Maumivu ya kichwa yananimaliza msaada please

Usiniogope na wala usiogope bei kwani uzima wako na pesa bora kitu gani? Uzima wako unaweza kuupata Hospitalini? Au kuna Mtu anaweza kukupatia uzima wako? Uzima ni kitu bora kuliko pesa, kwani pesa inatafutwa uzima wako utaweza kuupata wapi?

Jali afya yako kuliko.Nitafute kwa address niliyo kupa tupate kuzungumza zaidi na ikiwezekana niweze pia kukupa ushauri mzuri Mkuuu Usiniogope Ukiniogopa haya kaa na maradhi yako.
Habari mtaalam..

Mimi pia nna tatizo la kuumwa kichwa hususan nikitembelea sehemu zenye kelele nyingi au nikijihangaisha sana.

Kichwa changu mara nyingi huuma sehemu ya kipanda uso na katikati ya utosi ikiambatana na homa ya baridi na viungo kuishiwa na nguvu.

Hivi juzi kati nlitembelew daresalam nikaanza kuumwa hivyo mara ya kwanza nliumwa nikapona nikaenda tena DSM nikaumwa tena.

Hadi hapa nlipo naumwa hata sijui solution yake ni nini?

Pia nna tatizo la kuwa na kizunguzungu in such sometimes najihisi kama vile nataka kuanguka.
Na hata nikipita karibu na maspika yanayopiga mziki au nikiswali kuangalia chini au nikisimama mda mrefu kuongea na mtu huwa najihisi kama nataka kuanguka ijapokuwa sijawahi kuanguka umri wangu ni miaka 30
Naomba dr. Nisaidie japo kwa ushauri🙏
 
Habari!

1: Unahitaji kusikilizwa na kufanyiwa tathmini nzuri kwa tatizo lako. Hii tunasema ni kuhitaji kuunganisha dots za mwenendo wa maumivu husika.

2: Kwa maelezo ya awali hii inatoa uelekeo wa migraine, kwa mazingira haya huwa kuna dawa za kutibu na kuzuia kulingana na tatizo.

3: Kulingana na dalili zako unaweza kuhitaji kufanya kipimo pia kuondoa wasiwasi wa matatizo mengine ya kichwa ambayo ni hatarishi.

4: Kama ni migraine, zaidi ya dawa kuna haja ya kuwa na mabadiliko ya kimaisha kwa ujumla ili kupunguza baadhi ya vitu vinavyoanzisha attack/kuanzisha maumivu kama:

A: Mwanga mkali

B: Harufu kali/ pafyumu

C: Matumizi ya pombe

D: Stress

E: Matumizi ya maziwa/mtindi, kahawa na chocolates.

D: Vyakula vya kusindikwa/makopo na soda

F: Usikae na njaa muda mrefu/kuahirisha mlo.

G: Kutokuvuruga ratiba yako ya usingizi na uwe wa kutosha (saa 8).

H: Kwa akina mama, asitumie mfumo wa homoni wa uzazi wa mpango.

I: Usiwe mtu wa kukasirika mara kwa mara.

J: Kutokujichosha sana/kupita kiasi.

K: Kunywa maji ya kutosha, kulingana na eneo ulilopo, uzito wa mwili na aina ya kazi.

L: Kuna mambo yasiyoweza Kubadilishwa kama: kubadili hali ya hewa/ kutoka mkoa mmoja mpaka mwingine nk.

NB: Mtaalamu maalumu anaeweza kulifanyia kazi hili ni Neurophysician/daktari bingwa wa mishipa ya fahamu.
 
Sawa mkuu itabidi nikafanye vipimo hili tatizo ninalo mda mrefu sana.
 
Back
Top Bottom