Mavugo si mchezaji wa Kumbeza. Tatizo alilo nalo ni la kisaikolojia na si Uwezo

Mavugo si mchezaji wa Kumbeza. Tatizo alilo nalo ni la kisaikolojia na si Uwezo

Sodoku

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2016
Posts
1,271
Reaction score
2,903
Kumekuwa na maneno mengi ya kumbeza mafugoal ambaye mpaka sasa ana mabao 4 kama sikosei. Lakini kiuhalisia ludit mavugo ni mchezaji mzuri mwenye nguvu na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira.

Tatizo lake kubwa ni tension na pressure aliyo nayo kutokana namna usajili wake ulivyofanyika na mategemeo makubwa ya wanasimba kitu ambacho kinamfanya ajione kama ana deni kubwa sana.

Hii imempa sababu ya kuwa na uchoyo au uchu wa kufunga na akasahau kuwa wakati mwingne anaweza akawa anatengeneza magol kwa wengine. Hii ni kawaida imewah wapata wachezaj weng akiwepo zidane na sasa pogba.

Wachezaj hawa wanaweza kusaidiwa na kocha pamoja na wapenzi wa team husika.wakija zoea huwa wanakuwa wachezaj wazuri sana. Hivyo nawashauri washabiki wa mpira ukiweka mbali usimba na uyanga. Tunamwona chirwa naye alivyochukua muda mrefu lakini sasa anaweza akazoea na tukamwona akifunga

Mchezaji wa aina hii ili afanye vizur anapaswa atulie asijichukulie kama yeye anabeba team nzima na ana deni kubwa sana kwa team husika. Hii hali inaondoa umakini.

Lakini atakapocheza kama mchezaji wa kawaida atakuwa makini na kuepusha makosa anayosemwa. Lakin pia kumekuwa na juhudi za makusudi za wachezaj wa ndani kuponda wachezaj wa nje waonekane hawana maana.hili nalo si zuri.tuwape muda wachezaji wote hawa kwa nafasi zao.
 
Ana shida moja kwa upande wangu ni mchoyo. Mchezaji si lazima ufunge wewe unaweza kutoa assist na ukawika sana tu kocha amsaidie kwa hili aise.
 
Striker mpya Simba SC aja na rekodi za Ronaldo na Messi!!

Laudit Mavugo amekuja na rekodi ya kuwa na uwiano wa goli moja au zaidi katika mechi moja katika ligi kuu.

Katika msimu uliopita wachezaji waliokua na uwiano huo ni Christiano Ronaldo [CR7], Messi na "Tormentor" Laudit Mavugo.

CR7 alicheza mechi 38 akafunga goli 48, uwiano wake ni 1.4!

Messi alicheza mechi 38 akafunga goli 43, uwiano wake ni 1.2!

Laudit Mavugo alicheza mechi 28 akafunga goli 29, uwiano wake ni 1.04!

Ugonjwa wake ushapata dawa.. na sasa anatupia tu kama wachezaji wa kariba yake.. kina messi na CR7.. mpaka sasa mechi 4 goli 4, uwiano wake 1.0.
 
Back
Top Bottom