Mauaji ya Polisi: Gazeti la Jamhuri Laibua Chanzo Cha Ajabu!, "Makubwa!" Lapongezwa na "Jicho Letu"

Mauaji ya Polisi: Gazeti la Jamhuri Laibua Chanzo Cha Ajabu!, "Makubwa!" Lapongezwa na "Jicho Letu"

Safi sna hao ndo waandsh wa habari. Hongeren sn tens sn. Tunaomba vyombo vya ulnz na usalama wafanyie kaz hzo taarifa ukwel huko har n mbaya sn inaogofya na kuskitisha.
 
....Waswahili walishasema kuwa mficha maradhi kilio kutamuumbua...,

Acha niiishie hapo kwa sasa ntarudi bidae
 
Majambazi tu..kama wale waliovamia kituo cha polisi bukombe,wakati wa jk..ingekuwa leo hii uchunguzi wa kuuza magazeti pia ungesema ni boko haramu waliojipenyeza.
 
Mie nilijua tuuu tangu mwanzo issue kama hizi lazima ziwaangukie waislam tuu hata kama waliofanya matukio ni wakristo.walitengeneza story ya babu seyana ikafanikiwa itashindwa hii.
 
Siri ya mauaji | Gazeti la Jamhuri
Matukio ya ujambazi wa kutumia silaha, mauaji ya polisi na viongozi wa vijiji katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani, yanahusishwa na vikundi vya vijana wanaopata mafunzo kutoka kwenye kundi la al-Shabaab nchini Somalia, JAMHURI limefahamishwa.

Kwa miaka minne hadi mitano iliyopita, vijana kadhaa kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Rufiji, hasa Ikwiriri, wamekuwa wakisajiliwa na kundi hilo la kigaidi, huku wazazi wao wakiambulia ujira wa dola 3,000 za Marekani (zaidi ya Sh milioni 6).

Akizungumza na JAMHURI, mmoja wa wakazi wa Ikwiriri ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini kwa sababu za kiusalama, amesema kumekuwa na wimbi la vijana wenye umri wa miaka 16-25 kupelekwa kwenye mafunzo huko Somalia.

“Hapa Ikwiriri katika kipindi cha miaka kama mitano iliyopita kumekuwa na wimbi la vijana wadogo kupelekwa Somalia. Inasemekana wanakwenda kujiunga na kikundi cha al-Shabaab, lakini vijana hao wamekuwa wanapatikana kupitia kwa mawakala kadhaa kwenye misikiti.

“Si kweli kwamba polisi hapa Ikwiriri hawajui, maana hata ukifuatilia wale viongozi wa vijiji ambao wamekuwa wakitoa taarifa za vijana hao wamekuwa wakiuawa kwa staili inayofanana… sasa hapo unaweza kuona namna zoezi linavyokuwa gumu,” amesema.

Chanzo chetu kingine kimemtaja mtu ambaye jina lake tunalifupisha kwa kifupi kama S.B., kuwa ndiye hufanya kazi ya udalali wa kuwapeleka vijana hao nchini Somalia, huku wazazi wa watoto hao wakiambiwa kuna kazi wanakwenda kuifanya huko.

Chanzo hicho kimesema hata baada ya baadhi ya wenyeviti wa vijiji kupeleka taarifa za uhusika wa S.B. kilichofuata ni mauaji.

“S.B. alipotea hapa Ikwiriri kwa takribani miaka mitatu, hata baada ya kurejea amekuwa na mali nyingi. Mali ambazo si za kurithi na haziendani na utafutaji wa halali katika kipindi hicho kifupi. Yamekuwa yanasemwa mengi, lakini ukimgusa andaa sanda kabisa,” kimesema chanzo chetu.

Chanzo chetu kimeliambia JAMHURI kuwa vijana zaidi ya 27 kutoka maeneo mbalimbali wilayani Rufiji, wamechukuliwa kwenda kujiunga na al-Shabaab, chini ya udalali wa Bwana S.B.

Chanzo hicho kimesema mmoja na vijana ambaye alichukuliwa alishindwa aina ya kazi na akarudi.

