JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Vaa aina ya mavazi yanayokuonesha kuwa ni nadhifu na uko makini 'professional' .
Kwa mwanaume unaweza vaa suti, au shati na suruali ya kitambaa, pamoja na kiatu cha kufunika cha kiofisi.
Mwanamke unaweza kuvaa blauzi na sketi nzuri, isiwe fupi au ndefu sana hadi kukuletea usumbufu, vilevile unaweza kuvaa suti. Epuka viatu virefu sana na vyenye kutoa sauti kubwa unapotembea.
Aidha, rangi ya nguo ya bluu, nyeusi na hudhurungi ni rangi ambazo zinapendeza zaidi kwenye Usahili.
Upvote
1