Mauzo ya Anglo America kwa BHP msimamo wa serikali ni upi

Mauzo ya Anglo America kwa BHP msimamo wa serikali ni upi

Nchi zenye uwekezaji wa AngloAmerica amelistukia hili dili lakini kwetu naona kimya
Ulivyokazania sasa, daah

Fanya research mzee, Anglogold Ashanti (mmiliki wa GGM) hana ties zzt na Anglo America kwa sasa.

Unless kama wana mgodi mwingine hapa TZ, sio GGM
 
Yah GGM ni AngloGold Ashanti

Ila tahadhari ni muhimu tujifunze pia kesho utasikia hao BHP wanataka kununua GGM
ili tuwe na maamuzi kwa haraka

Sio tunavutana na fursa miaka zaidi kumi hutufikii maamuzi Kama bandari ya bagamoyo na Gas ya Mtwara na chuma leganga
tumezubaa tu hatuna maamuzi ya ndio au hapana
 
shida ikwapi hapo?, Anglo anamiliki migodi mingi Duniani na BHP ni superpower pia, Serikali inahusikaje hapo kama kila contract kati ya GOT na Anglo inaendelea kama ilivyokuwa kwa BHP?
 
Mkuu, sio suala la bidding tu, wakati wa marger ya accacia na new Barrick, Barrick waliwakataa minor shareholders na ndio ikabidi acccacia wajitoe dse na lse, akina yakhe ikabidi watupiwe share zao, tungekuwa makini akina yakhe wangeshirikishwa kwenye new barrick na sasa wangekuwa wanaupiga mwingi
 
Kwanza Anglo America hamiliki mgodi wa GGM (Geita Gold Mine)

GGM inamilikiwa na AngloGold Ashanti.

AngloGold Ashanti iliundwa baada ya merger ya Anglo Gold na Ashanti Goldfields (hii ndo alikua anamiliki Anglo America)

Lkn baada ya hio merger Anglo America akauza hisa zake zote alizonazo kwenye AngloGold Ashanti.

Kwa hio Tanzania hana cha kusema sababu haiwahusu unless Anglo America awe anamiliki mgodi mwingine hapa tz kitu ambacho sidhan.
Yeah
 
Yah GGM ni AngloGold Ashanti

Ila tahadhari ni muhimu tujifunze pia kesho utasikia hao BHP wanataka kununua GGM
ili tuwe na maamuzi kwa haraka

Sio tunavutana na fursa miaka zaidi kumi hutufikii maamuzi Kama bandari ya bagamoyo na Gas ya Mtwara na chuma leganga
tumezubaa tu hatuna maamuzi ya ndio au hapana[/QUOTE
 
Kwanza Anglo America hamiliki mgodi wa GGM (Geita Gold Mine)

GGM inamilikiwa na AngloGold Ashanti.

AngloGold Ashanti iliundwa baada ya merger ya Anglo Gold na Ashanti Goldfields (hii ndo alikua anamiliki Anglo America)

Lkn baada ya hio merger Anglo America akauza hisa zake zote alizonazo kwenye AngloGold Ashanti.

Kwa hio Tanzania hana cha kusema sababu haiwahusu unless Anglo America awe anamiliki mgodi mwingine hapa tz kitu ambacho sidhan.
Ok !
Hata mimi nilikuwa najua bado wanahodhi shared zao ,kumbe walishauza
Basi hii haitawagusa Anglo gold Ashanti hao wamiliki wa GGM hivyo zero effect Kwa mgodi
 
Hao BHP ni hatari na nusu , wako kila kona
Walianza na shughuli za uchimbaji wa dhahabu ila sasa hivi wanamiliki migodi ya chuma ,Nickel , copper nk
Wapo hadi kwenye petroleum industry
Kampuni ambayo imejitandaza na kumiliki migodi , visima vya mafuta na refineries kwenye nchi 90 si mchezo
 
Kuna mazungumzo yanaendelea kuhusu kampuni ya uchimbaji madini ya BHP kutaka kuinunua kampuni ya uchimbaji madini ya Anglo America. Kwa Tanzania Anglo America inamiliki mgodi wa Geita Gold Mine maarufu kama GGM. Nchi nyingi zenye uwekezaji wa Anglo America ikiwemo Botswana South Africa zimetoa msimamo wao juu ya uwekezaji huo wa BHP.

