Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
Wadau, naomba nifahamishwe. ‘Matusi' ni nini katika medani hizi za kisiasa? Na nani mwenye mamlaka ya kutafsiri ‘matusi' katika kampeni hizi? Najua CCM wangependa sana kuwa watafsiri pekee wa neon hili.
Hivi ‘matusi' aliyotoa Marando ya kuwataja vigogo wale wanne wa CCM anaowatuhumu kukwapua hela za EPA kutoka BoT ni matusi? Kwa tafsiri gani – ya Tido Mhando au tafsiri ya kamusi gani?
Mimi nafikiri ‘matusi' kutokana na tafsiri ya Tido Mhando kwa mfano ni kwa Marando ‘kutaja majina' ya hao waliosuka mipango ya kuibia BoT. Na pengine kilichomkera zaidi Mhando ni namna Marando alivyowataja – kwa kujiamini kabisa – kusema kuwa hawatamfanya chochote kwani anao ushahidi wa kuwaumbua.
Na hapa Tido Mhando asingetumia neno "matusi" wakati alipoongelea suala la kukata matangazo ya TBC hata kama yeye ndiye amejitwisha jukumu la kutoa tafsiri.
Kwani neno sahihi hapa lilipaswa kuwa ‘tuhuma' au ‘madai' dhidi ya mtu mwingine ambayo hana ushahidi nayo. Kukimbilia kusema eti matusi ni mbinu tu wanaoitumia CCM katika kuzikabili hoja kama hizi.
Mwaka 1996 katika mkutano wake wa kampeni wa kugombea Ubunge jimbo la Temeke, Augustine Mrema (wa NCCR wakati huo) alitoa tuhuma nzito dhidi ya rais Mkapa na viongozi wengine wa CCM kuhusu uchotaji wa hela Sh 900m/- kutoka serikalini. Sioni tofauti ya ile na hii ya Marando au na hata ile ya Slaa Mwembe Yanga ya 2007.
Serikali ya CCM ilimshitaki Mrema kwa kutoa tuhuma za uongo, lakini kesi dhidi yake ilitupwa.
Na ninamini bila chembe ya shaka kwamba jana Tido alipigiwa simu na mmoja kati ya vigogo wa CCM kumuamuru akate matangazo – kwani nina hakika baada ya kukaa BBC miaka kadha Tido anajua maadili ya profession yake na hivyo uamuzi huo haukuwa wake binafsi.
Kwa CCM kuziita hoja, tuhuma, na madai madai wanayotoa wapinzani dhidi yake kwamba ni ‘matusi' hazikuanza jana. Nakumbuka wakati vyama vingi vilipoingia hawa CCM (hasa Wabunge) hawakuwa wamezoea kuzikabili hoja nzito za kukosolewa kutoka kwa wapinzani (kuhusu masuala hayahaya ya ufisadi na matumizi mabaya ya hela za umma) na hasa pale yalipokuwa yanaandikwa magazetini na kutokuwa na majibu nayo.
Hoja hizo walikuwa wanaziita ‘matusi' kutoka kwa wapinzani. Nakumbuka katika kikao cha Bunge, Mbunge Ole Molloimet alilishambulia sana habari iliyokuwa imeandikwa katika Majira ikimnukuu Mrema kwamba ni matusi.
Halafu Tido anasahu kuwa ‘matusi' aliyotoa Marando siyo mapya – yalishatolewa kule katika mkutano wa hadhara wa Chadema kule Mwembe Yanga mwaka 2007 ambapo Dr Slaa alipoitaja ile timu ya mafisadi 11, wakiwemo hawa wanne waliotajwa na Marando jana.
Kitu ambacho CCM hawakukipenda ni jinsi TBC ilivyolazimika kuvipa fursa vyama vya upinzani nao kurusha matangazo yao – bila shaka kutoka msukumo na fedha za UNDP kama tunavyoelezwa.
Ingekuwa ni yenyewe CCM ingeweza kuunda hoja kwamba TBC ni chombo cha umma kwa hivyo kisijiingize katika kutangaza mikutano live ya vyama vya siasa na kuongeza kwamba TV/Redio binafsi ndiyo zitumike kwa shughuli hiyo.
Hapa wangewaweza wapinzani, kwani kwa kuwa CCM tu ndiyi ina mapesa mengi ingeweza kulipia coverage ya mikutano yao katika vyombo hivyo binafsi kitu ambacho vyama vingine vingeshindwa kutokana na gharama kubwa.
Pili vyombo kadha binafsi ambavyo tayari vimeonyesha kuishabikia CCM – kama vile ITV, Channel 10 na Star TV vingeweza pia kukataa kutoa coveragen ya mikutano ya wapinzani kwani ni kitu cha hiari.
Naweza kusema CCM inapenda kuona coverage ya kampeni zake zifike nchini kote na siyo za upinzani.