Maumivu sehemu ya kisogo na kichwa kuuma

Maumivu sehemu ya kisogo na kichwa kuuma

return of cs

Senior Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
130
Reaction score
23
Heshima yenu nawapa, naimani mko salama nmejitokeza kwenu nikiwa na tatizo ambalo mwanzo nliona ni kawaida tu ila sasa limenizidia, nimekuwa nikiumwa sehemu nzima ya kisogo pale ninapoegemea ukuta, kiti cha mbao hata sponji, hata naposafiri siwezi kuegemea kabisa kwa kuhofia maumivu hayo, pia napolala siwezi lalia kisogo pia.

Na usiku wa kuamkia leo imetokea nimelalia kisogo na nilisikia maumivu sana usiku na kuona kizunguzungu sana huku moyo ukienda mbio na kichwa kikiuma sana.

Mpaka sasa najisikia hvyo kichwa kuuma pamoja na mishipa yote ya kichwa kunicheza hata kuegama kwenye sofa nashindwa kutokana na maumivu!

Jamani hili tatizo lina tiba? Na chanzo huwa nini? Na ni ugonjwa gani huu? Nasumbuliwa hivi mwaka sasa. Naombeni ushauri na maelekezo yenu madokta waJF.

Amani iwe pamoja nanyi.
 
pole mkuu kuna wakati matatizo ka hayo huwa yanasababishwa na kukandamizwa kwa nerve kitaalam inaitwa Occipital nerve hasa Greater Occipital nerve na kusababisha hayo maumiv ambayo tunaita Occipital Neuralgia. wakati mwingine maumiv ka hayo shida hua wa zaid kwenye mfumo wa fahamu unaopita kwenye shingo na tunaita Cervicogenic Headache. ka upo dar nenda Muhimbili umuulizie Prof Matuja klinik yake ilipo akuone yeye amespecialize kwenye hizo stuff
 
Nashukuru mkuu ila mimi nipo mwanza nitajaribu kuilizia pale bugando
 
pia unapolala usiwe unaweka simu karibu. simu iwe mbali na kichwa au kitanda kabisa..
 
Back
Top Bottom