Maumivu ya tumbo la MP.

Linamo

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2011
Posts
9,976
Reaction score
24,496
Habari zenu wana JF?? Napata maumivu makali sana chini ya kitovu wakati wa MP ambayo yanapelekea kuninyima usingizi.Msaada kwa anayejua tiba yake.Nawasilisha.
 
Tumia maji ya moto, kuna chupa kwa ajili ya kuifadhi maji ya moto kwa nje ni mpira kwa hiyo ukiweka kwenye tumbo maumivu hupungua na kuacha kabisa kama huna chupa unaweza tumia chupa za maji kama ni uhai au kilimanjaro unaweka maji alf unaviringisha na taulo au kanga basi utapa hali ya umoto moto na utalala vizuri sana. Kwa mimi ndio njia nzuri nayotumia jaribu na wewe
 
Ahsante kwa msaada wako...nitajaribu nione nikifanikiwa nitakuambia.
 
Meza Meftal Spas......mara tatu kwa siku itakusaidia.......zaidi ya hapo kama hujapata mtoto.......jitahidi kufanya hivyo.......
 
Meza Meftal Spas......mara tatu kwa siku itakusaidia.......zaidi ya hapo kama hujapata mtoto.......jitahidi kufanya hivyo.......
hili halina dawa bwana ni kujikaza tu...kwani siku ngapi?
 
Meza Meftal Spas......mara
tatu kwa siku itakusaidia.......zaidi ya hapo kama hujapata
mtoto.......jitahidi kufanya hivyo.......
Hizi dawa nishatumia mwanzo zilikuwa zinanisaidia ila siku zinavyozidi kwenda nikimeza hazinisaidii tena maumivu yako palepale...labda hilo la mtoto...nami natamani ila hivyo MUNGU bado hajanijalia.
 
hili halina dawa bwana ni kujikaza tu...kwani siku ngapi?
Duh!! kweli siyo siku nyingi ni chache tu ila hayo maumivu yake siyo madogo kama unavyofikiria wewe...maumivu ni makali sana...halafu tunatofautiana huenda yako huwa kidogo ndiyo maana unavumilia.
 
Duh!! kweli siyo siku nyingi ni chache tu ila hayo maumivu yake siyo madogo kama unavyofikiria wewe...maumivu ni makali sana...halafu tunatofautiana huenda yako huwa kidogo ndiyo maana unavumilia.
dawa huwa hazisaidii ukishakuwa sugu hazitibu tena nenda kwa dokta akucheki vizuri mirija kizazi nk
 
Chemsha mchaichai unywe mara 3 kwa siku 5,tatizo litaisha ikishindikana ni PM nitakupa namba ya mama mmoja mwalimu atakupa dawa.
 
Chemsha mchaichai unywe mara 3 kwa siku 5,tatizo litaisha ikishindikana ni PM nitakupa namba ya mama mmoja mwalimu atakupa dawa.

weka tu namba hapa.....wahanga ni wengi wa hili janga..........
 
hili halina dawa bwana ni kujikaza tu...kwani siku ngapi?

hii isikie kwa jirani.....kuna watu wanaumwa Smile......nilishaona mtu anaingia uvunguni mwa kitanda hivi hivi bila sababu..........
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…