Mauaji ya Evelyn Howells: Je alikuwa ni mama au balaa ya familia………?

pamoja sana mkuu Mtambuzi ...ili ni funzo kwetu sote kwamba tusiwafanyie ndivyo sivyo watoto kwani wanaumia ila hawana jnsi tu,so shetani atatumia mioyo yao kutuangamiza hata kama si kama ilivyotokea hapa.....RIP mama mkorofi...
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na huyu mama kunyanyasa familia yake, mme wake alikuwa na tamaa ya mali za mke wake kitu kilichomfanya kuwachochea watoto wake kumchukia mama yao mpa kufikia hatua ya kumuua. Jambo hili si zuri na si busara kupandikiza chuki kwa watoto hata km wazazi wamekosana.
 
Mtambuzi, umenifunza sana kupitia kesi hii. Wazazi hii kesi iwe ni shule tosha kwa upendo na upole kwa familia.
 
hawa watoto walikua na umri gani kiasi cha kuchukua maamuzi magumu kiasi hicho.?
 
kwa kweli hapa nimejifunza mengi sana. Asante sana Mtambuzi kwa kisa hiki.
 
Last edited by a moderator:


Pole sana, hiyo inatokea kwakuwa wakati wa utoto ndipo mtu hutengeneza bond na mzazi/ mlezi na hiyo hufanyika kupitia upendo tu, ukikosekana huo basi mtoto anakuona kama mtu baki (stranger), ndipo ukubwani mtu huyu unakuta haoni shida kutokuonana au kutomsalimu mzazi/ mlezi pia hupata shida ktk kuhusiana na watu. Wazazi tunajukumu kubwa sana la kulea watoto katika upendo maana kile unachokipanda kwa mtoto leo hakika utakivuna mbeleni
 
Ahsante mkuu kwa hili somo. Nimejifunza kitu ya kuwa waendesha mashtaka wa huko majuu wanajali kazi na kuona haki imetendeka kuliko maslahi yake. Na pia naamini wanaajiriwa watu makini kwa kufanya upelelzi na kuendesha kesi kutokana na kile alichofanyia uchunguzi na kutenda haki
 
Malezi ya watoto yanahitaji umakini, ukali si njia ya kuwafundisha watoto, pia upole ulopitiliza si njia nje, pia kupandikiza chuki kwa watoto ni jambo la hatari sana. Watoto hawa wanaingia matata kwa sababu ya malez mabaya walolelewa na wazazi wao. Mtambuzi kisa hiki kinasisimua sn pia kinamafundisho makubwa sn, kilicho mhimu kwetu ni kujifunza tusije kupotosha watoto zetu
 
Mkuu Mtambuzi tunakushukuru tena kwa kutuletea kesi hii yenye mafunzo lukuki.Ila nashauri kila mara umalizapo kuandika.. uwaelekeze members kuwa hakuna haja ya kuquote habari yote ili tu mtu aandike " Mtambuzi nakushukuru sana ila habari yenyewe ni ndefu".
 
Thanx @Mtamnbuzi kwa kweli wale wale tunaowaamini na kudhania hawawezi kutudhuru ndio wauaji wetu.
Jamani hii familia ni kiboko mama alikuwa mkali wakupindukia je angeweza kuwadhuru watoto wake ?
Nadhani mama alitaka kuwa komaza wawe raia bora na wasijibweteke.

Baba na huyu mtoto wake wa kwanza ndio makatiri na wauaji wakubwa!

Eh mungu pisha mbali.
 
kuna wakati mzazi anageuka nyoka kwa familia yake mwenyewe,hasa kitendo cha kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine kwa miaka zaidi ya kumi ni ubabe na ubinafsi uliokithiri.
 
Asante sana Bwana Mtambuzi kwa kisa hiki cha kiuhalifu. Kama kawaida ya binadamu twapaswa kukumbushana kutokana na makosa ambayo yamewatokea wenzetu yawe ni hasi au chanya. Kwa mlolongo mzima wa matukio juu ya shauri hili kuna mabo mengi yaliyojitokeza na ambayo twapasa jifunza.

1.Yatupasa kuishi maisha yetu kama sisi au kutovaa ngozi ya kondoo ilihali kiuhalisia sisi ni Chui: Yawezekana ikawa ngumu kuielewa lakini watoto wa mjini wanaiita kuwa black au white kwa maana ya kujipambanua waziwazi tabia zako bila ya kuficha baadhi ya tabia zako hasa zile mbaya huku ukiwaaminisha watu kuwa u mtu mwema. Hii inadhihirishwa na sura mbili za tabia alizokuwa nazo mama EVELIN HOWELLS. Kwanza alionekana ni mtu mwenye tabia njema sana nje ya nyumba yake na hasa kwa kundi la wafanyakazi wenzake. Lakini kwa upande mwingine mama huyu alikuwa na tabia mbaya; tabia za kikatili kwa kuwatesa wanae na tabia za kuwa mkali wa kupindukia kwa kuwafokea watoto kupita kiasi na kuwatolea maneno ya kukatisha tamaa.

