Inatia moyo kuwa sauti zaidi zinazidi kusikika.
Kwamba:
"Machifu wa mkoa wa Mara nao pia wameomba kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu tukio la mauaji ya watu watatu yalitokea wilayani Serengeti waliouwawa kwa kupigwa risasi na askari polisi kwa tuhuma za ujambazi."
Hili ni jambo la kheri sana. Wito huu umfikie chifu mwenzao Hangaya popote kule aliko.
Inafahamika kuwa si nadra kwa polisi kujichukulia sheria mikononi na kuuwa au hata kuwapora watuhumiwa kinyume cha sheria.
Imethibitika sehemu nyingi kuwa walioporwa na hatimaye kuuwawa na polisi walikuwa wahanga wala hawakuwa majambazi.
Inawezekana hata Tarime ni yale yale ya Ifakara, Mtwara na kwingine kwingi.
NInakazia: ni aliye mhalifu pekee ndiye anayeweza kupinga kufanyika uchunguzi wa kuaminika kwenye kadhia kama hizi.
Source:
Machifu Mara wataka uchunguzi mauaji yaliyofanywa na polisi