wiseboy.
JF-Expert Member
- Aug 11, 2014
- 2,932
- 4,544
Nasikitika kuona serikali inameshindwa kulinda maisha ya hawa ndugu zetu, unyama gani huu? TISS kazi yake ni kuhakikisha wapinzani hawaendi ikulu na si kulinda uhai wetu? iko wapi roho ya mtoto mchanga Bahati Yohana? Kosa Lake ni kuwa mlemavu wa ngozi? ulemavu wa ngozi ni dhambi kubwa Tanzania? Ghadhabu Ya Mungu itashuka juu ya Tanzania na hakuna atakayebaki salama, mauaji ya albino yamekuwa too much nasema serikali inahusika maana haiwezekani uwezo wa kuwadhibiti wauaji kuwakamata na kuwanyonga upo lakini serikali imekuwa kimya ikipiga dili za Escrow, Ni Tanzania tu dunia nzima ndo inaua ndugu zake, laana kubwa ya Cain aliyoipata kwa kumuua Abel, mnadhani Mungu atakubali ujinga na ufedhuli huu? Nakuuliza rais Kikwete,mbona wauaji wa kamanda Barlow Walikamatwa Haraka Sana? kwa nini wauaji wa ndugu zetu hawakatwi? TISS iko wapi? rais Kikwete Kwanini Hivi
