Me and me
JF-Expert Member
- Nov 13, 2023
- 226
- 496
Salaam,
Vipindi mbalimbali vya harakati za wanawake vinavyorushwa na Televisheni za hapa bongo vinavyoendeshwa na Watangazaji machachari Vina maudhui chonganishi(kwa mtazamo wangu).
Yaani Ni kama vinaonyesha au vinachochea Hali ya Ukinzani iliyopo kati ya Mwanaume na Mwanamke katika jamii ya hivi leo.
Naomba nizungumzie Hawa Watangazaji na waandaaji wa vipindi hivi kwanza kisha nihamie katika hayo maudhui yenyewe.
WAANDAAJI WA VIPINDI HIVYO
Ni Vipindi Vinavyooendeshwa na Wanawake machachari Wengi wao wameshajikatia Tamaa kuhusiana na masuala ya FAMILIA, MAADILI NA Maelewano.
Watangazaji hawa bila ya kupepesa macho wameshaamua kuyaacha Yale maadili ya kiafrika, Standard African Culture (Zingatia neno "standard") Wengine hadi zimeonekana Video clip zao wakiwa faragha Wakichukuliwa na Camera (nadhani mnamjua).
Mavazi, Tabia na Mienendo yao inayoenda Kinyume na Tamaduni rasmi za kiafrika ipo wazi kabisa Na Sidhani kama ni Sawa wao Kukabidhiwa jambo Muhimu linalogusa moja kwa moja Familia na Jamii Yetu. Vipindi Hivi Nilitegemea Vingekuwa vinaongozwa na Watu wenye Heshima katika jamii.
Pia nilitegemea Wageni wataokuwa wanaalikwa katika vipindi hivi wawe ni watu furani Furani ikiwemo Viongozi wa Dini wa Kike na wakiume Viongozi wa Kimila na Watu Furani furani wenye Muelekeo Mzuri katika Masuala ya Familia na wanaokubalika kwa hekma zao katika Jamii.
Nilitegemea Katika vipindi hivi Kuwe Kunazungumzwa namna Mwanamke atatambua Nafasi yake katika Kuboresha Familia, Namna Mwanamke atamtii na kumheshimu Mumewe. Namna Mwanamke atakuwa Mama mlezi bora wa Watoto wake, namna Mwanamke atamsaidia mumewe kujikwamua kiuchumi na isiwe sababu ya Yeye kuwa Kikwazo cha Maendeleo katika Familia. Namna Mwanamke atakuwa kielelezo Muhimu cha Maadili katika Jamii.
Lakini ukiangalia Maudhui ya Vipindi hivi ni kama yanakwenda kinyume na hayo yote niliyoyaorodhesha.
MAUDHUI YENYEWE
Ni maudhui Yenye kulenga kuongeza Mifarakano kati ya wanaume na wanawake (jambo la kusikitisha kabisa).
Maudhui yenye Kuonesha Namna gani Mwanaume Ni Adui wa maendeleo ya Mwanamke. Namna gani Mwanamke atatoka katika Utii wa Mwanaume na kuwa Huru kufanya mambo yake (Jambo linalokwenda kinyume na Misingi ya Familia Imara).
Katika moja ya maudhui hayo katika Televisheni moja maarufu Inaonesha Binti wa Shule Akilaumu Majukumu ya kuosha Vyombo kuachiwa Wao(Mabinti) na Kaka Zao Wakiachwa katika hayo majukumu.
Sijui kama yule binti aliandaliwa kusema vile lakini Jee Jamii za Zamani zilikuwa na Kosa lipi kugawa Majukumu Furani furani katika jamii kwa kuzingatia Maumbile na uwezo baina ya watendaji?
Je, ni sahihi Mwanaume mwenye misuli mingi na ukakamavu wa mwili aoshe vyombo na kukata vitunguu. Kisha Mwanamke Mwenye Udhaifu kulinganisha na mwanaume eti aende kubeba zege au Kubeba mizigo.
KWA NINI HATUONI HEKMA ZA WAZEE WETU KATIKA HILI KABLA YA KUWALAUMU?
JE, KUNA MATOKEO YOYOTE CHANYA KATIKA HARAKATI HIZI?
Hakika jamii makini lazima ijuulize Na itafakari kule tulikotoka hapa tulipo na kule tunakoenda.
Je, Jamii Inaenda kuwa imara zaidi? jee Familia zinaenda kuwa Bora mara dufu kuliko wakati wowote ule?
Je, ni kweli Familia baada ya miaka 20 ya harakati hizi za Ki feminism zitakuwa bora kuliko Familia za miaka ya 1900s Jee tunaenda kuipata jamii iliyo na maelewano kuliko wakati wowote ule?
Kama jibu ni laa (Hapana) Je, hizi Harakati za nini kuendelea kuzishabikia?
Kwanini Hatuzinduki Kuwa maendeleo ya harakati hizi yanaenda sambamba na kuporomoka kwa maadili katika jamii yetu.
Kwanini hatuoni maendeleo ya harakati hizi yanaenda sambamba na Kuzolota kwa Familia na kukosa uimara na Maelewano, na Maadili katika jamii?
Kwani bado hatujastuka kuongezeka kwa matukio ulawiti na ubakaji kwa watoto wadogo? Kwani bado hatuoni wimbi la dadapoa linavyokuwa kwa kasi?
Je, tumeamua kukumbatia Tatizo kwa sababu tunataka tuone Mwisho wake?
Je, tutaweza kubadili hali tukishauona huo mwisho?
Je, Vizazi vijavyo vitatuona sisi ni watu wa aina gani kukubali hili litokee kwetu?
Mbaya zaidi katika hili wanaoumia zaidi ni Wanawake Wenyewe japo wanaaminishwa kuwa 'Nothing is wrong' kwa ule uhuru wa kufanya starehe na Anasa.
Nashauri Maudhui ya Vipindi vya Wanawake vinavyogusa familia na Jamii viwe na lengo la kujenga jamii na sio kuibomoa katika namna ya ushabiki na Vita baridi.
KATIKA HII VITA BARIDI INAYOENDELEA HAKUNA ANAYEENDA KUSHINDA AU KUSHINDWA NI WOTE AIDHA TUSHINDE AU TUSHINDWE KWA SABABU WOTE TUNATEGEMEANA.