Kwahiyo Kigwangala ambae alianzisha mjadala wa Bilion 20 ni Yanga, au?!Kinachonishangaza wanaotaka BIL 20 sana na kupiga kelele kwenye Mitandao Ni Yanga. Simba kwa asilimia 90 hatuna tatizo mi nashauri hata asizitoe... Abaki nazo kwani shida ipo wapi? Wachezaji wanalipwa kwa wakati, team imetulia haina shida. Hivi sasa on the way to nigeria. Yanga mbona mnateseka 😁😁😁😁😁
Unajua sijui ushabiki maandazi au uelewa mdogo!!! Yaani seriously unasema hata asipotoa kwani shida ipo wapi wakati Wachezaji wanalipwa na gharama zote zinafanyika?! Hivi mnaangalia mbele ya safari nyinyi?! Hivi Yanga si walikuwa hivi hivi mbele ya Manji? What happened next?!
BInafsi ingawaje mimi sio Simba lakini nashabikia suala la Mo Dewji na Bilion 20 kwa sababu kwangu naiona ni kama RED ALERT kwa GSM na Wenzake pindi watakapotaka kuichukua Yanga! Wala siwezi kujitia upofu na kusema "kwani tatizo lipo wapi wakati GSM wanasajiri na kulipa wachezaji" kwa sababu nilishaona madhara ya huu ujanja ujanja wakati tupo na Manji!
Na binafsi, nilikuwa mmoja wa watu ambao nilishukuru sana Manji kuondoka Yanga kwa sababu siwezi kufurahia maendeleo yasiyo endelevu ambayo ndiyo hasa yamekuwa chanzo cha soka letu la hovyo hovyo ambalo mipango yake ALWAYS ni ya short-run!!