Maumivu ya mgongo sugu wa juu, mabegani na misuli shingo kukaza homa ya uti wa mgongo (Pneumonical Meningitis)

Maumivu ya mgongo sugu wa juu, mabegani na misuli shingo kukaza homa ya uti wa mgongo (Pneumonical Meningitis)

MAUMIVU YA MGONGO SUGU WA JUU, MABEGANI NA MISULI SHINGO KUKAZA

HOMA YA UTI WA MGONGO ( PNEUMONICAL MENINGITIS)


View attachment 2184538
Ndugu zangu wana jamii forum kwanza nikili kwamba huu ugonjwa ninao na ni hatari sana kimaisha kiujumla na unakatisha tamaa sana kiasi kwamba mpaka inafika hatua unaweza kuchukua maumuzi magumu

DHUMUNI LA KUANDIKA UZI HUU NI KUSHEA NA WATANZANIA WENZANGU ILI WAUELEWE HUU UGONJWA

SASA HOMA YA UTI WA MGONGO NI NINI?

(pneumonical meningites)
Huu ni ugonjwa unaoshambulia utando unaofunika ubongo (brain) na Uti wa mgongo (spinal cord)

VISABABISHI VYA HUU UGONJWA
1.Bacteria
2.fungus
3. virus

NI NINI DALILI ZAKE?

DALILI AMBAZO NAZIPITIA MPAKA SASA


1.katikati ya kifua upande wa nyuma mgongoni kati ya scapula mbili za mabega Panauma sana kama pana moto mpaka leo

2.nikitaka kusoma kitu au kuandika kitu kwa mfano kama hii thread ndo naongeza maumivu zaidi

3.wakati huu ugonjwa unanianza tarehe 28/08/2016 nipo shule advance Form five misuli ya shingo , mabega , kifuani na mikononi ilikuwa inakakamaa sana na kuuma ila Hadi leo tarehe 11/04/2022 misuli ya mabega ndo inakaza sana misuli ya shingo na kifua ishaachia

4.majasho makwapani yalikuwa yananitoka sana ila saiz yamepungua

5.mwili kukosa nguvu

6. Mikono ilikuwa inakufa ganzi saizi inatokea mara mojamoja

7. Kipindi ndo naanza kuumwa nilikuwa sitaki mwanga kabisa hata simu ilikuwa shida kutumia ila macho yalikuwa yanaona vizuri tu saiz mwanga haunisumbui

8. Kukosa hamu ya kula

9.nikitaka kufikiri kwa kina ndo maumivu yanazidi
10. Nilikuwa nacheza mpira kwa sasa siwezi kucheza kutokana na huu ugonjwa ushaniharibu

HISTORIA YA MATIBABU YANGU

HOSPITALI NILIZOTEMBEA


1.kigonsera dispensary -Ruvuma
2.peramiho hospital - ruvuma
3.vwawa district hospital - Songwe
4.Ifisi hosipital -Mbeya
5.mbeya rufaa hospital-Mbeya
6.Muhimbili hospital -Dar es salaam
7.Moi hospital- Dar es salaam
8. Kairuki hospotal- dar es salaam
9. Vituo vya watu binafsi
10.Kanisani kwenye maombezi
11. Kwa waganga wa kienyeji

VIPIMO NILIVYOFANYA
1.Blood
2.makohozi
3.x ray za kutosha Hadi nahofia kansa
4.CT Scan - Mhimbili
5.MRI - MOI

NINI KILIONEKANA KWENYE HIVYO VIPIMO?

Cha ajabu hivyo vipimo havikuonyesha kitu chochote ndugu zanguni

JE HII HOMA YA UTI WA MGONGO WANAFANYA KIPIMO GANI?

Kipimo kinachofanywa kinaitwa lumbar puncture wanakuchoma sindando kwenye Uti wa mgongo na kuvuta majimaji ya kwenye uti wa mgongo kwa vipimo ili wajue kinachosababisha ni bacteria, fungus au virus

MATIBABU YAKE NI NINI?

Dawa za kutibu zinategemeana na vimelia walioshambulia uti wa mgongo watakaopatikana

WATU AMBAO WAPO HATARINI NA HUU UGONJWA

1. Wanafunzi
2. Watu wanaofanya kazi za kutumia akili sana

IKUMBUKWE

Hapa tanzania huu ugonjwa madakitari hawana ufahamu nao sana ukienda watakwambia upigwe x ray kumbuka elimu yetu tunasoma kwa kukalili

PIA

Nikubali kwamba madakitari huwa tunawaeleza tunasumbuliwa na mgongo kwa juu mabegani lakini kati ya madakitari wote niliokutana Nao baada ya kutokuona kitu huwa wanaishia hapo na hawapendekezi kipimo kingine . huu ugonjwa unatusumbua wale tunaoumwa mgongo sugu wa juu, mabegani, shingoni

Ukitaka kuuliza Kwa experience zaidi ya huu ugonjwa unaweza kunitafuta 0758954522

Ila mimi sio dakitari wala mganga ifahamike ivo nimeandika kwa faida ya wana jamii forum
View attachment 2184539
UKIFANIKIWA KUPITIA HUU UZI NJOO UTOE MREJESHO ILI KUSAIDIA KIZAZI KIJACHO NI UGONJWA HATARI KULIKO UKIMWI MAANA HUU NI MAUMIVU SIKU,MIEZI MIAKA NENDA RUDI😭😭😭😭


Nimechoka sana maisha yangu sijui nayaendesha vipi bado nina umri mdogo sana da! Miaka 24 ila naamini siku moja mungu atafanya maajabu

View attachment 2184536
pole aiseee. kwahiyo kwa sasa unaendeleaje? pole sana
 
Vipi mkuu mbn kama hzo dalili na mm ninazo sema yangu imeongezeka na maumivu makali yasiyoisha hii hali ilinianza nikiwa shuleni advance 2022 mpka Leo vp ww bdo hali ni hyohyo??
 
Vipi mkuu mbn kama hzo dalili na mm ninazo sema yangu imeongezeka na maumivu makali yasiyoisha hii hali ilinianza nikiwa shuleni advance 2022 mpka Leo vp ww bdo hali ni hyohyo??
Kuna afadhali ndugu yangu naomba mawasiliano yako tupeane experience kidogo
 
Bado ndugu yangu bila shaka wewe ni sickmate mwezangu naonaga thread zako unavyosumbuliwa ,,,mungu atusaidie tu
Mkuu vip unaendeleaje na ugonjwa umepona...nami tangu majuzi naona mgongo unaniuma sana upande wakushoto nyuma na katikati nikiinama pia naumamiaa sjui ni kitu gani
 
Back
Top Bottom