Mauzo ya bidhaa zetu nje yapungua kwa 50%!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Ni habari za kusikitisha lakini lazima tuzisikie na kujua jinsi ya kutatua matatizo yetu.
Kulingan na The Guardian gazeti la leo 2/10/2017, mauzo ya bidhaa za viwanda vyetu kwenda nje ya nchi, yamepungua kwa 46,5% kaika kipindi hiki cha mwaka mmoja.

Hizi ni habari za kushitusha sana.

Maana yake ni kwamba mapato yatakuwa yamepungua na vile vile ajira zitakuwa za wasi wasi.
Kulingana na The Guardian, mauzo hayo yaliyopungua yanafikia Trilion 1.6($700 million).

Gazeti hili likikariri ripoti za Benki Kuu(BOT), toka May 2016 hadi May 2017 mapato yameshuka toka $1,516million hadi $ 811.4million.

Ingawaje sababu halisi za kushuka mapato haya hazijulikani, hata hivyo hili ni janga kubwa kwa uchumi wa nchi, hasa tukifikiria azama yetu ya kujenga uchumi wa viwanda.
 
Wewe ni Msaliti
unatetea wezi
 
Utawasikia wenye akili finyu, wakifurahia kwamba wafanya biashara walikua wapiga deal tu, sasa tutakua sawa wote.....................hii roho haitatuacha salama.
 
Halafu uchumi unakuwa kwa nasi ya 7%
 
Huwezi waona hapa hao, au ukiwaona watakuambia Chadema wamesababisha mauzo yameshuka au watakuambia biashara ya nje imepungua kwa sababu hakuna dili tena
Mkuu mimi mwana CCM na sifurahishwi na hali hii.
Tuachane na wale wanao propagate cheap politics.
Hali hii si kichocheo cha uchumi wa viwanda.
 

If this is true, then we're in for it.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…