Mavunde azindua rasmi shughuli za uchimbaji madini mgodi wa Porcupine North- Chunya

Mavunde azindua rasmi shughuli za uchimbaji madini mgodi wa Porcupine North- Chunya

Mpepetaji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
346
Reaction score
213
Waziri wa Madini Anthony Mavunde amezindua rasmi shughuli za uchimbaji madini katika mgodi wa Porcupine North- uliopo Makongorosi Wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya unaomilikiwa na Kampuni ya Shanta Gold Mining Limited na kusema kuwa hatua hiyo ni matunda ya uamuzi wa Serikali kurudisha leseni ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha unawekwa utaratibu mzuri wa kuongeza mapato ya nchi kupitia sekta ya madini.

Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Aprili 03, 2025 katika hafla ya Uzinduzi wa Shughuli za Uchimbaji Madini Porcupine North – Kata ya Mkola, Makongorosi Wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya.

“Eneo hili ni eneo ambalo Leseni hodhi zimerudi serikalini kwa mujibu wa sheria. Baada ya kumalizika shauri la kimahakama na mwekezaji wa awali,serikali iliweka utaratibu wa wazi kumpata mwekezaji atakayeendesha eneo hili la uchimbaji na Kampuni ya Shanta Gold Mining Limited ilishinda kwa masharti ya kuanza uchimbaji ndani ya miezi 18,ambapo mashapo yaliyothibitishwa kwa sasa yanafikia wakia 110,000 na upo uwezekano baada ya utafiti zaidi kufikisha mashapo ya wakia 400,000 ambazo kupitia mrabaha,kodi na tozo mbalimbali zitasaidia kuongeza makusanyo ya Serikali” amesema Mavunde

Aidha, Waziri Mavunde amesema kuwa, Leseni moja iliyokuwa katika eneo la Saza, Mkoa wa Songwe, imekabidhi kwa wachimbaji wadogo ili kuhakikisha kundi hilo linanufaika na rasilimali za madini na kwamba eneo hilo la Saza lililokabidhiwa kwa Wachimbaji Wadogo, linakadiriwa kuwa na mashapo ya dhahabu yenye wakia laki mbili, thamani yake ikiwa ni takriban shilingi trilioni 1.2 kwa bei ya sasa ya dhahabu.
1743754722052.png
1743754739649.png


Chanzo Nipashe
 
Back
Top Bottom