Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,752
- 7,861
Jamani, hivi solution ya mauaji ya albino ni nini? ina maana selikali imeshindwa? au kwasababu viongozi wenyewe ndo wanashindaga huko kwa waganga na wametandaza hirizi kwenye viono vya vitambi vyao mle ndo maana wanasuasua kulimaliza?
Hawa waganga ni kuwafuta tu ili tz tusiwe na kitu inaitwa waganga wa jadi. kwasababu hawa walianza kuwaula watu wenye vipara na viungo vyao kupelekwa kwa waganga. watu wenye vipara walikuwa na wakatu mgumu sana nakumbuka kipindi fulani. ikaja watu kuchunana ngozi na kuipeleka kwa mganga. kule mbeya kulikuwa na upigaji watu nondo halafu ile nondo wanasema inapelekwa kwa mganga wa jadi aiuze kwa wenye mabusha ati ile damu aliyompiganayo mtu nyama zitatoka sana. wamekuja kwenye kung'ofoa viungo vya siri na kuviuza, hawa waganga wa nini? we need to solve this prob as soon as possible,
kwasababu, kuna siku wakimaliza albino, wataanza watu warefu na mangongochi kama sisis, wakimaliza hao watakuja watu wafupi, pengine watakuwa watu wanene, itafika kipindi yaani hapakaliki...hahaha. sasa hawa waganga wana nini haswa hata kutuyumbisha kiasi hiki? wahusika wa dola wanashindwa nini kuwashughulikia hawa watu, hivi waganga wa kienyeji wana faida kweli hapa tz? mbona ulaya watu wanaishi tu bila hawa waganga bwana....mi naona tuwafute, sheria itungwe kukataza uganga zt. nyie mnasemaje wajemeni.
...hawa (waganga wa kienyeji) ni sawa na wale wanaopromote ethnic cleansing! Tatizo nilionalo kwa viongozi wetu kuogopa kukemea suala hili kwa ukali, au kulitungia sheria ni 'jinsi tulivyo' na imani potofu ya kuwaogopa/kuwasifia watu wa Sumbawanga, mlingotini, nk kwa madunguli yao!
Ndio tamaduni hiyo, it's here to stay!