Mauaji ya Polisi wetu ni Ujambazi, Ugaidi au Retaliation? Nini kifanyike kukomesha hali hii?

Inaumiza sana, watu wamechangia mengi mazuri. Swali langu mim ni hili ivi Kama mtu anaujasiri wa kuvamia gari ya police ikiwa kwenye mwendo anamlenga dereva, bila shaka huyu ni mjuzi wa kutumia silaha sasa kama si gaid ujuzi huu anautoa wapi + ujasiri bila kusahau roho mbaya? Pia swali lingine ninalo jiuliza ivi kweli watanzania tupo salama? Maana nionavyo mim huyu mtu angeamua kuua raia tu, si angemaliza kijiji kizima jmn?
 
Ni Ugaidi(Kulipiza Kisasi),Jeshi Letu Lijisahihishe kuondoa uhasama kati ya Raia na Wao.
King kong,unayosema yanafanana,matokeo mengi yanatokea ya raia kuuwawa halafu serikali kutojali,haya ndio ndio mazao yake ni haya,waliuwawa vijana kule mkuranga wakatupwa mto ruvu,na vile vile hivi karibuni masikini vijana wa kimasai nao waliuwawa mkoa wapwani,ni kweli jeshi letu lijisahihishe kuondoa uhasama na raia,serikali imekuwa haijali kuanzia vitendo vya utekaji na uvunjwaji wa sheria vinavyofanywa vyombo vya usalama,na polisi,bila ya kutolewa Kauli thabiti kutoka Kwa viongozi wakuu wa nchi,na badili yake kumekuwa na ubabe na propaganda za ukandamizaji,zinatolewa na viongozi wakuu wa polisi,serikali imekosa kuwapa haki zao hata wabunge waliochaguliwa na wananchi,kabla ya kuendelea kwanza natoa pole kwa wazee ndugu na jamaa waliopoteza Jamaa kattka tukio hili.
Amani haiwezi kupatikana bila ya kuwepo kwa kuaminiana baina ya raia na vyombo vya kulinda Usalama,nguvu na ukiukaji wa misingi ya sheria ya utawala bora,ni misuguano inayokiuka haki za kibinaadamu,naongezea kwamba katika siku za karibuni kumesikikana,mambo mengi yanayokiuka sheria na haki za uraia.
Ushauri kwa serikali
Kuwasiliana na wazee katika sehemu ambapo vitendo hivi vya uvunjifu wa amani vinatokea na kutengeneza na kuboresha mahusiano,Kwa wazee na vijana,ill kurejesha Imani iliyokuwepo kabla.
Jambo lingine ni serkali kuunda muundo mpya wa kisheria,Kwa kushirikiana na chama cha wanasheria,kuunda muundo mpya wa kisheria kuanzia polisi mpaka mahakamani,wilayani,mikoani,itakayoleta haki Kwa raia na vyombo vya usalama,bila ya upande wowote kuikandamiza haki ya upande mwingine,hii itapelekea kuleta imani Kwa wananchi na kuboresha amani.
Mwisho watanzania Kwa pamoja bila kujali itikadi za kidini,vyama vya siasa na jinsia,tuungane Kwa namna kupinga uvunjwaji wa amani,na tuwe tayari kuinunua amani Kwa thamani yoyote.
Mwenyenzi Mungu ibariki Tanzania
 
Kwa sababu mawazo mazuri yameshatolewa hapa mimi nitachukua shortcut moja tu
***JESHI LA POLISI LIFUMULIWE KABISA ***
tuweke uongozi wenye dira ya kuboresha uwezo wa polisi kivifaa, kielimu, kimkakati na kiakili.
Vision ya jeshi letu sasa hivi ni kukandamiza upinzani kwa matarajio ya kupata promotion.
Hao ndo wanapandikiza chuki dhidi yao wenyewe na dhidi ya serikali.
Naamini siku jeshi la polisi likiacha kufanya kazi kisiasa na upinzani unakufa Tanzania.
Tusifike pahali ambapo wananchi wa kawaida wanafurahia polisi kuuliwa.

Ni vigumu kujua motive ya hawa watu ila ukweli ni kwamba they are up to something big. Pengine wapo kwenye hatua za awali tu za a kukusanya silaha na polisi wetu ndio easy target kuliko ku-smuggle.

It doesn't matter kama huu ni ugaidi au ujambazi au vyovyote vile . The point is you have 8 SMGs in the wrong hands. Zisiporudishwa ndio huishia kufanya massacres kwenye majumuiko huko mbeleni.
Nashauri hivi
1. Jeshi la polisi (hapo mbeleni) watoe kauli ya kutofanya kazi kwa namna yenye harufu ya upendeleo wa kisiasa (kauli ya juu juu tu inatosha , sio lazima wa-admit kuwa huwa wanafanya hivyo!)
2. Jeshi la polisi litengene open channel ya kupokea anonymous tips,
4. Tuunde kikundi cha Rapid Containment Unit chenye vifaa na "akili" za ku-handle situations kama hizi (I mean wasio form four failures)
Ikitokea situations kama hizi ni kuweka lock-down hata kama ni wiki nzima na kutafuta wahalifu. (Hakuna kuingia ama kutoka bila kukaguliwa) wapewe helicopta yenye infra-red night vision technology)
5. Jeshi la polisi liandae forums/open consultation meetings na wananchi kutafuta maoni ya jinsi ya kushirikiana na jinsi ya kuboresha jeshi hilo


Sikitiko langu kubwa hasa ni kwamba mawazo mazuri yaliyotolewa humu Jf kutozingatiwa na wahusika.
 
