Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Nasikitika kuona serikali inameshindwa kulinda maisha ya hawa ndugu zetu, unyama gani huu? TISS kazi yake ni kuhakikisha wapinzani hawaendi ikulu na si kulinda uhai wetu? iko wapi roho ya mtoto mchanga Bahati Yohana? Kosa Lake ni kuwa mlemavu wa ngozi? ulemavu wa ngozi ni dhambi kubwa Tanzania? Ghadhabu Ya Mungu itashuka juu ya Tanzania na hakuna atakayebaki salama, mauaji ya albino yamekuwa too much nasema serikali inahusika maana haiwezekani uwezo wa kuwadhibiti wauaji kuwakamata na kuwanyonga upo lakini serikali imekuwa kimya ikipiga dili za Escrow, Ni Tanzania tu dunia nzima ndo inaua ndugu zake, laana kubwa ya Cain aliyoipata kwa kumuua Abel, mnadhani Mungu atakubali ujinga na ufedhuli huu? Nakuuliza rais Kikwete,mbona wauaji wa kamanda Barlow Walikamatwa Haraka Sana? kwa nini wauaji wa ndugu zetu hawakatwi? TISS iko wapi? rais Kikwete Kwanini Hivi
 
Mada kama hii nilishawahi kuileta hapa ikaondolewa,

Sijui ni vigezo vipi ilikosa, ila ilikuwa na ushahidi wa picha zakichawi za ccm
 
Hupigwi ban na wala siredi haifutwi! Nakuhakikishia
 
Mada kama hii nilishawahi kuileta hapa ikaondolewa,

Sijui ni vigezo vipi ilikosa, ila ilikuwa na ushahidi wa picha zakichawi za ccm

Walitoa Kwa Sababu Ni Kweli CCM ndo mtuhumiwa namba moja,sidhani na hii kama itakaa.
 
Hakuna mwenyeakili mmoja akatuongonza nchini ili tuishi kwa amani kama enzi za Nyerere huyu dr Slaa kama anaweza leta tumaini jipya kwa kukamata washenzi wote.
 
Kweli inasikitisha sana, mtoto mwenyewe ana mwaka mmoja na kitu, hafahamu lolote lakini anafanyiwa kitendo ambacho ni cha kinyama na kinavunja haki ya ubinadamu!!
 

Ndo maana nikauliza https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...o-waombe-hifadhi-ya-ukimbizi-nje-ya-nchi.html
 
Ofcoz huwa kuna mkono wawatu tena wakubwa tu,kwani wangeamua kulikomesha hilo wala lisingechukua mda mrefu kiasi hiki,shida ni kuwa hata baadhi ya viongozi wa kubwa nao eanaamini kunufaika ma viungo hivo ndio maana hayaishi!!!
 
Mabaki ya maiti ya mtoto albino aliyepokwa toka kwa mamayake ambaye alijeruhiwa vibaya na kalazwa
Pesa madaraka cheo na umaarufu vimeleta ukatili huu
LAKINI MUNGU ANAONA NA ANASIKIA KILIO CHAO WASIO NA NGUVU
 
Binafsi nimesikitishwa sana na mauaji ya ndugu zetu Albino na watu wenye roho za kishetani, juzi alipokamatwa huyu mtoto nilisomo kwenye internet nikadhani wamerudia habari ile ya mwanzo. leo nasoma tena mtoto aliyetekwa Tanzania akutwa amefariki na viungo vimechukuliwa. ukisoma comments za wazungu utatamani uhame nchi jinsi wanavyotushangaa ! mtu gani ambaye hajali maumivu ya mama kunyang'anywa mtoto anaenda kuuwawa eti kumletea bahati mwingine.

Ombi langu
watanzani wa Dini zote tufanye Ibada ya pamoja kwa ajili ya vitendo hivi na kuomba adhabu kwa hawa watu mbele za Mungu. Mbeya walifanya hiki kitendo katika mji wa Tukuyu; unajua nini kilitokea, ni kwamba baada ya ile ibada( ilirushwa ITV 2012) wanafunzi wa shule ya msingi wakaanza kuongea (wao kwa wao katika maongezi yao); ' yule mbaba alienda nae kule mtoni wakati giza linaanza akamuua, n.k wote wakakamatwe na mchoro mzima ukajulikana, wengine walioshiriki ni watanashati balaa.
naomba kama Taifa tufanye hivyo ! viongozi na watumishi wa Mungu mnaosoma hapa hapa hepu tekelezeni jukumu hili muhimu tafadhali . Mungu ni mwema na hashindwi na lolote
naomba kuwasilisha.
 
