Maumivu katikati ya mgongo, mabega, chini ya shingo na kusambaa kwenye maungio ya mikono.

Maumivu katikati ya mgongo, mabega, chini ya shingo na kusambaa kwenye maungio ya mikono.

MAPUMA MIYOGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2013
Posts
3,792
Reaction score
2,365
Wana JF Doctor,

Nimekuwa na maumivu ya mgongo kwa muda mrefu na nimetumia dawa za maumivu bila mafanikio kwani hali hurejea kama awali baada tu ya kumaliza dawa.

maumivu ya mgongo katikati na mabegani hadi chini ya shingo ambayo husambaa sehemu kubwa ya juu ya mgongo kupelekea maumivu makali hasa nikiwa nimekaa sana. Mgongo huchemka na kuhisi uchovu usio kawaida na kunifanya nitamani kujilaza kwenye kitu kigumu na mtu anikanyage kanyage mgongoni. maumivu haya huyasikia hata kwenye mikono (joints) japo huku huwa sio sana na huja mara moja na kutoka.

Nikiwa natembea au nafanya muscular work huwa almost hakuna maumivu ila nikaa ndio huja, hii imenifanya mara nyingi niwe wa kujilaza na kutokaa muda mrefu ni-concentrate kwenye kazi ofisini. nimefanya hata Physiotherapy lakini nilipata nafuu kidogo tu japo Dr. alisema nakaa vibaya kwenye kiti ofisini, lakini sasa mbona siponi????

ushauri tafadhari na tiba kama inawezekana. Real Doctors wani-email kwenye mapumamiyoga@gmail.com na nitafanya mpango kuwaona kwenye vituo vyao.
 
pole ntakuandikia email. lkn sijajua kama wewe mwanamke au? cha kujua ni kwamba maumivu ya mgongo hayaponi haraka sababu yanauzisha mishipa mikubwa ya fahamu inayotoka kwenye uti wa mgongo.. jitahi kufanya mazoezi mepesi na tafuta multivitamin kwa sasa. ntakuemail dawa nkipata muda
 
Back
Top Bottom