Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,154
- 31,246
Darlene Krashoc alikuwa na ndoto ya kuwa mwanajeshi tangu angali mtoto. Alitaka kuwa kama mama yake ambaye naye alikuwa mwanajeshi na hivyo aliwataarifu wazazi wake kuwa anataka kutuma maombi ya kujiunga na jeshi kabla ya kumaliza masomo yake ya sekondari.
Kupatikana kwa Mwili wake
Kipindi anafariki, Darlene alikuwa akifanya kazi kwenye kampuni ya jeshi inayohusika na matengenezo huko Fort Carson Colorado. Watu wengi walikuwa wakisema ni binti anayependwa na wengi na mwenye roho nzuri.
Tarehe 17, Machi mwaka 1987, maafisa wawili wa jeshi walikuwa wakifanya lindo kama kawaida yao nyakati za saa 11 asubuhi amapo afisa mmoja aliona kitu kinachofanana na mdoli unaotumika kuonyesha nguo dukani. Waliposogea karibu na kutazama waligundua kwamba kumbe ulikuwa mwili wa mwanamke.
Mwanamke huyo alikuwa kalala chali, pembeni ya kifaa cha kuhifadhia taka katika maegesho yaliyopo nyuma ya jengo lenye maduka (shopping mall). Shingoni kwake kulikuwa na waya imezungushwa. Mwili wake ulikuwa na majeraha makubwa. Pia alikuwa na damu puani na mdomoni, michubuko kadhaa na alama za kung’atwa mwilini, na jicho lake la kulia lilikuwa limepasuliwa.
Mwili wa mwanamke huyo haukuwa na nguo kabisa. Alikuwa ana chupi ya kijivu iliyoteremshwa hadi kwenye vifundo vya miguu yake, na pia mguu wae wa kushoto alikuwa kavaa soksi na pia alikuwa abdo kavaa saa na pete. Pia kiatu kilipatikana karibu na kichwa cha mwili huo.
Kwa mazingira haya, askari hawakuwa na shaka kuwa uhalifu huu ulihusisha ngono.
Mazingira ya eneo lilizonguko mwili huo
Katika eneo ambapo ulipatikana mwili huo hakukuwepo damu, hivyo askari walijua kwamba huyo mwanamke atakuwa kauawa mahali pengine na kisha mwili wake kutupwa hapo. Waliamini kwamba mhusika alitaka kutupa mwili wake kwenye tanki la kuhifadhia taka ila bahati mbaya kwake ni kwamba lilikuwa lilmefungwa kwa kufuli.
Askari walipitia ushahidi wote wa eneo. Kulikuwa na henga za nguo, vipande vya sigara na nguo na vyote vilikusanywa. Mwaka huo 1987, utaalamu wa masuala ya DNA ulikuwa bado haujafika kiwango kizuri ila askari walijua bila shaka vile vipande vya sigara atakuwa kaviacha muaji. Pia kulikuwa na alama za tairi za gari katika eneo hilo ambazo askari waliamini lilikuwa ni gari ya mhusika wa mauaji.
Chini ya kile kiatu kilichokuwa karibu na mwili, askari walipata leseni ya udereva ambayo ilikuwa na picha na jina la Darlene Krashoc, mtaalam wa mambi ya kijeshi. Wazazi wa Darlene walitumiwa taarifa juu ya kifo cha binti yao na waliumia sana. Walichukua usafiri wa ndege hadi Colorado kusaidia upelelezi wa kifo cha binti yao.
Uchunguzi wa mwili
Ripoti ya uchunguzi wa mwili ilibainisha sababu ya kifo chake kuwa ni kukosa hewa kwa kukabwa kwa kutumia waya wa henga. Pia alikuwa kabakwa. Pia mchunguzi aligundua majani makavu na udongo kwenye mwili ule sawa na ule uliokuwa pale mwili ulipopatikana. Pia shingo kwake kw nyuma kulikuwa na alama y kovu la jeraha la mviringo jambo lililoashiria kuwa alisukumwa kwenye kitu fulani.
Jeshi la polisi la Colorado lilishirikiana na kitengo cha uhalifu cha jeshi kutafuta mtu aliyetenda unyama huu. Jeshi la polisi lilizunguka maeneo yaliyo karibu na eneo ambapo mwili uliokotwa. Hakukuwa na shahidi yeyote aliyeona chochote. Lakini walipata taarifa kutoka kwa mmiliki wa baa kuwa wakati wanafunga baa mnamo saa 8 na dakika 25 usiku huo mwili haukuwepo.
Washukiwa
Askari walitaka kujua ni wapi alipokuwa Darlene siku ya mwisho ya maisha yake. Walipata taarifa kwamba kitengo chake kiliruhusiwa mapema kurudi nyumbani kwa sababu kulikuwa kuna taarifa kwamba kutakuwa na hali mbaya ya hewa. Darlene na wenzake wawili wa kiume alienda kupata ulabu katika klabu moja ya usiku inayojulikana kama Shuffles.
Klabu hiyo ilikuwa umbali wa maili 5 tu kutoka eneo mwili ulipokuwa umetupwa.
Askari walizungumza na wanaume wawili ambao Darlene alikuwa nao usiku huo. Mmojawapo alikuwa kiongozi wa kitengo chake, Erik Lord. Aliwaeleza askari kwamba yeye, Darlene na mwanajeshi mwingine ajulikanaye kama Robinson walikuwa pamoja karibu siku nzima. Lakini yeye Erik aliwaeleza wenzake kuwa angependa kuondoka kabla ya baa kufungwa ila Darlene yeye alitaka abaki. Erik aliondoka pale baa mara baada ya Darlene kupewa ofa ya lift kutoka kwa mwanaume ambaye wote hawakumfahamu.
