Nimeona kupitia vyombo vyetu vya habari, ndugu zetu Albino wa ukanda wa ziwa, wakilalamika kuwa wanahisi kuwa wanasiasa wetu wa nchi hii, wanathamini maisha ya Tembo wetu kwenye mbuga mbalimbali za Taifa wasiteketee, lakini wakati huo huo hawajali jinsi Albino wanavyozidi kuteketezwa kwenye nchi hii kila kukicha!
Wametoa mfano kuwa wakati tembo wetu walipokuwa wakiteketezwa kiasi cha kutisha kwenye mbuga zetu, wanasiasa wetu walianzisha Operesheni Tokomeza Majangili, lakini wakati huo huo hawajashuhudia hapa nchini, pamoja na Albino wanazidi kuteketezwa, hakuna wakati wowote wanasiasa wetu, wamekuja na mkakati wa Operesheni Tokomeza Wauaji wa Albino.
Kwa mazingira hayo, naamini kwa mtu yeyote ataungana mkono na Albino hao kuwa wako sahihi kuhisi kuwa maisha ya Tembo wetu kwenye mbuga za wanyama yana thamani zaidi, kuliko maisha ya binadamu wenzetu Albino!
Vile vile tunapata ushahidi wa mazingira kuwa masterminders wa mauaji ya Albino hawa, ni wanasiasa wetu,kwa imani za kishirikina kuwa viungo vya Albino vitawapa 'mvuto' mkubwa sana, kiasi kuwa watapata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Ushahidi huo wa mazingira kuwa main suspects wa mauaji haya ya Albino kuwa ni wanasiasa wetu unazidi kupata nguvu, kwa kuwa rate ya kuuawa Albino huwa inapanda sana, kila ifikapo mwaka wowote wa uchaguzi mkuu.
Hebu tulijadili kwa pamoja suala hili zito sana linalohusu uhai wa binadamu wenzetu, unavyozidi kuteketezwa na watanzania wenzetu, kwa kile kinachoonekana ni kwa ajili ya imani za kishirikina.