Mauaji yatokea tena Kaskazini Mashariki mwa Congo

Mauaji yatokea tena Kaskazini Mashariki mwa Congo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Waasi wa kundi la ADF wameishambulia tena wilaya ya Beni Kaskazini mwashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kuuwa watu 22 katika tarafa za Ndombi na Kamango.
Symbolbild Opfer der ADF (Getty Images/AFP/K. Mailro)

Wakaazi wa wilaya ya Beni kwa mara nyingine wanahesabu maiti za wapendwa wao waliouawa kinyama na waasi wa ADF. Mmoja wa wakaazi aliyeponea chupuchupu katika eneo la Kamango, aliyezungumza na DW kwa njia ya simu, amesema walipoingia kijijini mwake waasi hao kutoka Uganda ADF walikuwa wakiuwa watu kiholela.

"Walipoingia walianza kuwafyetulia raia risasi, waliojeruhiwa ni wengi na waliouawa wapo. Milio ya risasi ilikuwa mingi kupita kiasi, jeshi liliingilia kati lakini lilichelewa kidogo. Isingelikuwa uingiliaji kati wa jeshi hilo, sote tungeliuwawa," alisema mmoja wa wakaazi wa Beni.

Mauwaji haya yanaendelea wakati jeshi la serikali linaendesha operesheni dhidi ya ADF, lakini wadadisi wa masuala ya usalama wanasema kuna uzembe katika uongozi wa jeshi hasa katika operesheni zinazotajwa na jeshi la Serikali kuwa ndio za mwisho kufanyika katika eneo hili, ili kuwatokomeza waasi wa ADF wanaowauwa watu kila uchao.

Mwanasheria Omar Kavota, mdadisi wa masuala ya usalama na akiwa pia naibu mwenyekiti wa mashirika ya kutetea haki za binaadamu CEPADHO, anahoji kwamba, mikakati ya kuwalindia usalama wakaazi katika viunga vya maeneo ya vita, haikupangwa vizuri kwani inajulikana wazi ya kwamba, ADF wanaposhambuliwa katika maeneo ya misitu, basi na wao wanawashambulia na kuwaua wakaazi katika maeneo ambayo operesheni bado hazijaanzishwa.

Ikumbukwe kuwa, katika ziara yake mjini Beni, na alipotangaza kwamba operesheni kabambe zitaanzishwa katika eneo hilo dhidi ya waasi wa ADF, rais Félix Tshisekedi aliwahi kuwaahidi wakaazi, kwamba waasi hao watatokomezwa kabla ya sherehe za Krismasi pamoja na mwaka mpya. Lakini ahadi hiyo inaonekana kubakia kuwa ndoto tu.
 
Mijitu mingine duniani ningekuwa na uwezo ningeyashushia moto wa volcano
Hao ADF kama wana nguvu kwanini wasiende vamia kambi za jeshi, wanakuwa kama waasi wa kiarabu nao yaani wanaenda kuuwa watu dhaifu wasio hata na silaha.
 
Nimekuja mbio nilifikiri Jiografia ya Tanzania.
Poleni!
 
Mijitu mingine duniani ningekuwa na uwezo ningeyashushia moto wa volcano
Hao ADF kama wana nguvu kwanini wasiende vamia kambi za jeshi, wanakuwa kama waasi wa kiarabu nao yaani wanaenda kuuwa watu dhaifu wasio hata na silaha.
Huyo mwandishi kalegeza tu, raia wengine waliuawa kwa kuchanjwa na shoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom