Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Kwa macho ya kitoto,aliwatazama,akajawa hofu. Alilia kitoto,kiganja cha mtu mzima, kikakibana kabisa kinywa cha mtoto Yohana Bahati.Sauti yake haikusikika kabisa.

Yohana Bahati hakujua kama yeye ni albino. Kwa akili za kitoto, saikolojia ya watoto, yeye alijiona salama mikononi mwa mama yake. joto la kifua cha mama, joto la manyonyo ya mama lilimburudisha na kujiona anapendwa tena yu salama.

Wanaume hawa wamemkaba...akiwa hai wanamnyofoa mikono mara miguu, maumivu makali ya visu na mapanga ya buchani yanasikika yakitenga ngozi, maumivu yanaingia ndani kwenye nyama na misuli,panga na kisu kinapogusa mfupa mchanga wa mtoto Yohana Bahati. Moyo mchanga wa Bahati unazimika. Hatimaye Bahati wa Geita kakata roho!!!

Yohana Bahati ameuawa hajui kama yeye ni albino.
Bahati ameishi mwaka mmoja na miezi miwili tu tangu aje duniani....
Kumbe Bahati hakujua kwamba yeye ni 'deal'.

Haya sasa mumeuuwa, Njooni...pandeni majukwaa ya kisiasa, tuwape "KULA" zetu. Pandeni jukwaani.
Mngetaka "KURA" zetu, MUSINGEMUUWA mtoto albino Yohana Bahati.

Mwaka 2009 waliwauwa albino wengi tu...
Wanausaka utajili...
Wauaji na wateja wanasaka vyeo vya kisiasa...

Vyeo na utajili uliojaa damu za albino....
Utajili na vyeo vyenye vilio na laana ya dunia yote.
Mabara matano ya dunia hii yamelaani mauaji haya. Visiwa vimelaani roho hii ya uroho wa madaraka na utajili ivumayo Tanzania.

Kwa heri, buriani mtoto Yohana Bahati...kifuani mwa Ibrahimu tutakuona. Pumzika mtoto mzuri...Bwana atakufuta machozi yako...usilie pumzika,,,nyamaza...Kisasi ni cha BWANA!!!
 
Na kweli kisasi ni cha Mungu..........Ole wake alitenda hayo maana atajutia siku aliyoletwa DUNIANI na MWANAMKE aliyemleta DUNIANI.............Atailaani siku aliyokuja DUNIANI................Ole wake na ole wao wale wayatendayo haya............:shock::hurt:
 
Inauma sana sana binadamu wamekuwa na roho mbaya kuliko shetani
 
1954tanu umeniliza...rest in Everlasting Peace Johana Bahati
 
Last edited by a moderator:

Hilo siyo suluhisho, kwani kwani hata kama ukifanya hivyo na kuwaondoa hawa watoto wenye ulemavu wa ngozi TZ basi tutahamia kwenye imani nyingine labda safari hii itakuwa watu wenye vipara, au sijui watu wanaopata mvi wakiwa wadogo tutaamini kama tunavyoaamini sasa hivi kwamba viungo vyao vina nguvu za ajabu!

Kitu cha kwanza kufanyika sasa hivi na kifanyike mara moja kwa ni serikali kutumia nguvu na kuwaorodhesha hawa watoto wote na kuwaweka boarding school kwenye ulinzi wa masaa 24 halafu hatua ya pili ni kuanza kwa Serikali ikishirikiana na Viongozi wa Dini kuelimisha watu kwamba hakuna kitu kama ushirikina na kuuondoa kabisa lkn hii kazi ngumu inahitaji muda, ila hilo la kwanza liko ndani ya uwezo Serikali na linaweza kufanyika hata sasa hivi ni swala la Pinda na Kikwete kutoa amri tu lkn sasa ni ngumu kwa maana Kikwete na Pinda ndiyo wauwaji wakubwa wa hawa watoto hivyo hawawezi kufanya chochote!
 

Kwa kweli haya matukio yananisikitisha sana mpaka natokwa na machozi,Yohana alijua kaja duniani kwa wasamaria wema,watu walioumbwa kwa mfano wa Mungu,kumbe kaja duniani kwa wakatili,wenye imani kuwa wataishi milele kupitia viungo vyake.Hakuwatutukana,na hata hata walimpomteka yeye bado aliamini yuko kwenye mikono ya watu salama hadi pale aliposikia maumivu ya kukatwa viungo vyake ndipo pengine kajiuliza hapa nipo wapi! Haya sasa waende wakapate huo utajiri,umaarufu na vyeo wanavyohitaji na kisha waishi milele hapa duniani wao na familia zao kwasababu wao ndiyo wanastahili kuishi hapa kuliko Yohana. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU YOHANA MAHALI PEMA PEPONI.Amina.
 
Watu wana roho za kikatili sana!
Pumzika kwa amani malaika Yohana Bahati.
 
Dah, yani nimelia. Its very sad. Halafu sijui jwa nini hii mijitu miovu inaishi maisha marefu.
 
