Maumivu upande wa kushoto mwa kifua, tatIzo nini?

Maumivu upande wa kushoto mwa kifua, tatIzo nini?

Unauma ukiwa unavuta pumzi kubwa au unaumaje. Pole sana.

Kama upo ndani jaribu kutoka nje upate hewa ya nje kwa dakika kadhaa. Na ukilala jaribu kulalia ubavu wa kulia usilalie kushoto.

Pole sana ndugu yangu.
Hapa nimekaa tu kitandani nashidwa kulala
 
Nenda nje au kama sivyo basi jaribu kuipata hewa ya nje japo kwa dirishani mkuu ila kwa nje itakuwa vyema zaidi.

Nasema hivyo coz nami nna tatizo la moyo huwa unauma muda fulani, huuma zaidi nikivuta pumzi kubwa ile. Nikitoka nje sehemu ya hewa nakaa kwa utulivu kwa muda hutulia tu wenyewe sasa sjui tatizo ni nini.

Kwa kiasi flani mi nasumbuliwa na JINNS sasa sjui huwa wananikamata hivyo hata sielewi mkuu jaribu kufanya hivyo kiongozi.

Pole sana aisee.
 
Habari ndugu nimekuwa natatizo la kusumbuliwa upande wa kushoto yani kamamoyo unavuta vile mwezi sasa tatizo nini??
Pole, hayo maumivu upande huo yana dalili zote za kuwa na uhusiano na matatizo ya moyo. Nenda hospitali haraka upime au uende kwenye vipimo vya tiba mbadala usaidiwe.
 
Halafu epuka sana kujitishatisha, hapo umekaa kitandani lakini image yako iko kama unamuona malaika wa ile kazi ngumu, usijitishe kaka vumilia jipe ujasiri, chukulia kama ni maumivu ya mguu tu, usie serious kufikiria saaana, patakucha salama inshallah utaenda hospitali.
 
Moyo upo upande kushoto zaidi wa mwili wa binadamu sasa unapolala usiuweke mkono chini ya huo ubavu wa kushoto na kuulalia, ukifanya hivyo unakandamiza mishipa ya damu hivyo unafanya damu itake kupita kilazima hivyo damu inatumia nguvu kubwa na pia unachelewa kufika.

Sasa maumivu yake hapo utatamani kusimulia, amka kunywa Maji ya moto halafu tulia kidogo kama dakika kumi then ukirudi kulala usilale kama mwanzo, lala mtindo mwingine. Usiku mwema mkuu kila la kheri.
 
Moyo upo upande kushoto zaidi wa mwili wa binadamu sasa unapolala usiuweke mkono chini ya huo ubavu wa kushoto na kuulalia ukifanya hivyo unakandamiza mishipa ya damu hivyo unafanya damu itake kupita kilazima hivyo damu inatumia nguvu kubwa na pia unachelewa kufika sasa maumivu yake hapo utatamani kusimulia amka kunywa Maji ya moto alafu tulia kidogo kama dk kumi then ukirudi kulala usilale kama mwanzo lala mtindo mwingine.usiku mwema mkuu kila la kheri
Asante ngoja nichemshe maji
 
Back
Top Bottom