MAUMIVU: Naumia sana wanavyomkosea heshima Mbowe

Master Legendary

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
576
Reaction score
876
Niongee ukweli kutoka Moyoni naadmire sana Siasa za Mbowe na namheshimu kama Jabali la Siasa za Tanzania, Huyu mzee kafanya kazi kubwa sana anastahili heshima yake pamoja na mapungufu yote ya kibinadamu.

Nafuatilia Uchaguzi wa CHADEMA naona kama CHADEMA aliyoijenga kwa jasho na damu leo inageuka Meza ya kumvunjia heshima,kumdhalilisha,kumtweza na kumtesa sana huyu kiumbe wa Dhahabu na sijui anapata maumivu kiasi gani.

Nafahamu ni Uchaguzi ila kiukweli watu wa Mitandaoni na tunamkosea sana heshima huyu mtu mpaka naumia mimi hasa nikisikiliza Interviews zake anavyojaribu kufafanua tuhuma anazopewa na ukweli wa mambo ulivyo.

Nimpongeze Heche kwa kutumia hekima kubwa sana katika Kampeni zake kwa kuhakikisha anailinda pia thamani na Brand ya Mbowe isipotee katika ramani ya nchi hii,binafsi namuona kama Heche ni Kiongozi na sitashangaa akishinda Umakamu Mwenyekiti.

Mbowe keshatangaza hiki ni kipindi chake cha Mwisho na nimemsikiliza AZAM leo anasema atapendekeza amalizie kipindi chake kwa Miaka 3 ili apishanishe Uchaguzi wa Chama na Serikali kwa Maslahi ya Chama, nawaomba wanaCHADEMA kwa Utumishi aliowapa Mbowe unganeni wote wenye akili kuitetea Dhahabu yenu isidhalilishwe dakika za Mwisho.Hakuna kosa alilofanya kugombea Katiba ya Chama chake inamruhusu kabisa.

Longlive bro we Love you na tunashukuru kwa Utumishi wako katika kujenga Upinzani wa Tanzania.
 
---Mbowe akae pembeni katika uenyekiti, lakini, naomba mnielewe, mbowe asikae mbali sana na chadema, still awe baba wa karibu wa chadema na ubunge agombee, Amini nisemacho hawa wanataka uongozi ipo siku na saa wataibwaga chadema nikimaanisha itawaelemea, Note this - - -
CC, Yericko Nyerere
CC, FreemanMbowe
 
Mijinga jinga ya ccm bhana wewe leo umekuwa wa kuionea huruma chadema
 
Huijui siasa wewe!

Kusikia tu hatagombea tena na umeamini?

Lisu alisema hatagombea nafasi atakayogombea Mbowe kiko wapi?

Aache kutiatia huruma,acha apelekewe moto watu tayari wana plan B.
 
Kwenye maburungutu ya mama abduli wange mtafuta huyu/ consultant.

Professor Nic Cheeseman​

Wa University of Birmingham.

Anakitabu chake na kina mbinu nyingi Sana ""how to rig an election without getting caught"
 
Mbowe kayataka mwenyewe na yeye ndo kafikisha hapa haya mambo kwaiyo ajilumu mwenyewe


Huwezi kuwafanyia Figisu Icon wa chama kwa kujifanya wewe ndo mpanga safu ya uongozi, na kujifanya Mungu mtu wa Chama,hutaki kupingwa

Nadhani hakufikiria kabisa kua Lissu au Meingine yoyote anaweza ku hukua Fomu na kum-chalange kwa upinzani mkubwa


Kwanini kila mtu anaeondoka ndani ya Chama anamlalamikia Yeye?
 
Sana sana mbowe atakua Mpinzani ndani ya Chadema atawavuruga ili ionekane wameshindwa
 
Dawa za kuzuia au kupunguza maumivu mbona zipo tele kwenye maduka ya madawa baridi?
 
Kama machawa wake ni hawa akina Wenje, Yeriko, Ntobi na Bon Yai acha tu Mbowe awe Chacha Wangwelized!

Kayataka mwenyewe! 🚮

Your browser is not able to display this video.


 
Mbowe alitakiwa kusoma alama za nyakati mapema.
Machawa na wapambe wake ndio waliomfikisha hapa alipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…