PreGE2025 Mavunde: Nawapatia Bima ya Afya Walimu wangu, atangaza Miradi ya maendeleo Mazengo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa Madini na Mbunge wa Dodoma mjini amewapatia Waalimu WA shule ya Msingi Mazengo jijini Dodoma bima ya Afya yenye Thamani ya shilingi Milioni 3 kila Mmoja.

Soma, Pia: Mavunde Akabidhi Kompyuta na Printres kwa Shule 50 za Sekondari Jijini Dodoma

Akizungumza leo katika hafla ya Ugawaji wa Vifaa vya masomo kwa watoto yatima na watoto waishio kwenye mazingira Magumu wa shule ya msingi zote dodoma mjini amesema kuwa lengo la kuwapia waalimu hawa bima za afya zamani hawakukuwa na Bima za Afya kwahiyo walikuwa hawana kabisa bima za afya

Ameongezea kuwa "Tutaanza ujenzi wetu wa Uzio katika shule yetu ya Mazengo jijini Dodoma na kwa kuanzia nitachangia matofali Elfu Tano 5000"

"Nitawawaletea pia viwanja vya michezo na nitaanza na kiwanja cha basketball na kiwanja cha mpira wa miguu na wiki ijayo nitaleta magoli"
amesema mhe Anthony perer Mavunde Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini.

Huu nao ni utapeli walimu Wana bima inayokatwa moja kwa moja kwenye mishahara yao? NHIF huu siyo uhuni kweli?
 
Ha ha haaaa...

Huyu Mh. Mavunde ni tapeli kabisa..

Walimu mbona wanazo bima.

Badala ya ku-deal na shida ya Maji pamoja na Migogoro ya Ardhi iliyoshamiri Kila Kona ya Jimbo la Dodoma yeye anakuja na porojo.
 
Waalimu wote na wafanyakazi wa serikali wanatumia bima ya NHIF pamoja na familia zao. Na fedha inakatwa moja kwa moja kwenye mishahara yao? Mavunde atuambie vizuri; Hii tunaijua.
 
Waziri wa Madini na Mbunge wa Dodoma mjini amewapatia Waalimu WA shule ya Msingi Mazengo jijini Dodoma bima ya Afya yenye Thamani ya shilingi Milioni 3 kila Mmoja.

Soma, Pia: Mavunde Akabidhi Kompyuta na Printres kwa Shule 50 za Sekondari Jijini Dodoma

Akizungumza leo katika hafla ya Ugawaji wa Vifaa vya masomo kwa watoto yatima na watoto waishio kwenye mazingira Magumu wa shule ya msingi zote dodoma mjini amesema kuwa lengo la kuwapia waalimu hawa bima za afya zamani hawakukuwa na Bima za Afya kwahiyo walikuwa hawana kabisa bima za afya

Ameongezea kuwa "Tutaanza ujenzi wetu wa Uzio katika shule yetu ya Mazengo jijini Dodoma na kwa kuanzia nitachangia matofali Elfu Tano 5000"

"Nitawawaletea pia viwanja vya michezo na nitaanza na kiwanja cha basketball na kiwanja cha mpira wa miguu na wiki ijayo nitaleta magoli"
amesema mhe Anthony perer Mavunde Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini.

Cheap politics za ulaghai.

Mwalimu ni mfanyakazi wa serikali, kila mfanyakazi wa serikali ni lazima ajiunge na mfuko wa bima NHIF na hela inakatwa kwa lazima na automatically mara tu mfanyakazi akianza kulipwa mshahara hata kama hajajaza fomu ya kupata kadi ya bima.
 
Back
Top Bottom