2. Mifumo madhubuti ya kutambua wahalifu katika kesi: Bado tunaendelea kuona namna wenzetu walivyo advance katika masuala mazima ya kutafuta ushahidi kwa wahalifu kwa kutumia tape recoder kwa kuziweka pahala ambapo si rahisi hata ya mhalifu kufikiria kwamba kuna ufuatiliaji dhidi yake.

3. Muda mrefu kutoa uamuzi mahakamani:Kesi ya mauaji kufanyika kwa siku 19 tu ni kwa kuwa mtuhumiwa alikiri yeye mwenyewe kuwa ndiye aliyeyafanya mauaji ya mama yake mzazi. Lakini vilevile hii haisiti kutukumbusha namna ya kesi zetu zinavyochukua muda mrefu mahakamani kwa dai lililozoeleka kuwa upelelezi bado haujakamilika. Vyombo vyenye wajibu wa kushughulikia masuala ya uhalifu vyapaswa kufanya kazi yake kwa weledi zaidi ili haki za wahusika zipatikane katika muda muafaka.

4. Vifungo jela chini ya miaka 18: Nimekuwa interested sana na adhabu ya DAVID GLENN kuanza rasmi baada ya kufikisha miaka 18 kwani makosa aliyoyafanya na ndugu yake yalitendeka kabla ya kufikisha umri huo. Kilichonivutia zaidi ni kwamba si kwamba muda wote huo wa kusubiria hukumu yao watakuwa wakivinjari nje ya milango ya magereza, la hasha, watakuwa wakiwa kizuizini kusubiri muda wao wa kuanza kutumikia adhabu. Nadhani leo hii kusingekuwa na malumbano ya umri wa LULU (ELIZABETH MICHAEL - Kumbuka hii kesi ya mauaji ya KANUMBA THE GREAT). Kesi ingekuwa katika kusikiliza hoja nyingine tofauti na hii.

5.Njia isiyo sahihi ya kutoa yaliyo moyoni/maudhi: Haikuwa jambo jema kwa DAVIS na BABA YAKE kwa kula njama na kuchukua uamuzi wa kuitoa roho ya EVELIN HOWELLS kwa mabaya aliyokuwa akiyatenda. Zipo njia nyingi zilizo sahihi za kuepukana na uamuzi wa namna hii kubwa ikiwa ni kumuomba Mungu ayasimamie maombi yako kwake ili kumaliza matatizo.

6.Kuwa makini na ushiriki wa makosa ya kiuhalifu: Waweza kuwa na nia nzuri ya kuwasaidia ndugu, jamaa aua rafiki zako katika suala fulani lakini suala lenyewe likawa na sura ya kiuhalifu kwa kudhani kuwa hakutakuwa na tatizo lolote. No one knows kwani mwisho wa siku utaweza kujumuishwa katika kesi ukiwa mshiriki wa kosa. Mfano mzuri ni hizi kesi za kifisadi hapa nchini kwetu. Kesi ambazo wakuu wa idara na vitengo au watu wenye dhamana katika taasisi fulani zinawafanya baadhi ya wahasibu au wataalamu wa mambo ya fedha kuwa washiriki wa uhalifu. Mfano mwingine ni kesi za ubakaji: Anaweza shitakiwa mtu ambaye ametimiza vigezo vyote vya tendo la ubakaji kwa mtu aliyebakwa. Hata hivyo yawezekana kwa namna moja au nyingine akawa ametimiza vitendo hivyo kwa msaada wa watu tofauti tofauti kama vile mshiriki mmojawapo kumshika mtu anayebakwa ili mbakaji aweze kufanikisha tendo lake, mshiriki mwingine kumletea mipira ya kiume, mshiriki mwingine kuweka ulinzi ili mtu yeyote asitambua kama tukio la ubakaji linatokea na mwingine kujaribu kuweka sawa mazingira ya ubakaji ili mtu asiweze kutambua kama tukio hilo limefanyika. Wote hawa ni washiriki wa makosa na kimsingi ni wakosaji wa tendo la uhalifu. Haya ndiyo yaliyompata mdogo wake DAVIS ingawa uzito wa kosa lake ulimpunguzia adhabu.

The Lister - Ex Detective​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…