Maumivu ya kuachana na mwanamke

Maumivu ya kuachana na mwanamke

fimboyaukwaju

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2020
Posts
2,977
Reaction score
3,798
Kabla sijaoa niliachana na wanawake kadhaa,ambao tulipendana sana nao,na niliumia sana moyoni.Wa kwanza ni Tana,ama nilimpenda sana lakini wakati huo kipato changu hakikuwa kikubwa,akachukuliwa na mkaka mmoja na akamtafutia kazi ya kujishikiza,aisee moyo uliniuma sana lakini ndio hivyo,hatahivyo huyo naye aliachwa baada ya boss mmoja kumuoa na kwa sasa huyo dada ni mjane.Wa pili ni Zaeli,mdada mzuri na mrembo haswa,huyu tulipendana sana na kila mtu kwao na kwetu alijua,na niliwaomba wazazi wangu nimuoe wakanikatalia,huyo mdada akapotea zake,hivi sasa ni singo maza anapambana na maisha.Wa tatu ni nati,huyu tulipendana sana wakati tukiwa sekondari,kitu kilichonishangaza akachukuliwa na rafiki yangu ambae tulikuwa tunasoma nae,urafiki ukavunjika na mrembo nikamkosa,roho ikauma sana,huyo nae hivi sasa ni singo maza na tunaongea mara kwa mara.Wanawake wote hao wamezeeka lakini tunawasiliana kwa salamu na kushirikiana kwenye matatizo ya vifo au magonjwa.Hatuna uadui tena.Vipi mwenzangu unayesoma uzi huu,uliwahi kuachwa na ukaumia sana?
 
Back
Top Bottom