwa majina wahusika wakuu wa sakata la epa,nani ni mgeni wa kashfa ya epa?anajaribu kuficha nini na kwa maslahi ya nani?uadilifu wake upo wapi?ni mzalendo kweli?klwanini asiende mahakamani kama anaona mgombea wao anakashfiwa kwa kuambiwa ni mshiriki ktk kukwapua rasilimali za watanzania?
=====

Wakati wa Kampeini huwa ni wa kuweka mambo wazi kuliko kuyaacha ukidhani yatakwisha yenyewe. Ndiyo maana Dr. Slaa ametangaza hadharani uvumi uliokuwa umeenea kuwa ana kimanda, na sasa amemtambulisha kuwa ni mchumba. Kwa hiyo badala ya Kinana kumtetea Kikwete kuhusu EPA, amwache Kikwete atueleze mambo matatu tu:

-Alihusikaje na EPA?
-Kwa nini aliamua kuwasemehe anaodai walirudisha fedha za EPA?
-Kwa nini hajawahi kuweka hadharani ripoti ya watu 6 aliowateua kuchambua kashfa nzima ya EPA?

Asimame hadharani atoe ufafanuzi, awaangalie watanzania usoni aseme anachojua kuhusu EPA maana ni fedha za wananchi na zilichukuliwa kutoka chombo kitukufu BOT. Mbona alisimama hadharani akamtetea mtoto wake Ridhiwani kuhusu ugomvi wake na Bashe?

Mkuu wa nchi kutajwa katika kashfa kubwa namna hii ukakaa kimya si salama hata kidogo. Akanushe na wanaomsingizia wapelekwe mahakamani. Mbona mgombea wa CUF Tanga amekamatwa kwa kumkashifu Kikwete? Mbona Mtikila yuko mahakamani akijibu tuhuma za kumkashifu?

 
Na anapaswa kuwaeleza watanzania juu ya nafasi yake ktk kumiliki bandari kavu iliyopo pale kamata inayoitwa shariff na wakati waliwafukuza watu kwa kisingizio cha kujenga stand ya mabasi yaendayo kasi,
 
Kwa maoni yangu naona kitendo hiki alichofanya Tido Mhando kukatisha matangazo kwa madai kuwa yaliyokuwa yakihutubiwa ni 'matusi', kimempunguzia kwa kiasi kikubwa, hadhi ya umakini wake wa kiitaaluma. Nitakuwa muangalifu sana siku zijazo kumuweka mtu kama huyu kuongoza chombo cha habari cha taifa.

DR. SLAA FOR PRESIDENT! Badilisha signature yako isomeke hivi: DR. SLAA FOR PRESIDENCY!
 
Sisiemu hawana jipya bana, Kinana tunavyojua ni msomali kwa hio si mtanzania kabisa.EPA ni mradi wa CCM lazima waelewe, kwani wao waliendesha hizo kampeni zo kwa kutumia hizo fedha, fedha za EPA zilikuwepo iweje ziliwe kipindi hiki cha utawala wa JK na Mkapa? JK nae ni mhusika wa EPA kwa kuwa kawalinda waliochukua na kurudisha hela za EPA, je mwizi akiiba kisha kurudisha anaachiwa? mwizi ni mwizi tu lazima sheria ichukue mkondo wake ila yeye alitangaza kuwasamehe, je utasamehe wezi wa fedha za walala hoi kwani hio fedha ni yake? Marando na Slaa wana kila sababu ya kusema hayo maana yanakera na wananchi hawana pa kuongelea zaidi ya kuwatumia hao waheshimiwa.Huree CHADEMA. PEOPLES POWERRRRRRRRRRRR, 2010 HATUDANGANYIKIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII.
 
Tunahitaji maelezo vile vile kuhusu nyara za serikali zilizokamatwa nje na ikadaiwa kampuni ya Mheshimiwa Kinana ndiyo ilizisafirisha.

Ila CCM ikishawekwa upinzani, kuna mengi sana yatabidi kuchunguzwa. Lile fagio la chuma alilozungumzia Mzee Ruksa bila matendo litatumika. Hiyo ndiyo siku utaonekana ukweli kwamba Watanzania sio mabwege. Sasa ni maneno tu.
 
kinana pia ni mwizi wa kutupwa ndiye anayeendesha biashara ya magendo ya nyara za taifa kama wanyama pori kwenda Nchi za Nje hususana Arabuni hana credibility ya kuongelea ufisadi wakati yeye mwenyewe ni jizi la kutupa
 
kinana pia ni mwizi wa kutupwa ndiye anayeendesha biashara ya magendo ya nyara za taifa kama wanyama pori kwenda Nchi za Nje hususana Arabuni hana credibility ya kuongelea ufisadi wakati yeye mwenyewe ni jizi la kutupa

Jamani wakati ndio huu wa kuweka mambo hadharani. Tafadhali tuwekee data za uhakika maana tuna kiu.
 
Wow
ndo kwanza kampeni zipo ahsubuhi
masikio yana njaa
 
huyo kinana kwanza mfitini sana
hana jipya tusilolijua

NDIYO kikwete ana mkono wake pale EPA

Watanzania ndivyo tulivyo! Kwani wasio jua kuwa EPA ni CCM ninani? Harafu wanatapika kuwa watu wasiseme kuwa WIZI wa EPA ni Mkapa!
 
Back
Top Bottom