Inahuzunisha sana, ndugu zetu Albino wamefanywa kama wanyama.
Hii ishu ya mauaji ya Albino huwa inashika kasi zaidi kila chaguzi za kiserikali zinapokaribia, Je serikali inaweza kutusaidia katika hili??, Nadhani kilichobaki ni sisi wananchi kuchukua sheria mikononi mwetu kutetea na kuulinda uhai wa ndugu zetu Albino.
 
Siri nzito kuhusu genge la mauaji ya albino zaanza kufichukaNa Julius Sazia, Shinyanga



Wanabodi, Mwenye infoz za Huyu Mfanyabiasha wa IGUNGA tafadhali tuwekeeni hapa... Inaelekea Master-mind wa Mauaji makubwa ya watanzania Yuko igunga...!

Mkuu hii habari iliishia wapi? je huyo mfanyabiashara kubwa wa Kule Igunga alitajwa? maana kwa jinsi nchi hii ilivyo inawezekana kabisa hakuna ilichofanyika na ndio maana matukio bado yapo kama lile la Mwanza na la juzi kule Geita kwani kiuhalisia inaonyesha tunaotaka wahusike kutusaidia kupambana na mauaji haya ndio haohao wanaoua hao Albino na ndio watumiaji wakubwa wa viungo hivyo.
 

Ki sayansi ni sawa ulichokiandika lakini kishetani na kinguvu za giza wanapingana na hoja yako kwani kama wangekuwa hawafanikiwi sidhani kama mauaji haya yangeendelea.
 
Jana Nilileta Mada Hapa Kuwa Ni ccm ndo inaua hawa watu Nashangaa Sana Mods Wameifuta,nilisema Dhahiri Kabisa Kuwa Mungu Kamwe Hataiacha Salama Tanzania Lazima Kuna Jambo Baya Sana Litaitokea Hii Nchi,nasema Tena Ghadhabu Ya Mungu Ipo Ktk Tanzania,tusubiri Tuone!
 
Kwa macho ya kitoto,aliwatazama,akajawa hofu. Alilia kitoto,kiganja cha mtu mzima, kikakibana kabisa kinywa cha mtoto Bahati.Sauti yake haikusikika kabisa.

Bahati hakujua kama yeye ni albino. Kwa akili za kitoto, saikolojia ya watoto, yeye alijiona salama mikononi mwa mama yake. joto la kifua cha mama, joto la manyonyo ya mama lilimburudisha na kujiona anapendwa tena yu salama.

Wanaume hawa wamemkaba...akiwa hai wanamnyofoa mikono mara miguu, maumivu makali ya visu na mapanga ya buchani yanasikika yakitenga ngozi, maumivu yanaingia ndani kwenye nyama na misuli,panga na kisu kinapogusa mfupa mchanga wa mtoto Bahati. Moyo mchanga wa Bahati unazimika. Hatimaye Bahati wa Geita kakata roho!!!

Bahati ameuawa hajui kama yeye ni albino.
Bahati ameishi mwaka mmoja na miezi miwili tu tangu aje duniani....
Kumbe Bahati hakujua kwamba yeye ni 'deal'.

Mwaka 2009 waliwauwa albino wengi tu...
Wanausaka utajili...
Wauaji na wanasaka vyeo vya kisiasa...

Vyeo na utajili uliojaa damu za albino....
Utajili na vyeo vyenye vilio na laana ya dunia yote.
Mabara matano ya dunia hii yamelaani mauaji haya. Visiwa vimelaani roho hii ya uroho wa madaraka na utajili ivumayo Tanzania.
 
You are right man, that's only way forward

Mkuu Naona kama vile serikali inaona kuna utata (controversy/ sensitivity fulani) kuanika jambo hili kwa kuelimisha jamii juu yatizo hii. Hatuwezi kuliacha likawa ni la kusuhughulikiwa na polisi na wanasiasa tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…