Ni habari za kusikitisha lakini lazima tuzisikie na kujua jinsi ya kutatua matatizo yetu.
Kulingan na The Guardian gazeti la leo 2/10/2017, mauzo ya bidhaa za viwanda vyetu kwenda nje ya nchi, yamepungua kwa 46,5% kaika kipindi hiki cha mwaka mmoja.
Hizi ni habari za kushitusha sana.
Maana yake ni kwamba mapato yatakuwa yamepungua na vile vile ajira zitakuwa za wasi wasi.
Kulingana na The Guardian, mauzo hayo yanafikia Trilion 1.6($700 million).
Gazeti hili likikariri ripoti za Benki Kuu(BOT), toka May 2016 hadi May 2017 mapato yameshuka toka $1,516million hadi $ 811.4million.
Ingawaje sababu halisi za kushuka mapato haya hazijulikani, hata hivyo hili ni janga kubwa kwa uchumi wa nchi, hasa tukifikiria azama yetu ya kujenga uchumi wa viwanda.