Pumzika kwa amani Bahati, Hakika ungepata fursa ya kukua na kuwa mtu mzima naamini usingekuwa CCM hata dk moja. IMESHINDWA KUKULINDA na kuchangia mauaji yako. Pumzika BAHATI
 
Kwa kweli duniani pamekua ni mahali pa ajabu kabisaa kwa nini watu hawapendi binadamu wenzao kiasi hiki?! Mungu ampokee na ailaze roho yake Yohana mahali pema peponi Ameni
 
Inahuzunisha sana na ningekuwa na mamlaka yoyote ningepiga marufuku waganga wa kienyeji.Mungu ailaze mahali salama roho ya malaika Yohana Bahati
 
Serikali yetu itakuwa ni ya Ajabu sana Endapo haitatoa Tamko la Maana kuhusu Mauaji ya Bahati!
Tanzania si salama tena. R.I.P Bahati!!...
 
Kwa kweli duniani pamekua ni mahali pa ajabu kabisaa kwa nini watu hawapendi binadamu wenzao kiasi hiki?! Mungu ampokee na ailaze roho yake Yohana mahali pema peponi Ameni

Inaonyesha ni kwa kiasi gani MTANZANIA wa kawaida au maskini hatakiwi kuishi ,wanaotakiwa kuishi ni VIONGOZI,WABUNGE,RAIS na watu wa familia zao....

Vinginevyo WATANZANIA tungelindwa na POLISI bila kujali ITIKADI zetu ,vilema vyetu,dini zetu,makabila yetu au uwezo wetu..........Tumefikishwa hapa na CCM...................
 
 
[Nashanga sana POLISI WETU NA INTELIJENSIA YOTE WANAWAACHA RAIA WAKE WANAUAWA. Iweje Polisi wetu wanaweza kupata taarifa za kiintelijensia kuhusiana na maandamano fulani ya wapinzani yataleta maafa lakini wanashindwa kutumia intelijensia kupata habario ya uwezekano wa maauwaji ya Albino, kisha wafanye ulinzi.

Napata shida sana kuwaeleqa hawa jamaa
 
Jamani naona ifike mahali utajiri wa watu wa kiajabu ajabu uchunguzwe. Mtu unakuta ana ishi maisha ya kuokota okota, elimu hana, biashara anayofanya hatujui au waweza kuta eti ana kiduka ila vuup ndani ya mwaka mmoja mnashangaa anaporomosha ligorofa na kusukuma migari ya hundreds of millions. Ila jamii haijiulizi. Zaidi anatukuzwa kuwa ni jembe na mpiganaji. Hii migorofa inayoahushwa mjini na watu binafsi kila kikicha ni vizuri kufanya tathmini hela ya kufanya hivyo mtu amatoa wapi?
I am not hating, wapo wanaostahili kuwa nayo kutokana na juhudi zao binafsi lakini ni maoni yangu wengi wao sio kwa njia halali. Tutakapoacha kutukuza utajiri bila kutathmini umetoka wapi, kusifia maendeleo bila vithibitisho vya utendaji kazi na ubunifu basi mambo kama haya hayataacha kuendelea na Taifa letu kudharaulika na kuo ekana kama wanyama hapa duniani. TUBADILIKE. Mimi nawaangalia with suspicion watu wote wenye utajiri mkubwa bila concrete evidence ya biashara yao wafanyazo.
Ukija kwenye siasa, sitaki taja majina ila kuna watu hata kumpa cheo cha usimamizi wa choo cha kulipia huwezi kutokana na weledi mdogo walionao lakini utashangaa wako kuanzia kwenye kutunga katiba, uwaziri, ubunge ukuu wa wilaya nakadhalika halafu tunawashangilia na kuwasifia kwa kupata vyeo hivyo wakati ni wajinga wahuni na tunaona wazi kabisa,!
Nchi yetu ya ajabu sana. ------ thrive while the rightoues perish. Unlesa this changes we as a nation are doomed.
 
Malaika yohana miezi tisa aliyokaa tumboni kwa mama yake alikuwa salama zaidi kuliko mwaka mmoja na miezi mawili aliyoishi kwenye dunia iliyojaa udhalimu wa hali ya juu. Kamwe hakupata nafasi ya kujitetea wala kuwajua wema na wabaya.
Alitabasamu na kucheka na kila aliyekatiza mbele ya macho yake bila kujua kama ana nia nzuri au mbaya. Kamwe asingekubali kuja duniani kama angeyajua haya.
Ameondoka akiwa hajui maumivu aliyobaki nayo mama yake ni makali zaidi ya aliyoyapata kipindi anamleta katika hii dunia iliyojaa madhalimu wakatishaji wa roho za watu ili wafanikiwe mambo yao.
Laiti mama yake angeyajua hayo yatakuja kutokea angetafuta namna ya kukukinga ila aliowaamini wameenda kinyume na matarajio yake.
Ameondoka na Kamwe hatutamuona tena yatabaki maumivu yasiyokoma ndani ya mioyo yetu.
Roho ya kisasi ya Mungu i juu yao. Pumzika kwa amani malaika yohana bahati.
 
One day your eyes will open,
And your mind will learn,
Your ears will hear,
And your heart will feel,
With pain and shame,
You will learn what you are.

By Jwani Mwaikusa.

Pole mama,RIP kijana wetu.
 
Mauaji ya albino sio kushindwa kwa serikali bali kushindwa kwa baadhi ya wananchi kujitambua.
 
Mauaji ya albino sio kushindwa kwa serikali bali kushindwa kwa baadhi ya wananchi kujitambua.

Ni kweli kabisa, serikali yako ni kusubiri kodi na kula rushwa, ufisadi then ducks kwa kwenda mbele.
Wananchi watajipanga wenyewe.

Hongera kwa kujisema mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…