Mavunde Azindua SACCOS ya Waendesha Pikipiki na Bajaji Dodoma

Mavunde Azindua SACCOS ya Waendesha Pikipiki na Bajaji Dodoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

MAVUNDE AZINDUA SACCOS YA WAENDESHA PIKIPIKI NA BAJAJ DODOMA.​

▪️Atoa rai SACCOS kuwainua Vijana kupitia mkopo wa Asilimia 10

▪️Ataka Vijana wamiliki vyombo vyao vya usafiri

▪️Wampongeza Rais Samia kwa ujenzi wa ofisi ya Waendesha Pikipiki na Bajaj Dodoma(UMAPIDO)

Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amezindua Ushirika wa waendesha Pikipiki na Bajaj Dodoma na kuwataka wasafirishaji hao kutumia fursa hiyo kujiimarisha kiuchumi kupitia mikopo mbalimbali.

“Ninawapongeza kwa uamuzi huu wa kuanzisha SACCOS yenu,ni wakati muafaka sasa kuwaona vijana mkimiliki vyombo vya usafiri vya kwenu wenyewe.

Kupitia SACCOS hii vijana wengi watabadilisha maisha yao na kujijenga kiuchumi.

Nitoe rai kwa viongozi wa SACCOS kuhakikisha mnatumia vizuri mkopo wa asilimia 10 wa mapato ya ndani ya Jiji la Dodoma ambapo mpaka sasa zimetengwa shilioni Bilioni 7 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya wakina mama,vijana na watu wenye ulemavu”Alisema Mavunde

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaj Jabir Shekimweri anewataka maafisa wasafirishaji hao kutumia SACCOS kutatua changamoto za msingi za kiuchumi za vijana wengi na kuahidi kwamba serikali itakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha inaweka mazingira rafiki ya ufanyaji wa shughuli zao.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma SACP George Katabazi amewataka maafisa wasafirishaji hao kuzingatia sheria za usalama barabarani na kwamba Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana nao kwa karibu kama wadau muhimu wa usalama katika jamii.

Akitoa shukrani zake Mwenyekiti wa UMAPIDO Ndg. Marwa Chacha Nyagate ameshukuru Mh. Rais Dkt. Sania S. Hassan kwa kuwajengea ofisi za chama hicho mkoani Dodoma na pia kumshukuru Mbunge Mavunde kwa mchango wa Tsh 15,000,000 kuiwezesha SACCOS yao kuanzishwa na kuahidi kwamba wataitumia SACCOS kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa vijana wote waliopo kwenye tasnia hiyo.

Mwenyekiti Marwa pia alisisitiza umuhimu wa vijana hao kushiriki uchaguzi mkuu 2025 ili kutimiza takwa la kikatiba.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.01.jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.01.jpeg
    97.8 KB · Views: 43
  • WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.02.jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.02.jpeg
    114.3 KB · Views: 44
  • WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.02 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.02 (1).jpeg
    184.1 KB · Views: 39
  • WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.02 (2).jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.02 (2).jpeg
    105 KB · Views: 37
  • WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.03.jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.03.jpeg
    136.9 KB · Views: 43
  • WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.03 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.03 (1).jpeg
    117.1 KB · Views: 40
  • WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.04.jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.04.jpeg
    78.1 KB · Views: 41
  • WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.04 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.04 (1).jpeg
    151.9 KB · Views: 35
  • WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.05.jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.05.jpeg
    163.4 KB · Views: 34
  • WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.05 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.05 (1).jpeg
    171.3 KB · Views: 37
  • WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.04 (2).jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-12 at 10.49.04 (2).jpeg
    96.2 KB · Views: 33
kuahidi kwamba wataitumia SACCOS kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa vijana wote waliopo kwenye tasnia hiyo.

Wanazidi kuchafua miji kwa kuleta cartels za bodaboda na bajaj

Miji ya kusini mwa Afrika Lusaka, Harare n.k haina aina hii ya usafiri, na raia wanaendelea na harakati za kiuchumi na kijamii bila shida yotote.
 
Back
Top Bottom