Habari ambazo JAMHURI, limezipata zinaonesha kwamba kikundi hicho cha wauaji kimekuwa kikimtumia mtoto mdogo mwenye umri chini ya miaka 18, kuwapelekea chakula huko msituni eneo la Mparange wilayani Rufiji. Jina la mtoto huyo tunahifadhiwa kwa sababu za kitaaluma.

“Kijana huyo mdogo amekuwa akitumiwa na hao wauaji kuwapelekea chakula. Mtoto huyo amekuwa akiwahudumia pasipokuwa na simu. Akikamatwa huyo anaweza kusaidia sana upelelezi wa polisi… hapa kila mtu amejaa hofu kuhusu usalama,” kimesema chanzo chetu.



Ushauri

Baadhi ya wataalamu wa masuala ya usalama waliozungumza na JAMHURI wametoa ushauri kwa Serikali wa namna ya kukabiliana na wimbi la mauaji ya viongozi na polisi yanayoendelea Mkuranga, Kibiti na Rufuji mkoani Pwani.

Serikali inashauri wa kuwahusisha viongozi wa dini na wataalam wa saikolojia katika kutatua vitendo hivyo.

Akizungumza na JAMHURI, mchambuzi wa masuala ya usalama mwenye makazi yake Johannesburg, Afrika Kusini, ambaye kwa maudhui ya kiusalama tunamtambulisha kwa jina moja la Alexandre, anasema sehemu kubwa ya Afrika Mashariki inakabiliwa na matatizo ya usalama, hivyo njia pekee ya kukabiliana na tatizo hilo ni kuzihusisha pande zote.

Alexandre, anasema kumekuwapo tatizo linalohusishwa na vitendo vya ujambazi (ugaidi) katika Pwani ya Bahari ya Hindi, ukanda wa Mombasa, Tanga, Zanzibar, Mtwara, Lindi na Dar es Salaam.

“Ninashauri kwamba mamlaka; hasa vyombo vya usalama visifikirie kuhusu ‘confrontation’ na vikundi hivyo…Polisi wanapowaua, hao ‘majambazi’ nao wanahakikisha wanalipa kisasi. Katika mambo kama hayo ni busara wanasaikolojia pamoja na viongozi wa dini wakaingilia kati.

“Wanasaikolojia wanatakiwa kufanya utafiti, kwanini matukio kama hayo yamekuwa yanajirudia katika eneo hilo hilo katika siku za hivi karibuni? Hapo inawezakana kukawa na jambo kubwa zaidi…” amesema.



Hali ilivyo Mkuranga, Kibiti na Rufiji

Hali ya usalama katika maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji imezidi kuwa ya wasiwasi, huku vyombo vya usalama vikiweka zuio katika maeneo hayo.

Baadhi ya mazuio hayo ni marufuku ya kuendesha pikipiki kuanzia saa 12:00 jioni, wananchi hasa maeneo ya Ikwiriri wilayani Rufiji wamekuwa wakitakiwa kulala mapema.

Akizungumza na JAMHURI, Mbunge wa Jimbo la Kibiti, Ally Ungando, anasema hali si nzuri kutokana na ukweli kwamba wananchi hata yeye mwenyewe wako katika sintofahamu ya kiusalama.

JAMHURI: Mheshimiwa Pole kwa yanayotokea jimboni kwako

UNGANDO: Asante sana kaka, nimeshapoa!

JAMHURI: Unaweza kuzungumzia kuhusu hali ya usalama jimboni kwako?

UNGANDO: Yaani katika hili, naomba nisiwe mzungumzaji maana mwenyewe niko katika ‘danger zone’ viongozi wangu wa vijiji wanauawa, huoni kwamba anayefuata hapo ni mimi? Nisingependa kulizungumzia hata kidogo, unanitafutia balaa, sitaki kuongea kwenye vyombo vya habari, maana nikiongea utaandika kwenye magazeti, na hao wenzetu (wauaji) wanasoma. Hapa mimi nasubiri hatma yangu kaka!

JAMHURI: Umeshapata ujumbe wowote kutoka kwa wauaji?

UNGANDO: Hata kama nimepata ujumbe siwezi kusema maana hali ya usalama imekuwa tishio kwangu na wananchi wenzangu. Jitihada za pamoja zinahitajika katika kutatua tatizo hili, si kazi ya mbunge pekee.