Nasie watanzania tungependa kujua faida na athari iwapo BHP watainunua Anglo America. Ikumbukwe sekta ya madini ina mchango mkubwa katika upatikanaji wa fedha za kigeni ajira na biashara za wazawa na maamuzi yeyote yatakayo yanayoweza athiri sekta yetu ya madini ni vyema tukayatizama kwa jicho pevu.
Sina hakika na kama mmiliki wa mgodi tajwa anauza au vinginevyo.

Ila msingi wa hoja na kuuzwa kwa mmiliki mpya.

Tanzania imewahi kuwa na kampeni ya simu inaitwa Celtel na serikali alikuwa mwanahisa. Ikauzwa kwa Zain na baadae ikauzwa kwa Airtel, serikali haikuweza kuzuia mauzo.

Tigo (MIC Tanzania) ilikuwa chini ya waingireza enzi hizo inaitwa Mobile, baadae ikauzwa kwa Tigo na sasa RA kainunua ikibaki na jina lake Tigo.

Mgodi wa North Mara ulianza kama East Africa Gold mines wamiliki wakiwa Australians kabla ya kuuzwa kwa Barrick ambae alikuwa na migodi chini ya ACACIA ambayo sasa iko chini ya kampuni ya Twiga Corporation na serikali ya Tz ikiwa mwanahisa.

Fuatilia Williamson Diamond (mwadui imeuzwa mara ngapi)

Fuatilia Tanzanite one (mgodi wa Tanzanite) umeuzwa mara ngapi

Fuatilia Hotel ya Sheraton ikaja kuwa Royal Palm na sasa ni Serena umeuzwa mara ngapi kwa wamiliki wapya.

Sio jambo la ajabu kampuni moja kufikwa bei na kampuni nyingine. Mfano yote nimetoa ambayo iko ardhi hii hii ya 255
 
Kuna mazungumzo yanaendelea kuhusu kampuni ya uchimbaji madini ya BHP kutaka kuinunua kampuni ya uchimbaji madini ya Anglo America. Kwa Tanzania Anglo America inamiliki mgodi wa Geita Gold Mine maarufu kama GGM. Nchi nyingi zenye uwekezaji wa Anglo America ikiwemo Botswana South Africa zimetoa msimamo wao juu ya uwekezaji huo wa BHP.

Nasie watanzania tungependa kujua faida na athari iwapo BHP watainunua Anglo America. Ikumbukwe sekta ya madini ina mchango mkubwa katika upatikanaji wa fedha za kigeni ajira na biashara za wazawa na maamuzi yeyote yatakayo yanayoweza athiri sekta yetu ya madini ni vyema tukayatizama kwa jicho pevu.
Acquisition ni jambo la kawaida katika biashara ya kimataifa muhimu Sheria na maslahi ya Nchi yalindwe
 
Nasie watanzania tungependa kujua faida na athari iwapo BHP watainunua Anglo America. Ikumbukwe sekta ya madini ina mchango mkubwa katika upatikanaji wa fedha za kigeni ajira na biashara za wazawa na maamuzi yeyote yatakayo yanayoweza athiri sekta yetu ya madini ni vyema tukayatizama kwa jicho pevu.
Usingizi wa pono tuliolala wa Tz sijui ni laana au ninini!
 
shida ikwapi hapo?, Anglo anamiliki migodi mingi Duniani na BHP ni superpower pia, Serikali inahusikaje hapo kama kila contract kati ya GOT na Anglo inaendelea kama ilivyokuwa kwa BHP?
Kufungua macho ni jambo la msingi, japan hawana mgodi wa BHP wala Anglo lakini wanafuatilia kwa karibu hii biadhara, kwani deal hili kwa vyovyote lina trickle down effect
 
Kufungua macho ni jambo la msingi, japan hawana mgodi wa BHP wala Anglo lakini wanafuatilia kwa karibu hii biadhara, kwani deal hili kwa vyovyote lina trickle down effect
Japan na China no waathirika. Direct WA hili suala , maana wana sekta kubwa sana za heavy machinery and equipments manufacturing , ambapo metals kama copper ,chuma nk ndio man raw materials so BHP akitengeneza Monopoly anaweza pandisha bei ya hizo bidhaa sokoni kutokana na competition kuwa ndogo na kuongeza gharama za uzalishaji wa bidhaa za viwandani kama mitambo ,magari nk
 
Back
Top Bottom