Jambo mnalosahau ni kwamba, Wazawa, Waafrika Kusini, WALIPEWA nafasi za kusoma BURE, elimu madaraja yote, kuanzia chekechea hadi chuo kikuu! Walikataa! Wakaona bora waendelee kupeta, kufurahia UHURU wao! Nafasi pia za ajira ya upendeleo kwa Wazawa, zilitolewa. This is documented, Google it and you will find... Start with South African Affirmative Action Programmes.
Sasa, nafasi hizo ziliishia kati kati ya muda wa utawala wa Mbeki. Serikali yake iliona, kama watu wanapewa nafasi na wanazikataa, sasa waendelee kutumia pesa za walipa kodi kuendelea kutoa matangazo ya kuhamasisha bila response ni waste of time and much needed financial resources. Ni mfano wa utawala mbaya, kutumia fedha ambazo huoni matokeo yake. Wakaacha kutangaza, wakasitisha mipango hiyo miwili.
Sasa Wazawa wamejikuta, (i) hawana elimu na (ii) nafasi za kazi za upendeleo zimesitishwa. Walie na nani? Wageni!
Wameamua kuhamisha lawama za uzembe wao, kwa wageni, na kudai kwamba wageni ndio wamevamia ajira zao. Huo si ukweli hata kidogo!
Kumbukeni, hizi chuki dhidi ya wageni hazikuanza jana wala juzi. Zimeanza tangu miaka ya 90. Mimi nina kesi ambayo rafiki yangu mpendwa alipatwa na msiba, baada ya kaka yake (ambaye alikuwa ameishi RSA kwa takriban miaka 7) kuuwawa, baada ya kugundulika kuwa ni Mtanzania. Kaka yake huyo, kwa kuhofia kwamba angekuja kuuwawa kwa kujulikana kuwa si raia wa kule, aliamua kubadili jina, na kwa kuwa Wangoni ni kabila moja sawa na Wazulu, hakutofautiana kilugha na kwa matamshi, akawa anakubalika kama Mzulu.
Vijana fulani kule Capetown walimwonea wivu yeye na mchumba wake, ambaye alikuwa Mzulu Mzawa. Wakaanza kumpeleleza, wakagundua kwamba ni Mtanzania. Walimvamia usiku, wakamteka nyara, wakamsiliba kwa kumchoma visu na kumpiga, kisha wakamwashia risasi saba (risasi moja kwa kila mwaka alioishi RSA), na kuutupa mwili wake kwenye mojawapo ya fukwe za Capetown!
Baada ya siku tatu toka kupotea kwake, mwili wake ulionekana, na hatimaye maiti ikasafirishwa hadi nyumbani, akazikwa hapa Dar.
Sasa mnadhani kwamba sisi hatuna haki ya kuishi kule kwao? Mbona wao wako hapa, tena wengi, kila mkoa, na sisi hatuwafukuzi wala kuwafanyia fujo? Au na sisi tufanye kama wao wanavyofanya?
Mimi nimesema, TUWASUSIE! Vodacom, Shoprite, Game, Truworths, W Store, 4u2, Stanbic Bank, Tanzania Breweries, na kila kampuni inayojulikana ni ya Afrika Kusini, tusinunue bidhaa zao na tusitumie huduma zao. Nimesahau, kuna Blue Finance na Bayport Finance, labda Platinum Credit, lakini wamekuja pia hawa Instant Credit (
www.instantcredit.co.za), ambao nao wanastahili KUSUSIWA!
Hakuna jambo linaloweza kubadilisha fikra na maoni ya watu, kama kuwanyima mapato yao halali. Tukianza sisi, wapo wengine watakaofuatisha mwenendo wetu, hatimaye inaweza kuwa a GLOBAL CAMPAIGN! Think locally, act globally, for maximum effect!
Na ni TUSI kusema kwamba ndugu zetu waliopo RSA wanajihusisha na vitendo vya uhalifu. With WHAT FACTS? No research, no right to speak! Waje na concrete data, si uzushi!
A luta continua!
./Mwana wa Haki