Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 471
- 1,217
Ulivyo wewe sivyo alivyo mwingine hivyo mtihani wa kwanza wa kupambana nao ni jinsi ya kuishi na watu bila wao kukuharibia siku yako.
Huu ni mtihani kwako kwa sababu wewe ndio unatakiwa ujifunze kuishi nao na sio wao wajifunze kuishi na wewe hivyo hawana habari utaumia au la ila wataishi vile walivyo .
Kuwa tu mwanaume tayari ni tofauti na mwanamke sio tu kibaolojia ila hata namna ya kuishi pamoja haiwezi kuwa sawa hivyo wanaoishi pamoja tayari huo ni mtihani kwa kila mmoja kuishi katika namna ambayo hutakuwa mtu wa msongo kila mara.
Kuna watu wamezidi kwenye tabia ngumu inaweza ikawa ni kibailojia ndivyo walivyo au hawana mafunzo ya namna ya kuishi na wengine sasa ukikutana na huyo kama huna uwezo wa kumpuuza jiandaye kushambuliwa na matatizo ya moyo.
Tatizo la magonjwa ya moyo linaonekana kuwa kubwa zaidi kwa wanaume kuliko wanawake kumbe kuwa tu mwanaume jua tayari una vita ya kupambana nayo usikubali kuwa mtu wa kukwazika kwa kila chukizo au kuchukulia kwa ukubwa kila kikwazo kuna mengine yaone kama yalivyo na yaache kama yalivyo ukisema upambane na changamoto utashindwa.
Mfano unamsalimia mtu hajaitika acha makisio ya kuumiza mwache alivyo yawezekana ana changamoto zake anapambana nazo.
Ghafla tu unaona mtu anakuchukia hapo sio suala lako kutafuta sababu utaumiza kichwa bure wewe mwache na chuki zake siku akiwa sawa mtacheka tena akiona sivyo basi kila mmoja ajali mambo yake.
Mambo muhimu uliyonayo ni mengi usiwe mtu wa kukimbizana na haiba za watu .