Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Ni dhahiri shairi awa wenzetu watani zetu usiku wa kuamkia leo nafikiri awajapata usingizi kutokana na matukio yaliyojiri jana, Ni maumivu makali wameyapata na awatoyasahau kabisa.
Maumivu yao ya kwanza ni kutoa sare na singida big star pale liti, wanajua kabisa kumuondoa yanga pale juu kileleni ni sawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano na ahueni yao ni kushinda mechi zao lakini gape la point linazidi kuongezeka na wanajua yanga akirudi ni mwendo wa dozi iyo sare imewavuruga.
Maumivu ya pili walikuwa wanajipa matumaini na timu yao ya wanawake kufanya vizuri dhidi ya mamelodi lakini na wao jana iyo iyo wakabatizwa kwa moto kelele zikaishia hapo.
Maumivu ya tatu ambayo ndo yamekuwa makali zaidi kwao mithili ya kisu kwenye kidonda ni yanga kucheza mpira mkubwa mbele ya waarabu ugenini na kufanikiwa kuwapakata kule kule kwao kwa ushindi wa dhahabu imewafanya wakose hata hamu ya kula, Walikuwa wamebaki na tegemeo la yanga kutolewa na waarabu ili wapate kichaka cha kujiliwaza lakini kikafyekwa kibabe.
Walikuwa wanavizia Kocha Nabi ashindwe kufuzu walijua kabisa atatimuliwa wamdake ndo maana walikuwa wanasikilizia hii mechi itaishaje ili waajili kocha na sasa baada ya mechi kuisha na yanga kufuzu utaona harakati zao za kuajiri kocha zitaanza kwa nguvu maana waliyekuwa wanamvizia kafaulu mtihani na ajira yake iko salama kwa sasa.
Poleni sana mitaa ya msimbazi akiba ya maneno unatakiwa kuwa nayo kama kweli unaufahamu mpira na natangaza rasmi ya kwamba nchi iko kwenye mikono salama na imetulia, YANGA.