GE2025 Matusi marufuku kwenye Kampeni. Kuna maisha baada ya Uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, amewataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kuhakikisha kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2025 zinafanyika kwa kistaarabu, bila kutumia lugha za matusi, kashfa au vitendo vyovyote vinavyoweza kuhatarisha amani na mshikamano wa kitaifa.

Akizungumza Jumatatu, Agosti 18, 2025, katika Mafunzo kuhusu Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Kituo cha Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), mkoani Dar es Salaam, Jaji Mutungi amesisitiza kuwa vyama vya siasa vina wajibu wa kuendeleza misingi ya amani na mshikamano wa taifa.

"Nendeni mkafanye kampeni za kistaarabu mkiwanadi wagombea wenu. Jiepusheni kabisa na lugha za matusi, kashfa, uchochezi au vitendo vyovyote vinavyoweza kuvuruga amani na utulivu wa taifa letu," amesema Jaji Mutungi.

Ameongeza kuwa amani na mshikamano ni urithi ulioachwa na waasisi wa taifa, hivyo viongozi wa kisiasa wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa wananchi.

"Kumbukeni kuna maisha baada ya uchaguzi. Uchaguzi si mwisho wa siasa wala maendeleo. Turithishe amani hii kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo," amesema.
Your browser is not able to display this video.
 
Mamaee. Huu usenge wote unaofanywa na serikali juu ya uchaguzi ni miongoni mwa wanaoharibu. Siku ukifa watu watafurahia kifo chako sana.
 
Mamaee. Huu usenge wote unaofanywa na serikali juu ya uchaguzi ni miongoni mwa wanaoharibu. Siku ukifa watu watafurahia kifo chako sana.
The same na yule anaitwa mahera .. yule jamaa anaonekana ana roho mbaya sijapata kuona
 
Mamaee. Huu usenge wote unaofanywa na serikali juu ya uchaguzi ni miongoni mwa wanaoharibu. Siku ukifa watu watafurahia kifo chako sana.
Wakiongea hivyo utadhani ninwastaarabu kumbe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…