Wakati Mbunge wa Kibiti, akizungumza na JAMHURI, Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, yeye amesema hawezi kuzungumzia jambo hilo, badala yake anasubiri uchunguzi wa vyombo vya dola ukamilike.



Tukio la Kibiti

Tukio la wiki iliyopita, limechukua uhai wa polisi wanane. Nao ni Inspekta Peter Kigugu, F.3451 Koplo Francis, F.6990 PC Haruna, G.3247 PC Jackson, H.5503 PC Siwale, H.1872 PC Zacharia, H.7629 PC Maswi na H.7680 PC Ayoub.

Mauaji hayo ni mwendelezo wa matukio mengine saba ya aina hiyo yaliyotokea katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja mkoani Pwani.



Tukio la kuuawa kwa askari wanane limetokea ikiwa ni siku chache baada ya askari wa Jeshi la Polisi kuwaua kwa risasi wanaume watatu waliokuwa wamevalia baibui.

Wanaume hao ambao walikuwa na pikipiki mbili, walikuwa wakijaribu kukwepa vizuizi vya polisi vilivyokuwa vimewekwa katika Daraja la Mkapa.

Februari mwaka huu, watu watatu akiwamo Ofisa Upelelezi wa Wilaya (OC CID) ya Kibiti mkoani Pwani, Mrakibu wa Polisi, Peter Kubezya, waliuawa kwa risasi.
 
Kka Pascal Mayalla , kama gazeti la Jamhuri kwa muda mfupi tu wameyajua hayo yote we unafikiri watu waSerikali (Usalama) hawajui?, wakati mwingine wanaweza kuacha hayo yanafanyika wakiwa kwenye mkakati wa kujua chanzo/Shina, maana wakikamatwa mapema ni vigumu kujua mtandao mzima
Haya mambo ya ugaidi yanatakiwa busara sana kuyafatilia, unaweza shangaa kusikia mfanyabiashara mkubwa kabisa anahusika kufadhiri vikundi hivyo, nadhani wahusika wanaunganisha nukta
 
Huu si ujambazi kwakweli,wakati mwingine tuwe wakweli. Kufumbia macho tatizo si Dawa ya kuepuka matatizo tuache uoga.
Hali hii itaongezeka iwapo vijana watazidi kukosa ajira na gharama za maisha zikizidi kupaa huku serikali ikikosa majibu ya maneno na vitendo.
 
Polisi na watu wa usalama kwa ujumla wao wanafahamu matukio yote ya ujambazi yanayotokea. Mambo mengine ya usalama si ya kuweka hadharani.
 
Jamhuri wamelitendea haki sana jambo hili, bila kujali ukweli wa taarifa yenyewe. Nimekuwa nikijiuliza kwanini wanahabari wetu hawajaenda hatua moja zaidi-kujua sababu za matukio haya, lakini nikakumbuka kilio cha Jerry Muro. Wakati akihojiwa na Salama, Muro alikiri kutamani kurudi tena ktk tasnia ya habari-japo wamiliki na mabosi wa habari hawamtaki. Moja ya sababu za Muro kutamani kurudi ni kukosekana kwa investigative journalism. Alitolea mfano sakata la IPTL/PAP/Tegeta Escrow lililokuwa linavuma wakati huo. Kwamba watu hawajui hata hiyo IPTL iko wapi na picha za mahali ilipo hiyo mitambo hazipo wakati kampuni hiyo ipo Tegeta tu hapo.

Huenda waandishi wetu hawakutaka kuchunguza kwa sababu za kiusalama, maana tuna kasumba ya kujifanya mabubu kwenye masuala ya usalama wa taifa kama ilivyoonekana bungeni. Lakini masuala haya yanapoachwa bila kushughulikiwa kwa muda mrefu kama suala la Kibiti huko pwani, lazima waandishi wa habari wachimbue. Lazima wahoji kwanini vyombo vya dola viko busy na upinzani wakati mambo ya msingi hawashughulikii? Press ilikuwa lazima washtuke pale askari wanaposema tukio la kuuawa askari 8 ni la ujambazi wakati hata siku moja haijapita ikiwa na maana hata uchunguzi haujafanyika. Hapa kuna cover-up. Hata kama walikuwa wanahofia usalama wao kama waandishi, wanapaswa kutambua kuwa hata hao magaidi wanapenda airtime, hawawezi kuwadhuru waandishi maana wanataka kufikisha ujumbe na ajenda zao.

