Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?


Mi sijAwahi kusikiA hukumu yoyote kwa wahusika wa haya mauaji, mwenye ushaidi aniambie hapa, viongozi kutoa takwimu tu, hakuna uhalisia na hasa kipindi hiki cha uchaguzi ndo haya utokea, walaaniwe wote wanao husika.
 
umenikera sana kusema hii ni serikali sikivu,futa usemi wako haraka ndo twende sawa,wewe mwenyewe umekiri kuwa ccm inaua ndugu zetu leo usikivu wa hawa kenge umetoka wapi? mimi ni mbwa nitawala wote hadi kikwete ngoja kichaa cha mbwa kianze.

Hata mimi nilitaka kutapika niliposoma neno hilo..!!!
 
Tatizo la nchi hii hakuna hatua inachukuliwa hata kama ni baya iwapo waathirika ni wananchi wasiokuwa na uwezo. Hivi serikali inataka tuamini wanashindwa kuwakamata waganga wanaohusika na shughuli hii ambayo inalitia aibu Taifa letu ulimwenguni.

Kama serikali ingetaka kulishughlikia suala hili, polisi ingepandikiza watu wake CID kujifanya wanatafuta hawa waganga ili wapate dawa ya kupata utajiri, lakini hawana muda wa kulifuatilia jambo hawana faida nalo, wakiambiwa walifuatilie container lina mali ya wizi wote wataacha kazi zote kulifuatilia hilo container moja kwasababu wanajua kuna ulaji.
 
Wadau kwa wenye kujua sababu za maalbino kuuwa na kupotea mara inapo karibia uchaguzi?
 
Wanahusishwa naushirikina kijana ndo tatizo letu wabongo wanauliwa na kuchukuliwa viungo very sad yote hayo ni ushirikina
 
Cha ajabu zaidi ni kuwa mpaka sasa walioshikwa na viungo vya albino ni wachungaji wa kanisa.
 
...uuaji wa albino ni ujinga tu uliosababishwa na ccm
 
nipe ushahidi ndo nitaamini wachungaji hawako hivyo watakuwa wanawachafua tu

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Bw.Zelothe Stephen aliwataja watuhumiwa wawili kuwa ni Mchungaji wa kanisa la Pentekoste Idiwili,Cosmas Mwasenga (39) na Luseshelo Mwashilindi (38) ambao walikutwa na viungo vinavyodhaniwa vya maeneo ya mikono wakipita kutafuta wateja huku wakiviita kwa jina la ¡viungo vya Kunguru mweupe¢.


Kamanda Stephen alisema kuwapolisi walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu kuwepo watu waliokuwa wanatafuta wateja wa viungo hivyo vya albino katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya Makunguru na Mwanjelwa wakitamka jina la kunguru mweupe.

Source: Dullonet Tanzania | Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste akamatwa na viungo vya Albino.
 

Asante kwa ushahidi wako mzuri. Unajua Umeniongezea imani. Yesu alisema si wote waniitao bwana bwana watakoupata ufalme wa mungu. Kumbe duniani wako wachungaji wanajifanya kumwita YESU lakini mioyo yao IPO kwengine. I'm Christian Damu. I love Jesus Christ more than anything... Because maneno yake yanadhihirisha unabii aliousema unatimia.
 

Wako wachungaji na maaskofu wanaolawiti na kulawitiwa. Ulikuwa pia hujuwi? Unataka ushahidi?
 
Wako wachungaji na maaskofu wanaolawiti na kulawitiwa. Ulikuwa pia hujuwi? Unataka ushahidi?

Woooooo nakuamini sasa huna haja ya kuleta ushahidi....
Hakika bwana Yesu ni mkuu. Alisema haya yote kuwa yatatukia na yakitukia tukumbuke alichokisema alipokuwa nasi duniani ...hakika wako mbwa mwitu waliovalia ngozi ta kondoo. Jina la bwana Yesu lipewe Sifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…