Mavunde Akabidhi Kompyuta na Printres kwa Shule 50 za Sekondari Jijini Dodoma

Mavunde Akabidhi Kompyuta na Printres kwa Shule 50 za Sekondari Jijini Dodoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MAVUNDE AKABIDHI KOMPYUTA NA PRINTER KWA SHULE 50 ZA SEKONDARI JIJINI DODOMA

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumekuwa na mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu nchini, ikiwemo ujenzi wa vyuo vya VETA, shule za msingi na sekondari, hatua ambayo imeondoa adha kwa wananchi kuchangishwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule.

Mhe. Mavunde ameyasema hayo Machi 10, 2025, katika Shule ya Sekondari Viwandani alipokuwa akikabidhi kompyuta na printer kwa shule 50 za sekondari zilizopo Jijini Dodoma, sambamba na kuzindua maabara ya kisasa ya chumba cha kompyuta na kugawa kompyuta kwa ofisi zote za kata 41 zilizopo ndani ya Jiji la Dodoma.

Waziri Mavunde amebainisha kuwa ongezeko la shule limeleta matokeo chanya katika kuboresha elimu jijini Dodoma.

“Tumeanza kuona matunda ya kazi iliyofanyika, Shule za msingi na sekondari zimeongezeka sana, Nyie ni mashahidi—shule za msingi zilikuwa 96, lakini leo tuna shule 107, ndani ya miaka miwili pekee, shule mpya 11 zimejengwa,” amesema Mhe. Mavunde.

Waziri Mavunde ameeleza kuwa kompyuta hizo zitakuwa na nyaraka muhimu kwa wanafunzi, ikiwa ni pamoja na mitihani ya taifa iliyopita ya kidato cha pili, kidato cha nne, na kidato cha sita kuanzia mwaka 1988 hadi 2024.

“Kompyuta hizi zitakuwa na mitihani ya taifa iliyopita ya kidato cha pili, kidato cha nne, na kidato cha sita kuanzia mwaka 1988 mpaka mwaka 2024. Hii itasaidia wanafunzi kujifunza kwa urahisi na kwa ufanisi zaidi,” amefafanua Mhe. Mavunde.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Viwandani, Mwl. Ester Simchimba, amemshukuru Mhe. Mavunde kwa mchango wake mkubwa katika kusimamia taaluma na kuboresha miundombinu ya elimu jijini Dodoma.

“Mheshimiwa Mavunde amekuwa mdau mkubwa wa elimu hapa Dodoma. Amehakikisha mazingira ya kujifunzia yanaboreshwa na taaluma inaendelea kukua,” amesema Bi. Ester.

Ameongeza kuwa, kwa jitihada za serikali ya awamu ya sita pamoja na mchango wa Mbunge Mavunde, azma ya elimu bure yenye mazingira safi na rafiki kwa wanafunzi imefanikiwa kwa kiwango kikubwa jijini Dodoma.
 

Attachments

  • GltTce3XEAAmGth.jpg
    GltTce3XEAAmGth.jpg
    154 KB · Views: 1
  • GltTdgoXAAAsRxE.jpg
    GltTdgoXAAAsRxE.jpg
    374.5 KB · Views: 1
  • GltTdpQXcAAvzNP.jpg
    GltTdpQXcAAvzNP.jpg
    253 KB · Views: 1
  • GltTdpFWgAEwgNg.jpg
    GltTdpFWgAEwgNg.jpg
    254.4 KB · Views: 1
  • GltTdozWMAAkNsV.jpg
    GltTdozWMAAkNsV.jpg
    266.8 KB · Views: 1
  • GltTkjxXgAI_n-v.jpg
    GltTkjxXgAI_n-v.jpg
    228.4 KB · Views: 1
  • GltTkjeWYAA0x52.jpg
    GltTkjeWYAA0x52.jpg
    312.8 KB · Views: 1
  • GltTkjtXYAAyoW_.jpg
    GltTkjtXYAAyoW_.jpg
    345 KB · Views: 1
  • GltTkjNWAAA2bS9.jpg
    GltTkjNWAAA2bS9.jpg
    366.6 KB · Views: 1
Back
Top Bottom