Mauzo ya hatifungani ya CRDB Al-Barakah Sukuk yaingiza shilingi bilioni 125.4

Mauzo ya hatifungani ya CRDB Al-Barakah Sukuk yaingiza shilingi bilioni 125.4

President of China

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
34,781
Reaction score
94,550
Benki ya CRDB imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 125.4 na Dola za Marekani milioni 32.3 kupitia mauzo ya hatifungani yake ya CRDB Al-Barakah Sukuk, hatua iliyovuka malengo ya awali kwa zaidi ya asilimia 400.

Uuzaji huo uliofanyika kwa siku 40 kuanzia Agosti 9 hadi Septemba 19, 2025 umevutia zaidi ya wawekezaji 1,000, jambo linalotafsiriwa na wachambuzi kuwa dalili ya kuongezeka kwa imani na uhitaji wa bidhaa mbadala za kifedha zinazofuata misingi ya Sharia.

Baada ya mauzo kukamilika, CRDB Al-Barakah Sukuk imeorodheshwa rasmi katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Elijah Mwandumbya amesema mafanikio hayo yanaonyesha uimara wa sekta binafsi katika kuendeleza masoko ya mitaji na kuongeza fursa za uwekezaji kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, amesema mwitikio mkubwa ulioonekana ni ishara ya kuongezeka kwa uelewa wa huduma za masoko ya mitaji, hususan Sukuk kama chombo cha uwekezaji.

Ameeleza kuwa kiwango kilichokusanywa kinawakilisha asilimia 418 ya malengo ya uwekezaji kwa fedha za ndani na asilimia 646 kwa fedha za kigeni.


View: https://www.instagram.com/p/DRRqms4it4p/
 
Back
Top Bottom