Erik na Robinson wote walikuwa tayari kukaguliwa kama watapatikana na alama za majeraha na pia walitoa nywele na damu zao kwa ajili ya DNA. Robinson alipatikana na michubuko mgongoni lakini askari walipata taarifa kwamba Robinson alienda baa nyingine na kukutana na mwanamke mwingine ambaye alienda kulala naye. Na mwanamke huyo alithibitisha hilo.
Pia Erik na Robinson walifanyiwa jaribio la polygraph, na wote walifaulu. Askari kufikia hapa waliamini hawakuhusika na waliondolewa kwenye orodha ya washukiwa.
Mume wake
Baada ya askari kuachana na rafiki zake waligundua kuwa Darlene alikuwa kwenye mgogoro wa taraka na mumewe ajulikanaye ka Glenn.
Pia Glenn alionekana kuwa angefaidika na kifo cha Darlene kwa sababu ndiye angepata malipo ya bima ikiwa Darlenee angekufa.
Askari walimhoji Glenn na alisema kuwa yeye na Darlene walikuwa wako sawa na yeye tayari alikuwa kwenye mahusiano mapya ambayo alikuwa anayafurahia. Pia aliwaambia kuwa siku ya tukio yeye, mpenzi wake na marafiki walikuwa pamoja usiku wakiburudika hivyo isingewezekana kutenda uhalifu huo. Pia alikaguliwa ili kuona kama ana majeraha yoyote lakini hakupatikana hata na jeraha moja na marafiki waliweza kuthibitisha kuwa alikuwa nao.
Mshukiwa mwingine
Baada ya askari kukosa ushahidi, walipokea simu kutoka kwa mwanasheria fulani. Mwanasheria huyo alikuwa akimwakilisha mwanajeshi fulani ambaye alikuwa anatuhumiwa kumbaka mtu huko Ft. Carson.
Mwanasheria alianza kumtilia mashaka baada ya kuona majeraha kweye viganja vya mwanajeshi huyo ambaye alikuwa akizungumza mara kwa mara kuhusu mauaji ya Darlene. Na pia aliwambia askari kuwa mwanajeshi huyo alionekana kuwa na wasiwasi mkubwa sana.
Mwanajeshi huyo alihojiwa na akari, lakini alikana kuhusika na mauaji hayo. Alidai kuwa alijua kuhusu mauaji hayo kupitia vyombo vya habari.
Gari la mwanajeshi huyo lilipekuliwa. Kwenye gari, askari walikuwa henga za waya, koleo, na nyasi kavu. Pia walipata kopo la mviringo ambalo lilikuwa na rangi ya viatu. Kopo hilo lilikuwa na umbo sawa na lile kovu lililokuwa kwenye upande wa nyuma wa shingo ya Darlene.
Mwanaume huyo alikana kabisa kuhusika ka kifo cha Darlene na alifanyiwa jaribio la polygraphg na kufaulu. Aliwapatia askari nywele zake kwa ajili ya DNA. Askari walikosa ushahidi wa kumuunganisha moja kwa moja na mauaji hayo.
Kesi inashindwa kutatuliwa
Askari walishindwa kutatua kesi hii kwa miaka mingi. Mwaka 2005, baada ya maendeleo makubwa katika sayansi ya DNA ilifanya askari kufungua upya uchunguzi wa kesi hii.
Jennifer Coslin, mtalamu wa mambo ya bailojia katika kitengo cha maabara ya kuchunguza uhalifu ya jeshi la Marekani alifanyia uchunguzi wa DNA henga, nguo na vipande vya sigara vilivyokusanywa mwili ulikopatikana. Vitu hivi vilibainika kuwa na vinasaba (DNA) ya mwanaume ambaye hakutambulika. Matokeo haya yaliwekwa kwenye mfumo wa kulinganisha DNA (CODIS) lakini hakuna matokeo yoyote yaliyopatikana. Yani, hakuna mtu aliyekuwa na DNA kwenye huo mfumo aliyeonekana kuendana na DNA hiyo.
Pia DNA hiyo ililinganishwa na wale washukia wengine wa mwanzo, lakini hakuna iliyeendana naye.
Mwaka 2019, timu ya DNA ilisikia kuhusu kwamba kulikuwa sasa na uwezo wa kutumia DNA ya mtu mwingine kutambua ndugu zake. Hivyo, askari waliamua kutumia DNA waliyo nayo kujaribu kupata wanafamilia wa mhusika. Waliipa tenda hiyo maabara binafsi na baad aya mieiz 9 walipokea majibu.
DNA iliwaongoza polisi hadi kwa binamu wa mbali wa mwanaume anayeitwa Michael Whyte ambaye kwa mwaka 2019 tayari alikuwa na umri wa miaka 58. Mwaka 1987 alikuwa kampangiwa kituo cha kazi huko Ft. Carson na alikuwa Colorado wakati Darlene alipouawa.
Askari walishituka kwamba Michael hakuwa na rekodi yoyote ya uhalifu sasa ilikuwaje akafanya mauaji ya kikatili vile.
Kwa kipindi chote Michael alikuwa akiishi Colorado. Askari kanzu alimfuatilia na kuchukua kikombe alichotumia mgahawani kisha kilitumwa kwenye maabara kwa ajili ya DNA na DNA hiyo ilifanana kabisa na ile iliyokusanywa kwenye vitu vilivyokusanywa kwenye sehemu mwili ulikopatikana.
Haki inapatikana
Michael alikamatwa akiwa nyimbani na ilionekana kama vile alikuwa akijua ipo siku atakamatwa.
Mwaka 2021, kesi ya Michael ilianza kusikilizwa na kufungwa kifungo cha maisha.
========
Darlene Krashoc