Wao wapo busy na tochi tu,utawakuta trafki na polisi wa kawaida wooote wanahangaika na tochi tu
 
Shhhhhheeeeeeeednzzzzzzzzi nyangau kuna ngaruwe pori amehusisha haya mambo na dini ya Uislam halafu mtoa mada Thanks very objective ingeongelew ukatoliki wenu ungekuja kutoa povu hapa.
 
Kuhusisha mambo ya mauaji na dini ya uislam.
Beautifulgirl
ukinionyesha hata neno moja tuu kwenye thread yangu ambayo nimehusisha mauaji haya ya polisi na dini ya Kiislamu, nitakushukuru sana!.
Ukikosa hata neno moja tuu, then just say sorry na yaishe.

Humu jf tuko watu wengi wa makabila tofauti, umri tofauti na uwezo tofauti.
Kwa mtazamo wangu, wewe unaonyesha ni binti mdogo unaweza kuwa ni mwanangu wa kumzaa, hivyo mimi naweza kabisa kuwa ndiye baba yako, hivyo kumtukana baba yako au mtu wa umri wa baba yako bila kosa sio tuu ni kujichumia dhambi bali unajitafutia laana za bure!.

Ukijimlisha na kabila langu, kutukanwa na mwanamke ni dharau kubwa sana kwa kabila langu, hivyo nakushauri just say sorry kabla karma ya matukano yako hayajakushukia.

Paskali
 
Raia walitekwa kelele zikapigwa...
Wabunge walitekwa na wametishiwa kutekwa, kelele zikapigwa...

Wabunge wenye weledi wakataka kuwe na mjadala.

Viongozi wa wabunge wakasema hayo si mambo ya muhimu kujadiliwa.

Basi hata hili tuliache...tufanye kazi...tufanye kazi tu.
 
kuna watu hawatanielewa ila hayo ndio mapendekezo yangu. hii inaweza kusaidia kupunguza au kudhofisha hali ya mauaji ya raia yanayoendelea huko.

nawasilisha
 
Baada ya Mhe. Zitto kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kulichafua jeshi la polisi, nafanya tuu rejea ya kuangazia usafi wa jeshi letu la polisi.
Tuungane kuombea Zitto atendewe haki, lakini pia tusiache kulitaka jeshi letu la polisi, wajitathmini
Paskali.
 
Wanabodi, katika bandiko hili, niliilaumu amri hii ya JPM, lakini tukio la leo, la kichaa mmoja kutuulia polisi wetu 3 na mlinzi mmoja, leo sasa ndio nimegundua JPM aliona mbali.

Ningekuwa mimi ndio kiongozi wa operation ile, ningetumia snipers kumshoot strategic areas to destabilize him, ili abaki hai kwanza, and they make him talk before they are done with him ili tujue the motive and the ring. Kitendo cha kumalizana nae, there and then, then police have lost everything.

RIP askari wetu wa polisi, RIP Mlinzi wa kampuni binafsi, na pia RIP Jambazi, Gaidi, besides everything, he was a human being, he deserves some dignity!. Na kwa msio jua, hata Osama, pamoja na ufirauni wake wote aliofanya kwenye September 11, baada ya kuuwawa kikatili, mwili wake ulioshwa Kiislamu na kuswaliwa na Sheikh, kisha alizikwa Kiislamu na kutazamishwa kabila!.

Japo JPM, haupo nasi, lakini uliona mbali, amri yako ndio imeanza kutekelezwa, nakuomba Rais Mama Samia, ili kumuenzi JPM, wapandishe vyeo askari hao mashujaa.

P
 
Polisi wamemmaliza kuficha ushahidi....Jamaa inasemekana amedhulumiwa Madini Dhahabu na askari.
 
Polisi wamemmaliza kuficha ushahidi....Jamaa inasemekana amezulumiwa Madini Dhahabu na askari.
Tumuombe rais Mama Samia aunde Tume huru kulichunguza hili tukio. Inawezekana ni kweli jamaa alikuwa provoked, due to provocation akapata pseudo insanity, ndio akawawasha polisi waliomprovoke na kuzichukua silaha zao na kuwa target polisi tuu!.

Niliwahi kushauri

Kwa vile tayari kuna tuhuma za polisi kuhusika, you can't be a judge on your own case!.
RIP Askari wetu.
RIP Mtuhumiwa.
P.
 
Ndugu
nasikitika kukuambia kuwa uko very shallow na hii habar ya ugaidi mana unasema cjui majambazi wakat alikuwa mmoja

pili unaongea pumba , hakuna uhalisia wowote eti polisi wapewa license to kill wakati kila siku wanaua majambazi na huyo jamaa kauwawa .

katika uzi uloandikwa hauna kichwa wala miguu ni huu

Kuwa busy na vitu vingine
 
mzee usikurupuke eti raia wapenda amani

ushawahi ona ndugu yako anapigwa na polisi ?

polis!! wa sasa wamezidi tamaa na kubambikia watu kesi ,mm binafsi cjaumiaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…