James Kasonda
Member
- Apr 2, 2012
- 84
- 49
Mavazi aliyovaa Salma Msangi jana akiwa anatangaza kipindi cha TV kwenye Chanel Ten yanapotosha jamii kabisa, hasa mabinti wadogo wanaokua. Mtangazaji wa vipindi vya TV anapaswa kujiheshimu kimavazi akikumbuka kwamba yeye ni kioo cha jamii.
Salma alivaa kijisuruali cha Jeans kilichobana sana na kilichoraruliwa kwenye mapaja. Hii haikubaliki. Kama baadhi ya magazeti yamewahi kufungiwa kwa sababu mbalimbali basi huyu binti anapaswa kupigwa marufuku kutangaza vipindi vya TV. Na si yeye tu, hata hicho kituo cha Chanel Ten kinapaswa kufungiwa kwa muda kadhaa ili wajifunze maadili mema ya utangazaji.