Hongera sana gazeti la Jamhuri, mlichoripoti ndicho tulikuwa tunafikiria kinatendeka, lakini tulitamani kiwe uongo maana hatutaki tufike huko kama taifa. Endeleeni kulimulika jambo hili, vyombo vya dola havifanyi zenye maslahi kwa nchi bila kusukumwa na wanasiasa. Wanasiasa wanapoziba masikio, ni wakati wa media kuvituma vyombo vya dola kufanya kazi yenye maslahi kwa umma.
 
Haya ndio maajabu ya Tanzania!
Intelijensia ambayo huwa wanasema imeshindwa kubaini chanzo ila gazeti ndio limebaini!
Wonderful Tanzania
 
Ukiona mtu anakuambia Askari 8 wameuawa na majambazi na hakuna jambazi hata mmoja aliyejeruhiwa wala kuuawa wakati wa mapambano hayo, basi jua huyo mtu anakudanganya-hakuna jambazi mwenye uwezo huo wa medani za mapambano. Hapo ndipo alarm ya waandishi wetu ilitakiwa ipige kelele.
 
Ifikie hatua dini ya Kiislamu ifanye uchambuzi wa waumini wake maana kuna waislamu wema kiasi kwamba utatamani hata kusilimu na kuna hawa wanaovaa nyanya puzo bila hata kupepesa macho wana mafundisho ya kikatili sana. Nafahamu tatukanwa lkn niseme tu kuwa mie nimeishi Zanzibar na nilitafutiwa kazi na Wazanzibar waislamu wema. Mwisho ni waumini wote waislamu mtoe woga wa kuambiana mapungufu yenu kiitikadi, sie tulioko upande mwingine ukweli tunashindwa tu kuwaambia kuwa hao jamaa zenu wanawaharibia tu jina lenu kwa mafundisho ya hovyo kabisa
 
Kubenea na Mwanahalisi wanajiita waandishi wa habari za kiuchunguzi. Mbona hatuwaoni katika hili? Mwanahalisi ni kwa ajili ya jamii au ni kwa ajili ya wanasiasa fulani?
Hilo gazeti linamilikiwa na chama kwa mkakati maalumu
 
Mkuu Paskali ungetuwekea na ripoti yenyewe tuisome chief, wengine huku tulipo sio rahisi sana kulipata hilo gazeti........binafsi ningependa sana kujua chanzo, maana ukisema ni ujambazi haiingii akilini.
Kaweka, angalia vizuri. mimi nimeisoma yote.
 
  • Serikari (Raisi John Magufuli) na vyombo vya ulinzi na usalama wasipochukua hatua kali siku si nyingi pwani ya nchi yetu itakuwa haikaliki
  • Boko haram kule Nigeria ya kaskazini walianza hivi hivi, walikuwa wakiua kidogo kidogo na serikari yakule nayo ilikuwa ikisema ni uhalifu wa kawaida
 
Nimeiweka
Siri ya mauaji | Gazeti la Jamhuri

Na nimekiita cha ajabu kwa sababu Taifa limeaminishwa ni ujambazi lakini gazeti limetuwekea chanzo ni mengine makubwa ya ajabu!.

Paskali
Mkuu nimekuelewa Sana,

Ila unaweza nikumbusha Ni mambo lipi tumewah fanya kwa weledi Kama taifa na tukatekelez za maazimio yake?

Sawa, gazeti linasema wauaji wamepata mafunzo Somalia.... Hivi inaingia akilini kweli?

Sawa kipi cha kuamini, Gazeti ama ripoti ya polisi?

Hivi imefika mahali Jeshi letu la polisi haliaminiki tena?
 
mficha 'uchi' hazai, acha ukweli usemwe!
serikali si inasema ni 'ujambazi' wa kawaida tuu, ujambazi gani wa hivyo? yaani jambazi mmoja tuu analipiga tairi ya gari la polisi risasi 1 tuu, then gari lilikosa mwelekeo anauwa polisi 8???, jambazi gani huyoo??
 
Back
Top Bottom