Maumivu ya kitovu kwa mtoto wa kike

Maumivu ya kitovu kwa mtoto wa kike

Obel

Member
Joined
Jun 11, 2023
Posts
56
Reaction score
72
Hello Doctors na wanajamii forum wote kwa jumla. Nna mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 6 kasoro anasumbuliwa na maumivu ya kitovu kwa muda wa mwaka mmoja sasa! Nimeshakwenda hosp mara kwa mara tatizo halionekani!

Kwa mara nyingine nmeenda tena kuoanana na specialist wa watoto..akafanyiwa vipimo vya damu, haha kubwa, ndogo pamoja na ultra sound lkn hajaonekana na shida yyte japo dr.aliniambia kuwa kuna ka uwazi kwenye kitovu chake kwa juu na sio kwa ndani! Hakuwa na uhakika kwamba uwazi huo ndio chanzo cha maumivu hayo!

Alituandikia antibiotics (metro) pamoja na omeprazo! Amemaliza dozi still bado analalamika tumbo linauma(eneo la kitovu).
Nahitaji kurudi tena hosp lkn naombeni mawazo na ushauri wenu pia ni muhimu! Je huenda ikawa ni tatizo gani hili?
 
Madokta mje kutoa msaada huku,
Mzazi usijali tatizo la mtoto wako litapata ufumbuzi, hakuna shida isiyo na jibu
 
Kamcheck ultra sound labda ana hernia ya kitovu.
Alifanyiwa ultrasound Dr.akaniambia ana kauwazi kwenye kitovu ila haipo kwa ndani ni kwa nje kwenye ngozi,! Nikamuuliza je inawezakana ikawa ndio chanzo cha maumivu hayo? Hakutoa jibu la moja kwa moja..alisema huenda ikawa hivyo! It means haina uhakika! Ndio akampa hizo dawa!
Tunaweza kaa hata wiki au wiki mbili simsikii kulalamika..na yanakuja km sekunde kadhaa hivi af yanapotea
 
Pole ndgu nikushauri utumie kuwa unampakaa mafuta ya nyonyo hapo kwenye kitovu na tumbo kwa ujumla mpkae asubuhi akiamka na usiku akitaka kulala fanya hilo zoezi ndani ya wiki 3 hadi 4 utaona matokeo
 
Pole ndgu nikushauri utumie kuwa unampakaa mafuta ya nyonyo hapo kwenye kitovu na tumbo kwa ujumla mpkae asubuhi akiamka na usiku akitaka kulala fanya hilo zoezi ndani ya wiki 3 hadi 4 utaona matokeo
Asante sana! Naenda kuyatafuta leoleo
 
Pole sana dada kwa changamoto unayopitia
Nitoe mchango wangu kidogo;
Maumivu kwenye kitovu cha mtoto huweza kusababishwa na vitu vingi
1. Mtoto asipo pata choo mara kwa mara (constipation)
2. Mtoto akiwa anapewa moja ya chakula ambacho ana allergy nacho (Food intolerance)
3. Mtoto akipata Kidole tumbo (appendicitis) na madactari wengi husahau kucheki hii
4. Mtoto akiwa na uvimbe kwa ndani karibu na kitovu (Umbilical hernia)
5. Mtoto akishindwa kutoa gas (baada ya kula vitu vyenye gas) nk

Ni vizuri pia kujua kama mtoto anapata dalili nyingine yoyote tofauti na hayo maumivu ya kitovu?
1. Mfano: kuhisi maumivu yana hamia upande mmoja wakati mwingine na baadae kurudi katikati (Appendicitis)
2. Kupunguza ham ya kula na pengine kuchoka choka?
3. Mtoto wako akila vitu kama maharage (anatoa gas?)
4. Angalia pia choo chake (asubuhi) kama kina trace zozote za damu

Hayo maelezo ukiyafuatilia vizuri ukamuelezea dactari naamini ataweza kumtibu bila shida
 
Ahsante kwa ushauri! Huwa hapendi maharage anasema akila maharage tumbo humuuma! Lkn me naona hata asipokula tumbo humuuma.
Kingine sio mlaji kabisaa hamu ya Kula inapungua wakati mwengine anakaa sawa!
Namtengenezea chakula tofauti tofauti mara kwa mara!
Aliwahi kufanyiwa ultrasound sasa cjajua je alichekiwa Mambo yote hayo ama laa! Na nilipokuwa chumba cha ultrasound nilijaribu pia kumueleza Yule Kaka vile mwanangu anaumwa ili na yy atazame vizuri na kwa umakini! Nilimwambia arudierudie ili tupate uhakika zaidi! Yaan niligeuka Dr. Kumbe maskin cjui chochote!
Dr. Alitoa majibu akasema Hana shida yyte Ile japo ana kauwazi kenyewe pia hakako kwa ndani japo nje ya kitovu! Hivi huo uwazi kwa nje unaweza ukasababisha hayo maumivu anayoyasikia?
 
Back
Top Bottom